ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 24, 2015

MAHUJAJI ZAIDI YA 700 WAFA KWA KUKANYAGANA WAKITEKELEZA IBADA YA HIJA

Profesa Ibrahim Lipumba, akisalimiana na Hujaji mwenzake kwenye msikiti mkuu wa Mecca, Saudi Arabia, wakati wa ibada ya Hija.
KWA uchache Waislamu 717 wamefariki dunia kwa kukanyagana wakati wakitekeleza ibada ya Hija nje kidogo ya Maka (Mecca).
Watislamu wengine 863 wamejeruhiwa kwenye kadhai hiyo iliyotokea wakati Waislamu wanaoshiriki ibada ya Hija, walipokuwa wakitekeleza tendo la kumrushia mawe shetani.
Mkanyagano huo ambao umetokea kwenye daraja la bonde la Minna, kilomita chache kutoka mji mtakatifu wa Maka nchini Saudi Arabia ambapo takriban mahema 160,000, yanayohifadhi mamilioni ya waumini wa Kiislamu wanaoshiriki ibada ya Hija mwaka huu.
Tukio hilo lilitokea wakati makundi makubwa mawili ya watu, waliokuwa wakijiandaa kutekeleza moja ya matukio ya mwisho ya ibada yalipokutana kwenye “njia panda” (makutano ya barabara), Maafisa wa Saudi Arabia wameviambia vyombo vya habari leo Septemba 24, 2015
Mkanyagano huo uliacha mlundikano wa maiti na majeruhi kwenye mitaa huku joto kali likitawala eneo hilo, Picha za video zimeonyesha.

Zaidi ya waokoaji 4,000 wamepelekwa eneo la tukio ili kusaidia shughulia za uokoaji na kutoa huduma ya kwanza ambapo mamia ya watu waliojeruhiwea vibaya walichukuliwa kwa helikopta na wengine kwenye mamia ya magari ya kubeba wagonjwa.
Vifo hivyo ni vingi mmno kutokea kwenye eneo hilo kwa wakati kama huu, ambapo mnamo mwaka 1990, mahujaji 1,400 walifariki dunia baada ya kutokea mshtuko miongoni mwa mahujaji wakiwa kwenye njia ya chini ya kupitia kuelekea eneo hilo la kumrushia mawe shetani
Lakini pia ni tukio la pili kutokea katika kipindi hiki cha hija, ambapo mwanzoni mwa mwezi huu, zaidi ya watu 100 walipoteza maisha baada ya winchi kubwa lililokuwa kwenye eneo la ujenzi kwenye msikiti mkuu wa Maka, kukatika na kuangukia majengo na watu.
Watu wengine zaidi ya 200 walijeruhiwa kwenye tukio hilo.

4 comments:

Anonymous said...

Poleni sana ndugu zangu Waislamu kwa mkasa huu mkubwa. Mungu awape nguvu na kuwapokea waliofariki katika utukufu wake.

Anonymous said...

Mi naomba kueleweshwa kila mwaka ni lazima mahujaji wafe kwa kukanyagana, ina maana serikali ya hiyo nchi haijaweza kuwa na solution ya kuepuka hivo vifo kila mwaka au ndio mambo yetu yale

Anonymous said...

Shetani karudisha mawe,na ashindwe

Anonymous said...

mwana hizaya uliyetoa comment wa mwishooooo. hapo juu.watu wamekufa unaleta mzaha istidhai wewe.mwanahizaya mkubwa.na uangamiye kabisa.