ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 10, 2015

MKUTANO WA WAGOMBEA UWAKILISHI ZANZIBAR KUZUNGUMZIA MAADILI YA UCHAGUZI MKUU

 Mkuu wa Utawala na Uendeshaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndg Saadun Ahmed, akitowa maelezo ya Mkutano na Wagombea Uwakilishi wa Majimbo ya Unguja kutowa maelezo ya Mkutono huo ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutowa elimu ya maadili ya uchaguzi na kuwepo kwa amani katika kipindi cha uchaguzi Zanzibar. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa salama bwawani Unguja.
Waheshimiwa Wagombea Uwakilishi katika Majimbo ya Unguja wakiwa katika ukumbi wa Salama.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibae Ndg Salum Kassim Ali akizunhgumza wakati wa mkutano wa Ufunguzi wa Mkutano huo na Wagombea Uwakilishi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Maadaili Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Nassor Khamis Mohammed kutowa mada kuhusiana na kufuatwa kwa maadili ya Uchaguzi wa Zanzibar yaliosainia na Viongozi wa vyama vyao.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Mhe Nassor Khamis Mohammed akitowa Mada kuhusiana na Maadili kwa Wagombea Nafasi za Uwakilishi Zanzibar katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli Zanzibar.
Washiriki wa Mkutano huo wakipitia makabrasha ya Maadili yanayotakiwa kuzingatiwa wakati wa Kampeni na Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wakati iliwasilishwa na Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Wagombea wakifuatilia Mada hiyo wakati ikiwasilishwa katika mkutano huo ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuzungumzia Maadili wakati wa Kampeni na Upigaji wa kura Zanzibar. 
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Mhe Nassor Khamis Mohammed akizungumza wakati wa mkutano huo na Wagombea wa Uwawakilishi Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar
        Wagombea Wakifuatilia kwa makini Mada ya Maadili ya Uchaguzi wakati ikiwasilishwa.
             Wagombea Wakifuatilia mkutano huo wa  Tume kuhusiana na Maadili.
Wagombea Wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatili mkutano huo wakati wa kuwasilishwa kwa mada mbili za Maadili ya Uchagu na Rushwa .
Afisa Sheria wa Mamlaka ya Kuzuiya Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZECA) Ndg Abubakar Mohammed Lunda akitowa Mada kuhusiana na miaya ya Rushwa wakati wa Mkutano huo mna Wagombea wa Uwakilishi ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar na kuwashirikisha Wagombea wote wa Uwakilishi Unguja uliofanyika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
      Wagombea wakiwa makini kufuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano huo.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kwamtipura Mhe Hamza Hassan Juma akiuliza swali kuhusiana na mahusiano ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar na ile ya Bara wakati wa mkutano huo wa Maadili 
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Nassor Mohammed akiuliza swali kuhusiana na kuzungumziwa kwa Jeshi la Polisi na kutokusikia kuhusiana na Vikosi vya SMZ kuzungumzia katika Mkutano huo.
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Dimani Unguja Mhe Dk Mwinyihaji Makame akiuliza swali kuhusiana na Mgombea wa Urais kufanya mikutano yake kwa sehemu mbalimbali za kampeni zake vipi kuhusiana na wanachama kufuatilia mikutano hiyo ikiwa yeye ni kiongozi wa kitaifa. 
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Chumbuni Unguja Mhe Mashavu Juma Ali Kwa , ameuliza kuhusiana na kampeni za nyumba kwa nyumba vipi hizi zinaashiria rushwa kwa wagombea.
Mgombea wa Chama cha NRA Mhe Salum Sultani Saleh Jimbo la Kiembesamaki ameuliza kuhusiana na utoaji wa viwanja wakati wa mikutano ya kampeni ni nani muhusika na suala hilo la viwanja hutokea mitafaruki katika baadhi ya viwanja wakati wa kampeni.
Mgombea Uwakilishi kupitia CCM Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said, akiuliza swali kuhusiana na baadhi ya Vyama vya siasa hufanya mikutano yake ya kampeni katika maeneo ya viwanja vidogo katika maeneo ya makaazi ya watu na kutoa maneo ya kashfa zidi ya mgombea 
Mgombea Uwakilishi Jimbo la Makunduchi CCM Mhe Haroun Ali Suleiman akiuliza swali kuhusiana na utamaduni wa baadhi ya Wananchi hufanya michezo mbalimbali na kutowa zawadi kwa timu shiriki vipi swali hili liko katika rushwa. 
CHANZO: ZANZINEWS

No comments: