ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 19, 2015

MSIBA ATHENS, UGIRIKI

Familia ya Marehemu George na Mama Rhoda Malongo wa Upanga, Dar es Salam wanasikitika kutangaza kifo cha binti yao mpendwa Esther Glory Malongo kilichotokea ghafla baada ya kuugua kwa muda mfupi tarehe 16/09/2015 Athens, Ugiriki.(1 Timothy 4:7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeiilinda.)

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa na watanzania waishio Athens, Ugiriki siku ya jumanne tarehe 22 September 2015 na kusafirishwa kwenda Dar es Salaam Alhamisi, tarehe 24 Septermber 2015.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 26 September 2015, Dar es Salaam Tanzania.
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inaendelea kufanyika Athens, Ugiriki. Msaada wa hali na mali unahitajika kwa ndugu, jamaa na marafiki ili kuweza kufanikisha kuulaza mwili wa kipenzi chetu Esther.

Kwa yeyote aliyeguswa unaweza kutoa mchango wako kupitia Western Union, Athens Greece kwa Ms Edna Neilly Malongo.
Kwa mawasiliano zaidi:-
Edna Malongo +30694 922 8337 au +255 784 600 577(WhatsApp only)
Tunatanguliza shukrani nyingi za dhati kwa upendo na ushirikiano wenu, Mungu awabariki sana na akanyanyue watu wa kuwasaidia wakati mkihitaji msaada.

No comments: