Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akimnadi mgombea Ubunge pamoja na madiwani katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Arusha mjini tarehe 5/9/2015 katika uwanja wa soko kuu jijini Arusha.(Picha zote na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha).
Umati wa watu uliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM jimbo la Arusha mjini katika eneo la soko kuu jijini Arusha, ambapo rasmi walizindua kampeni za ubunge na udiwani
Mbunge jimbo la Arusha mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Philemon Mollel maarufu kwa jina na Monaban akimwaga sera zake katika uzinduzi huo ambapo alikiri kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo endapo ataibuka mshindi katika uchaguzi mkuu.
Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Ferooz Bano ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi akiongea katika mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera Mahusiano na Uratibu Dkt.Mary Nagu akisalimiana na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za CCM jimbo la Arusha mjini tarehe 5/9/2015 katika eneo la soko kuu jijini Arusha.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa kutoka Arusha mjini, Godfrey Mwalusamba akiongea katika uzinduzi huo.
Mbunge viti maalum kundi la wanawake (UWT), Catherine Magige Mkoa wa Arusha akizungumza katika uzinduzi huo.
Mbunge viti maalum na Kada maarufu kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Violet Mfuko akiongea katika uzinduzi huo.
Aliyekuwa dereva wa Mbunge, Lema Shubet akiongea jukwaani alisema hamuogopi lema kwa kuwa mbinu zake zote anazijua hivyo hawezi hata kuua mende nyumbani kwakwe licha ya kumtangazia atamtumia majambazi nyumbani kwake.
Mwigizaji maarufu wa sauti za viongozi mbalimbali Oscar Nyerere akichekesha katika uzinduzi huo.
Mbunge mstaafu kupitia CCM jimbo la Longido, Lekule Laizer maarufu kwa jina la “kiboko wa wapinzani” akiongea katika uzinduzi huo, aliwataka wananchi wa Arusha kumchagua Monaban kwakuwa ni kiongozi muadilifu mwenye sifa ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
Mh.Phidesia Mwakitalima kulia anasema CCM mbele kwa mbeleeeeeeeeee!
Meza kuu.
Mwenye miwani aliyekaa chini pamoja na wananchi Mustafa Panju ambaye alikuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika kura za maoni akifwatilia uzinduzi huo.
Mustafa Panju ambaye alikuwa mgombea wa Ubunge kupitia CCM katika kura za maoni akiagana na wananchi baada ya kumaliza kampeni hizo.
No comments:
Post a Comment