Mwanamuziki mkazi London, Freddy Macha, anatazamiwa kutumbuiza kwa ngoma na muziki wa gitaa, kwenye tafrija ndogo kutangaza na kuuza picha za watoto wa Kitanzania. Tafrija na maonesho yametayarishwa na wapiga picha watatu wa Kizungu, Amy Read, Evelina Moceviciute na Saraya Cortaville waliofanya kazi za kujitolea Mbeya vijijini mapema mwaka huu. Mauzo ya taswira yatatumika kusaidia maisha na elimu ya watoto hao hao waliopigwa picha. Mradi mzima unaitwa "Ahsante Children"...kutukuza na kutangaza lugha ya Kiswahili, Tanzania na wananchi Afrika Mashariki.
Onesho litafanywa mkahawa wa
The Chapel
St Margaret's House,
21 Old Ford House,
Bethnal Green,
Hackney, London E2 9PL.
Jumapili 4 Oktoba 2015.
Saa 11 na nusu jioni hadi 3 usiku.
HABARI ZAIDI
www.freddymacha.com/
Freddy Macha na ngoma. Picha ya Luis Tome Passarello

No comments:
Post a Comment