Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Willibrod Slaa.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Willibrod Slaa amesema anakwenda Marekani pamoja na familia yake kwa mapumziko.
Hata hivyo, taarifa zinasema Dk. Slaa amekwishandoka nchini kuelekea Marekani pamoja na familia yake tangu jana jioni.
Huku akiwa Marekani kupumzika na kujiendelea katika kozi fupi katika tasnia ya Sheria na Lugha, Dk. Slaa amesema nyumba yake itakuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa leo asubuhi na kituo cha televisheni cha Azam, mwanasiasa huyo amesema akiwa mapumzikoni Marekani, nyumba yake itakuwa inalindwa na Jeshi la Polisi kutokana na vitisho ambavyo amekumbana navyo tangu alipoamua kuachia ngazi Chadema.
“Ninatishiwa maisha, ni lazima nichukue tahadhari….., ninatishiwa kupigwa mawe. Ni kweli ninalindwa na usalama,” amesema Slaa akiwa anahojiwa na mwanahabari nguli, Tido Mhando.
Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye ameshawahi kuwa mbunge wa Karatu mkoani Arusha amesema anashangazwa na taarifa zinazoenea kuwa amelala katika hoteli ya kifahari ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhoji wakati wa uchaguzi mkuu, 2010, alilala mahali hapo lakini hakuna aliyehoji.
Kuhusu gharama alizotumia kufanya mkutano na wanahabari katika hoteli ya Serena, Dk. Slaa amesema, alipoenda Marekani katika ziara ya kichama, alizuru majimbo 13 na hakutumia fedha za Chadema bali marafiki zake ambao hakuwaweka bayana.
Dk. Slaa amesema licha ya kuwa ng’ambo katika kipindi hiki muhimu kwa taifa, ataendelea kufuatilia yanayojiri nchini. Ameahidi kurudi kupiga kura muda ukifika.
MWANANCHI
7 comments:
NENDA NENDA MSALITI WEE KUMBUKUMBU ZA WASALITI WA TANZANIA HAZITAKUA ZIMEKOSEWA KWA WEWE KUTAMKWA KUWA KINARA WA WASALITI WA MABADIRIKO YA KIDEMOKRASIA TANZANIA.KATIKA ORODHA YA VINARS WA USALITI ILI KUIHUFAISHA CCM[SIKIO LA KUFA] WA PILI NI PROFESA LIPUMBA WA TATU NI CHRISTOPHER MTIKILA NA WA NNE NA WA MWISHO KWA WASALITI WA DARAJA A+ NI ZITTO KABWE.HAWA WATU NI HATARI KULIKO HATA NAPE NAUYE
Huyu mzee aache za kuletwa. Huku US huwezi kupata ulinzi wa polisi kama wewe unakuja kutembea unless kama wewe ni Rais wa nchi nyingine au a top diplomat. Or unless kama wewe ni terrorist utawekwa chini ya ulinzi. Aache kuwadanganya watu hakuna cha ulinzi wa polisi wala nini. Na kama atakuwa na ulinzi wa polisi that's a long and a VERY expensive process.
Kachafua hali ya hewa lakini watu wamepulizia air fresher,speed 120 kwenye corner,mwendo mdundo.Baba slaa nenda katumie mkwanja uliopewa,alijaribu lipumba sembuse wewe?
Unaweza kusema cha kawaida kwa Slaa alichokifanya lakini amejiingiza kwenye matatizo makubwa sana kwanza kapoteza muelekeo wa kisiasa anasubiri aidha msaada wa CCM kama wakimkumbuka
Karibu sana marekani lakininujue unewasha na kuvhochea waTanzania waungie kusikotakikana lakini tisa kumi Mungu yupo kinacholengwa ambacho hata wewe mwenyewe ulikuwa unakitaka kitakuwa. Sisi tuliokwisha kukusikia tangu ukija kwa marafiki zako Marekani Marekani tunakuelewa zaidi. Sasa umekuja kwa mkono wa chama ingine wala hakuna ubishi. Ulinzi wa usalama nao??
Hata aende akhera hatujalishi yeye kimada wake
Mtu mzima kuwa muongo kuwa kiasi hiki
Tunajuta kukupa cheo kile
Mzee anaenda kula mihogo marekani, na kuamisha hela kwenye accounts mbalix2.amemsikia Sumaye ( aliyemwita Mr. Zero) kuwa atazirudisha hela zote zilizowekwa nje UKAWA ukichujua Dolla
Post a Comment