Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI, Mohammed Tibanyendela akizungumza na waandishi wa habari masuala mbalimbali ikwemo viongozi wa juu kufanya kikao kinyemela leo Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini,Thomas Nguma.
Kamishna wa Tanga wa NCCR-MAGEUZI, Ramadhan Manyeko akizungumza na waandishi wa habari juu ya kushiriki kikao cha jana cha utoaji taarifa nje ya utaratibu wa chama leo Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini,Thomas Nguma.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI,Mohammed Tibanyendela katika ofis za Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka
Na Chalila Kibuda
CHAMA cha NCCR-MAGEUZI kimesema
mkutano uliofanyika jana katika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho hawajajua lengo lake kutokana na kutokwepo kwa baraka
ya vikao kwa mujibu wa chama hicho.
Akizungumza leo na waandishi habari jana Mwenyekiti wa Baraza
la Wadhamini wa Chama hicho, Mohamed Tibanyendela amesema kuwa mkutano huo
hujafanyika kwa kufuata taratibu hivyo wanaamini kuwa walikuwa
wanazungumza masuala yao wenyewe na sio
masuala yanayohusiana na chama hicho.
Amesema kuwa Makamu Mwenyekiti na
Katibu ndio watendaji katika uendeshaji wa vikao vya chama lakini hadi
wanakwenda kuzungumza na waandishi wa habari hakuna taarifa ya maandishi katika
ofisi hiyo.
Tibanyendela amesema kama kumekuwepo
na manung'uniko katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) suala hilo
lingezungumzwa ndani ya vikao kutokana
na viongozi waliozungumza walikuwa wakishiriki katika vikao vya UKAWA.
Amesema kuwa kikao kinachotambulika
kilifanyika Septemba 16 katika ofisi ya chama lakini kufuatia na kikao cha jana
hakikuwepo hivyo watakwenda tafsri
katiba juu ya viongozi kuzungumza masuala ya chama bila kuwepo kwa vikao
vinavyotambuliwa kikatiba.
Aidha amesema kuwa katika harakati zozote lazima kutakuwa
na milima na tambalale yote haya ni kwa ajili ya kuitoa CCM madarakani.
Kamishina wa Tanga wa Chama hicho
,Ramadhan Mnyeko ambaye alikuwa katika kikao hicho amesema kuwa yeye aliitwa na
Mwenyekiti lakini alikuwa hajui anaitiwa nini katika hoteli ya Land Mark.
Amesema gharama za kuja Dar es
Salaam amejilipia mwenyewe kwani na
taarifa ya kufika alipigiwa simu na sio barua.
CHANZO: MICHUZI BLOG
CHANZO: MICHUZI BLOG
4 comments:
pesa ndio tatizo katika vyama hivi mwalimu nyerere aliviita vyama hivi kuwa ni "vyama vya ruzuku" sisi tunataka kuitokomeza ccm muda huu, wao wanatafuta malumbano ya kutumwa ili wapate ruzuku.
Mmechelewa ukawa ndio hiyo hata mkitoka hii leo chadema na cuf na atakae bakia wanatosha kutimiza lengo nyie mnaweza kutoka,kumbukeni hamna mgombea urais wala ubunge muda huruhusu na umesha fungwa sasa mnataka nini?
mdau.
Iringa.
Kuliko na moshi, ja kuna moto.Ni dhahiri kuwa hali ndani ya NCCR mageuzi si shwari.Na kwa mtazamo wa baadhi ya wadau nje na ndani ya chama huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa NCCR.
Busara kubwa inahitajika kuweka mambo sawa.
WAna NCCR, kamati iliyounda hili jambo hebu angalaieni kwanza Taifa la Tanzania, kwani na ninyi wenyewe lengo ni kuiondoa CHAMA TAWALA ILIYOTUNYANYASA SANA MIAKA 50! Sasa mkianza malumbano kipindi hiki kifupi cha kuingoa CCM kweli mnautaka upiinzani au labda mmegawiwa hela na CCM yenyewe ili mharibu mipango. Hebu tulizaneni ili basi nanyi mkaingia kwenye nguvu moja kwani nafasi si zitakuwepo nyingi tuu. Hebu wekeni nguvu pamoja! Msiipe kuendeleza utawala wa kidhalimu, mpeni nguvu mwenyekiti wenu aweze kuwavusha na wagombea wote mlio nao. MABADILIO TUNAYATAKA October 25, October 30 tunazungumza vinginevyo. Asanteni/
Watu wamechoshwa na uongo na tamaa ya viongozi wenu ndio maana wanaanza kuwastukia ingali mapema. Watu wameshindwa hadi sasa kuelewa sera za Ukawa nini kwani kila muongeapo mnapiga kelele tu kuwa shida yenu ni kuing'oa CCM kwenye madaraka. Kama kuing'oa CCM kwenye madaraka ndio sera baada ya hapo nini? Ikiwa wanachama na baadhi ya viongozi ndani ya Ukawa hawaelimishwi vizuri na hivyo wanashindwa kuona matumaini huko mbele matokeo yake yanaweza yakawa ndiyo chanzo ya hizi vurugu tunazoziona sasa ndani ya makundi haya yanayounga muungano huu. Vurugu kama hizi zikiachwa zikaendelee kwa muda mrefu bila suluhisho zitaathiri hata hiyo azma yote ya kutaka kuing'oa CCM. Matokeo yake ni kuwa azma hii itabaki kuwa ndoto na badala yake tutaona kusambaratika kwa upinzani mara tu baada ya tarehe 25 Oktoba 2015.
Post a Comment