ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 15, 2015

MAGUFULI; REKODI YAKE YA UCHAPAKAZI INAIBEBA CCM

Mhe. John Pombe Magufuli anayegombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa kwenye mkutano wa kampeni.


Harakati za uchaguzi nchini zipo katika kipindi muhimu cha kampeni ambapo mwaka huu wa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, Watanzania wameamka zaidi kwa kufuatilia na kusikiliza sera na vipaumbele vya wagombea mbalimbali wa nafasi zote kutoka vyama vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Ukitazama uchaguzi huu utaona kuwa nafasi ya urais ndiyo inayozungumziwa sana kwa sasa kwa kuwataja wagombea wawili wakubwa wanaochuana vikali ambao ni Mhe. John Pombe Magufuli anayegombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa anayegombea kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho ni moja kati ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Nguvu ya wawili hawa inapimwa na mambo mengi, mengine ni ya kishabiki lakini mengine ni ya kimantiki zaidi kwa maana ya rekodi zao kwa kipindi cha nyuma cha utumishi wao, kila mmoja akiwa serikalini.

Japokuwa ana historia ndefu ya kisiasa, wananchi wengi walianza kumfahamu Lowassa mwaka 2005 alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wadhifa ambao hakudumu nao kwani miaka michache baadaye alijiuzulu kwa tuhuma za ufisadi.

Kwa upande wa Magufuli, wengi walianza kumfahamu mwaka 1995 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato) kabla ya baadaye kuwa waziri kamili wa wizara hiyo aliyoitumikia kuanzia mwaka 2000 hadi 2005. Mwaka 2005- 2008 alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi huku akiendelea kuwa Mbunge wa Biharamulo Mashariki.

Mwaka 2008 alihamishiwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akiwa waziri kamili huku akiendelea na nafasi yake ya ubunge hadi mwaka 2010 ambapo kuanzia mwaka huo hadi hivi sasa alirudishwa tena kwenye Wizara ya Ujenzi.

Akiwa kote huko, Mhe. Magufuli aliweza kujitengenezea sifa kubwa ya uchapakazi kuliko mawaziri wengi wa kipindi chake. Sifa hiyo inatajwa kutokana na matukio kadhaa aliyoyafanya ambayo mpaka sasa yamebakia ndani ya vichwa vya Watanzania.

Moja ya matukio yaliyobaki ndani ya vichwa vya wengi ni lile la kukamatwa kwa meli ya Wachina ikiwa na tani 293 za samaki waliokuwa wakivuliwa kwa siri kwenye Bahari ya Hindi mwaka 2009 wakati huo Mhe. Magufuli akiwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Umaarufu wa sakata hilo ulisababisha samaki waliokamatwa kupewa jina la Samaki wa Magufuli huku kupitia wizara yake, serikali ikitangaza kuitaifisha meli na kugawa samaki hao wa taasisi mbalimbali za umma.

Tukio hilo ambalo liliamsha sifa za uchapakazi wa Mhe. Magufuli liliishia kwa kuachiwa kwa wafungwa hao 35 kwa amri ya Mahakama Kuu mwaka 2014, wakati huo Mhe. Magufuli akiwa waziri wa ujenzi ambapo akiwa huko aliwastaajabisha Watanzania baada ya kuwafukuza wafanyakazi wa vituo vya mizani wapatao 400 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kubaini suala la rushwa iliyokithiri.

Mbali na tukio hilo, Mhe. Magufuli, akiwa ndani ya wizara ya ujenzi amefanikiwa kukibeba chama chake kwa kujivunia idadi ya madaraja na barabara nyingi zenye kiwango cha lami zilizojengwa na serikali kupitia wizara hiyo huku yeye akiwa msimamizi mkuu asiyekaa ofisini pekee.

Kuna kipindi alilazimika kuwawajibisha makandarasi wavivu waliokuwa hawakamilishi ujenzi katika muda uliopangwa na wale wanaokamilisha kwa kiwango cha chini bila kusitasita.

Wapo wanaobeza kishabiki uwezo wa Mhe. Magufuli kwa kumfananisha na wagombea wengine lakini kwa wale wanaotumia jicho la tatu kumtazama mgombea huyu watagundua kuwa ni mtu mwenye karama ya kipekee ya uongozi uliotukuka kwa kuwa mtu asiyependa majivuno, asiye na makundi, mnyenyekevu na mchapakazi anayefuata kanuni na sheria bila kuyumbishwa kirahisi.,

Utakumbuka sakata la bomoabomoa liliyoikumba nyumba ya meneja wa TANROADS iliyokuwa Ubungo na jinsi alivyotaka kuigharimu serikali kwa kutaka kubomoa jengo la Tanesco, Ubungo kwa kuwa limejengwa ndani ya hifadhi ya barabara.

Sifa zake ni nyingi ambazo nikisema nizitaje zote, kurasa hazitatosha lakini kwa kifupi, ipo wazi kwamba utendaji wake wa kazi uliotukuka ndani ya serikali za awamu zote alizowahi kuzitumikia, ni hazina nzuri kwa chama chake na yeye mwenyewe na kama Watanzania wataachana na ushabiki usio na mantiki, watamchagua kuwa rais kwani anazo sifa na vigezo vingi kuliko mgombea mwingine yeyote.

GPL

10 comments:

Anonymous said...

As long as huyu Magufuli yuko ccm, it doesn't make any difference ni kwamba yuko katika chama cha uozo. Mabadiliko yanatakiwa na wananchi wa kawaida walio wengi wamepoteza imani na ccm kabisa. Wewe hata ukinandika vitabu milioni moja vya hadithi ya sifa za Mzee Pombe, ccm hatukitaki. Niko tayari kuipigia jiwe kura but not ccm tena. Magufuli angekuwa anatokea chama kingine, ninaweza kidogo nikabadilisha mawazo yangu. Lakini akiwa ccm, mimi na tulio wengi sahau mwaka huu ccm. Zaidi cha kukusikitisha wewe mwandishi, nikwambie tu mimi bado mwanachama wa ccm lakini nimepoteza imani nayo. Magufuli nampenda lakini simpi kura yangu kwa sababu siitaki ccm ishinde.

Anonymous said...

Inatuwia taabu kutathmini uwezo wako wa kufiria.

Anonymous said...

Geeeeez!! Wewe Anoy hapo juu. Who gave you the authority to speak on behalf of all Tanzanians -toa mada sio talking points za Ukwawa. EL reminds me of Donald Trump candidancy.. Let us see.

Anonymous said...

HIZO RECORD UNAZIJUA WEWE. MZEE WA NGUVU MPYA ARI MPYA NA MAISHA MAPYA AMEISHIA WAPI ZAIDI YA KUONGEZA MAFISADI. MWENYE MACHO AAMBIWI TAZAMA.

Anonymous said...

Jamani kukaa ulaya tabu sana. Hiyo comparison ya EL na Trump wapi na wapi?

Anonymous said...

Under what basis do you relate between the two? One is outspoken, the other hmmm.
Trump's wealth is accountable the other not..
One is a failed government official who was forced out of office due to corruption the other not ..

Anonymous said...

Kwani Kati ya CCM na UKAWA ipi ilioza? Mimi naona ukawa sio kuna uozo tu bali kuna vimelea vya maradhi ndani ya ukawa na chadema. Kwanini Dk slaa kakimbia? Kwanini Ibrahim lipumba kakimbia? Kwanini lowasa na ukawa hawataki kulizungumzia suala la rushwa jibu rahisi yeye mwenyewe binafsi Lowasa amepita kuwa mgombea pekee wa uraisi wa ukawa kwa njia ya rushwa na ndio maana akina Dk slaa na lipumba kisa cha kukasirika na nakuahudi kabla ya kampeni kumalizika lowasa na lipumba watakuja kutoka hadharani kulielezea hili la lowasa kutoa rushwa ili mtu mwengine yeyote asiruhusiwe kugombea uraisi isipokuwa yeye tu mtabaki kutoa tuhuma zisokuwa na mshiko kuwa wamenunuliwa na CCM. Sasa kama mgombea mwenyewe wa uraisi kapatikana kwa njia ya rushwa kipi kinachoipa uhalali ukawa na chadema kuwa chama safi mbele ya watanzania? Watanzania tumechoshwa na ubabaishaji na uongo uliokisiri ndani ya ukawa magufuli ni chaguo letu .

Anonymous said...

Hapa Kazi tu#

Anonymous said...

Jamani hivi tunachagua mtu au Chama? Naomba nielimishwe kidogo! Maana naona mmeniacha njia panda! So Kama ni chama kweli Ccm watanzania Wengi wamekuwa hawaipendi kwa sababu ya maendeleo ya pole pole, Lakini Kama ni mtu wa kuiongoza nchi yetu hakuna mwingine tena Kama Magufuli! Watanzania wenzangu Kama kweli tuko serious!!

Anonymous said...

Nashukuru mwandishi wa habari hii kwa uchambuzi wako na uwekaji bayana ufanisi wa kazi wa wagombea hawa wawili. Pamoja na kuwa uchambuzi wako unatokana na mawazo yako binasfi lakini hata mimi kwa hili naunga mkono. Kama kweli Watanzania wote tutafanya uchambuzi wa kina na mahili kama huu bila kujali ushabiki au mwelekeo wetu kichama au mgombeaji hakika tutakuwa na fursa nzuri ya kumchagua kiongozi atakayeiletea maendeleo nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania.