Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.
Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.
Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.
Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.
Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.
Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.
Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.
“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.
“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”
Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.
Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.
Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.
Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.
Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.
Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.
“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.
Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.
Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.
“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.
Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.
CHANZO MWANANCHI
15 comments:
Mafisadi asilimia 75 wako ndaninya utawala bado! Swala hili.la Richmond tumelichoka waTanzania hatuhitajinkuendelea kulisikia. Vyema mzungumzie ESCROW na nani walihusika kikamilifu na mengine makubwa. Tunaona awamu B inaanza kichafuana na tusishangae yatakayotajwa yasije kuwa kichocheo cha kulumbana hadi kupigana. Tuendesheni Siasa ya utulovu na tutawakwamua vipi waTanzania. Taifa kwanza halafu siasa!!.
Embu acheni masihara, ukweli uwekwe mezani na ajulikane muhusika kuliko kutupiana mpira kama nyimbo za taarab hapa sio wakati muafaka. We need truth!!!!!!! na Skendo zote hadi ya mwisho za Pembe za ndovu.
Wezi wote wako kwenye mfumo mbovu wa ccm. Hakuna haja kutafuta mchawi, kila aishie ndani na tunguli ni mchawi. CCM tumewachoka kipya hamna hata mseme nini nyuma haturudi kura zote kwa Mhe. Lowassa.
Hivi tukiyasoma yaliyoandikwa tunayaelewa kweli au ndiyo kejeli tu za kuwa basi na sisi wacha tuaandike! Tundu Lissu amejibiwa kuwa mhusika wa Richmond yuko naye huko mikoani ni kitu gani ambacho hamjaelewa? Kwa wafuatiliaji wa blog hii na pia maandiko mengi kwenye vyombo vya habari tumesoma mengi kuhusu uhusiano wa Lowassa na Richmond bado tunataka tuelezwe kitu gani kingine zaidi!
Hakuna aliyekataa kuwa chama tawala kilikuwa kimegubikwa na mafisadi! Uzuri ni kuwa mafisadi hao sasa wanahama chama tawala kwa kasi kubwa baada ya kuona kuwa mirija yao imeanza kuziba na hivyo kukimbilia kwenye vyama vya upinzani ambako yanapata hifadhi yao mpya.
Angalieni kampeni za Morogoro jana Tundu Lisu kasema Richomond ni ya KIkwete hajababaika kuficha ukweli, na akasema kama anabisha Asogee na aiambie umma ya Watanzania
Pia nataka kujua kwa nini Twiga wakapanda ndege? tena first class wakati sisi wazalendo walala hoi malofa hela ya dala dala hatuna,richmond hata ikiwa ya lowassa na escrow iwe ya KIKWETE Tanzania tuna taka chama kingine kushika dola tatizo sio watu, mfumo ndio tatizo hata mwalimu nyerere angelikuwa hai basi ingelimbidi achague moja kutoka chama au kuwa fisadi.
mdau.
sokoni ilala.
Hapa inaelekea siku ya siku tutakuja toana macho mambo mengi yamefichwa na serikali haitaki kuyashughulikia iliyolengwa sasa nimkulazimisha usshindi kwa namna yeyote na kwa gharama yeyote ile kulinda mafisadi kwa kuilinda ilani. Tunusuru umeyufikisha pabaya!!
ILE Hatari ya kuanza kuchafuana inaanza hizi ni siasa au kampeni za hasiri huenda kutokana na mwelekeo mbaya unaoendelea kujitokeza. Vyema tukubali tusifanye hasira! TAIFA LA TANZANIA NA WATU WAKE KWANZA!/
Kwanini wanatuqmbia kuhusu Richmond ya miaka minane iliyopita kwanini hawaongei watu waliohuza nyumba za serikali.Escrow ambayo bado mbichi kabisa watueleze pembe za ndovu vipi zinavyoka Tanzania zinakwenda kukamatwa china,Kenya pia watwambie twiga zilizopandishwa kwenye ndege ni nania laiye zipandisha?watwambie vipi miaka hamsini ya Uhuru hadi sasa bado watu wanakunywa maji machafu vipi raia wanabahatisha kula hivi kabisa wagombea hamna hata huruma kuona wakina mama wakilala kitanda kimoja wakina mama watatu hadi wanne he mmeshindwa miaka hamsini je hivi mtaweza kwa sasa?au porojo ili mpate kula siyo kura
Kwanini wanatuqmbia kuhusu Richmond ya miaka minane iliyopita kwanini hawaongei watu waliohuza nyumba za serikali.Escrow ambayo bado mbichi kabisa watueleze pembe za ndovu vipi zinavyoka Tanzania zinakwenda kukamatwa china,Kenya pia watwambie twiga zilizopandishwa kwenye ndege ni nania laiye zipandisha?watwambie vipi miaka hamsini ya Uhuru hadi sasa bado watu wanakunywa maji machafu vipi raia wanabahatisha kula hivi kabisa wagombea hamna hata huruma kuona wakina mama wakilala kitanda kimoja wakina mama watatu hadi wanne he mmeshindwa miaka hamsini je hivi mtaweza kwa sasa?au porojo ili mpate kula siyo kura
Mwenyekiti hapa utakuwa umeteleza. Mbona ulikaa kimya muda wote wakati yeye anaonekana alijiuzulu kuilinda Serikali na Chama kisipoteze mwelekeo?? Tunakubea umalize huu muda wako mfupi uliobakia usiwaachie waTanzania simanzi la malumbano kwani watakaoumia ni wale wachovu!! Asante nadhani Rivchmond ilishayeyuka midomoni mwa waTanzania. Tunafikiria uchaguzi tuu na njaa kali.. Amani.
Ukisikia UTAPELI ndo huo iweje leo hii akamtaja mwizi wa Richmond wakati yeye alikuwa rais skendal hii ilipotokea? Kwa nini asimpeleke mahakamani kama anamjua mwizi wa Richmond...ukisikia siasa za maji TAKA ndo hizo!!
Yaani rais mzima badala ya kuchukua hatua unatuletea story za kijiweni? Kama rais una act kama mwananchi wa kawaida asiyekuwa na power, je wakuu wa idara husika unategemea watafanya nini? Ulichaguliwa urais utalii au uwatumikie watanzania?
Huu ni mchezo wa kitoto. Rais wa nchi anatakiwa awe na maamuzi magumu. Huyu wa KWETU sijui vipi. Sisi wananchi tumeanbiwa yeye ndio mhusika mkuu. i
Nadhani kiwete alisema EL hakuhusika ila ilikuwa ajali ya kisiasa, sasa leo unaleta porojo za kijiweni. Ni vyema watanzania kuamini TZ haikuwa na raisi kwa miaka 10 kama raisi akiwa jukwaani anaongea huu utumbo kama ni kusafiri na kutumia kodi ya wanyonge.
Post a Comment