ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 14, 2015

Mtuhumiwa wa ugaidi ajaribu kujiua kwa kujirusha ghorofani



Kamishna wa polisi Kanda Maalum wa Dar es Salaam, Suleiman Kova

Mtu anayedaiwa kuwa mratibu wa matukio ya ugaidi, uporaji wa silaha na mauaji katika vituo vya

Dar es Salaam. Mtu anayedaiwa kuwa mratibu wa matukio ya ugaidi, uporaji wa silaha na mauaji katika vituo vya polisi , Ally Ulature (60) amejeruhiwa baada ya kujirusha katika ghorofa kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni azimio la kujiua au kutoroka.

Akizungumza leo, Kamishna wa polisi Kanda Maalum wa Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema Ulature ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mnandimkongo, wilayani Mkuranga alikamatwa mwezi huu baada ya msako mkali wa polisi.

Kamanda Kova amesema Ulature amejirusha kutoka ghorofa ya tatu katika jengo la makao makuu ya polisi alipokuwa akihojiwa na maofisa upelelezi.

“Amejirusha kutoka ghorofa ya tatu hadi chini baada ya kuaga kuwa anakwenda msalani, tunadhani lengo la mtuhumiwa lilikuwa kujiua au kutoroka lakini yote hayo hayakufanikiwa badala yake amejeruhiwa,” amesema kova

Amesema mtuhumiwa huyo amepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

Kova amesema mtuhumiwa huyo ndiye aliyekuwa `mchoraji’ wa matukio ya uvamizi katika vituo vya polisi vya Ikwiriri, Kimanzichana na Stakishari ambako alisababisha mauaji na uporaji wa silaha.

Amesema alikamatwa katika kijiji cha Mamdimkongo ambako alikuwa akiishi kwa kujifichaficha. Kamanda Kova amewashukuru wananchi kwa ushirikiano na kutaka waendelee ili kukomesha matukio ya uhalifu kanda ya Dar es Salaam.
:Source:Mwananchi

No comments: