ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 24, 2015

MJUE EDWARD LOWASSA MGOMBEA URAIS WA CHADEMA ANAYEBEBA BENDERA YA UKAWA

Edward Ngoyai Lowassa Alizaliwa Agosti 26, 1953,na kukulia Katika Kijiji Cha Ngarash huko Monduli,akiwa ni mtoto Mkubwa wa Kiume Kwa Mzee Ngoyai Lowassa.

Alisoma Shule Ya Msingi Ya Monduli (1967-1971), Shule ya Sekondari Arusha Kwa Kidato Kwa Kwanza hadi cha nne (1967-1971) na Shule ya Sekondari Milambo kwa kidato cha Tano Na Sita (1971-1973).

Ana Shahada ya Elimu na Sanaa kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam Aliyohitimu Mwaka 1977, Na Shahada ya Uzamivu Katika Maendeleo kutoka Chuo Kikuu Cha
Bath Nchini Uingereza aliyohitimu Mwaka 1984 Kwa udhamini Wa British Council.

Ni Mume wa Regina Lowassa na Wamejaliwa Watoto Watano, watatu wa Kiume Na wawili wa Kike.

Kikazi, Lowassa amekulia na kufanya kazi zaidi ndani ya CCM Na Serikali yake. Mara Baada ya Kumaliza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam aliajiriwa na CCM Kama Katibu Msaidizina baadaye Katibu
wa Wilaya. Alipata kuwa Msaidizi wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, Daudi Mwakawago Na Horace Kolimba.

Alifanya kazi pia Jeshini Sambamba na Rais Jakaya Kikwete Pamoja Na Abdulrahman
Kinana na Aliondoka Jeshini akiwa Na cheo cha Luteni.

Jambo moja ambalo watu Wengi hatukulijua kabla ni kwamba Lowassa Ni Miongoni mwa Wanasiasa Wanajeshi waliopigana Vita nchini Uganda mwaka 1978/1979.

Aliingia katika Siasa za serikali mwaka 1985
alipoteuliwa kuwa Mbunge kupitia Umoja Wa vijan UVCCM sambamba
na Anne Makinda na Jenerali Ulimwengu.

Akiwa bado Mbunge mwaka 1989 aliteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Cha Arusha (AICC) ambako alidumu hadi Mwaka 1990 alipochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Monduli hadi leo.

Baada ya Kushinda kura za Ubunge aliteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi Ya Makamu Wa
Kwanza wa Rais akishughulikia Mahakama na Bunge 1990-1993, na Baadaye aliteuliwa kuwa Waziri Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mijini 1993-1995.

Mwaka 1997 aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa
kuwa Waziri Katika Ofisi ya Makamu wa Rais akishughulikia Mazingira na Umasikini.
Mwaka 2000 hadi 2005 alikuwa waziri wa Maji naMaendeleo ya Mifugo.
Aliteuliwa na Rais Kikwete Kuwa Waziri Mkuu
Desemba 30, 2005, Nafasi aliyodumu nayo hadi
Februari 7, 2008 alipojiuzulu kwa kile kinachojulikana kama kashfa ya Richmond.

5 comments:

Anonymous said...

HUYU NDIYE RAIS WETU MPENDWA,MTARAJIWA WA AWAMU YA TANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA KIRAIA UNAOTARAJIWA KUFANYIKA TAKRIBANI SIKU THELATHINI ZIJAZO YAANI MWEZI MMOJA TOKA LEO TAREHE 25 OCTOBA 2015.PAMOJA NA KUPITIA HUJUMA,NJAMA,VITISHO NA MAPINGAMIZI LUKUKI KUTOKA CHAMA DOLA TAWALA CHA CCM,KILICHOOITAWALA NCHI TANGU UHURU,MIAKA 55 ILIYOYOPITA,MHESHIMIWA LOWASSA AMEZIDI KUPAISHWA NA KUUNGWA MKONO NA MAMILLION YA WATANZANIA WALIOKUWA NA WENYE HAMU KUBWA YA MABADIRIKO.MWANZILISHI WA HARAKATI ZA UKOMBOZI NA UHURU WA MAREKANI BENJAMIN FRANKLIN [JAN 17,1706 TO APRIL 17,1790] ALIWAHI KUSEMA 'GROWTH MEANS CHANGE AND CHANGE INVOLVES RISK,STEPPING FROM THE KNOWN TO THE UNKNOWN'.SASA HIVI UMAARUFU NA KUKUBALIKA KWA MHESHIMIWA LOWASSA KUNASIMAMIA KWENYE ASILIMIA 80 [80%] MAIN THEME YA WATANZANIA KWA SASA:'LOWASSA MABADIRIKO,MABADIRIKO LOWASSA'.

Anonymous said...

Tunashukuru kwa kutusimulia ndoto yako.Endelea kuota tutakuamsha 25/10/2015.

Anonymous said...

Change within CCM is what people are looking for. By the way can you post a recently taken photo of your candidate!

Unknown said...

SIFA STAHIKI WATANZANIA TUNAZOHITAJI KWA MGOMBEA ANAEWANIA NAFASI YA KAZI YA URAISI WA AWAMU YA TANO YA JAMHURI YA TANZANIA NI KAMA IFUATAVYO

Watanzania tunataka raisi mwenye angalau PHD
katika kiwango chake cha elimu. Mtu genius kama john pombe magufuli. Mchapa kazi kama maghufuli. Muadilifu kama maghufuli. Ananguvu na afya ya kufanya kazi kwa muda 24/hours bila ya kuchoka kama maghufuli. Watanzania tunataka raisi si mkabila kama maghufuli. Tunataka raisi ambae anatoka katika chama kisicho na muonokano wa ukanda kama chama cha magufuli. Watanzania tunataka raisi mwenye mali ambazo akiulizwa amezipata vipi awe na majibu sahii kama ya magufuli. Watanzania tunataka raisi asie mdini na asiepita makanisani kuhubiri siasa kama maghufuli. Watanzania tunataka raisi mwenye CV safi ya maisha yake ya kazi isio na maswali kama maghufuli. Watanzania tunataka raisi tutakae mkabidhi nchi yetu na rasili zake pamoja na mikataba mihimu ya gas, mafuta, madini kwa mtu asie na sifa mbaya ya ufisadi na udokozi kama magufuli. Watanzania tunataka kumkabidhi uraisi kwa mtu ambae asiefikiri kwamba kwa kuwa rafiki yake kawa raisi basi na yeye anastahiki kuwa raisi hata kama kuna watu waliomzidi kisifa stahiki ya kushika nafasi ya juu ya kazi ya nchi. Na kwa Tanzania hakuna kama maghufuli raisi mstahiki mtarajiwa wa Tanzania.

Anonymous said...

Kwa kuwa hakuna chama cha siasa kinachoitwa UKAWA nchini Tanzania tusidanganyike kuwa LOWASSA ni wa UKAWA; ni wa CHADEMA. Ukawa unatumiwa na CHADEMA kama "a trojan horse" tu. Kimbunga kikiisha baada ya uchaguzi mkuu, takatataka zote zitaanza kuanguka chini ki-vyama vya UKAWA. Endapo Chadema kitashinda, CHADEMA kitaamua kutwaa yote na kuwa CHADEMA. Hata hivyo, UKAWA sio starter Bungeni bila kuwa na wabunge zaidi ya CCM ambao wanaweza kuweka break kiasi cha kuishinda UKAWA bungeni. Endapo CCM kitashinda, ndio mwisho wa UKAWA na kusambaratika kwa vyama vya upinzani!