ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 10, 2015

NAWASHANGAA MAWAZIRI WAKUU WENZANGU WALIOSTAAFU,WAKIDAI CCM MIAKA 50 HAKUNA KILICHOFANYA-JAJI WARIOBA

 Waziri Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Butiama ambapo aliwaeleza Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MARA

WAZIRI Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ameibuka katika kampeni za mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli na kusema kuwa anashangazwa na hatua ya mawaziri wakuu wenzake kuhama CCM na kudai hakuna kilichofanyika katika miaka 54 ya Uhuru.

Pamoja na hali hiyo amesema anajua wazi huenda hata wanachokifanya hawajui wajibu wao walipokuwa katika madaraka hayo kama washauri wakuu wa rais.alisema  sasa umefika wakati wa watu wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa katika kampeni zao wajitafakari zaidi.

"Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu kama dira halafu unasema CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote walimfuata wanapita kwenye misingi yake," alisema Jaji Warioba
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Bunda leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
 Dkt akionesha fimbo hiyo aliyokabidhiwa na Chief wa Wazanaki,Japhet Wanzagi
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge kulia ni Nimrod Mkono kutoka jimbo la Butiama Vijijini na  Profesa Sospeter Muhongo ambaye anatoka jimbo la Musoma vijijini.

 Mamia ya Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira,shoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba,kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini Nyamuswa jioni ya leo.
 Wananchi wa Nyamuswa wakimsikiliza Dkt Magufuli.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Ndugu Sospeter Muhongo,kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira wakati wa mapokezi mkoani Mara,pichani kati ni Mtoto wa Baba wa Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki,Mh Makongoro Nyerere
  Umati wa wakazi wa Butiama wakimsikiliza Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Sehemu ya Wananchi wa Butiama wakishangilia jambo

7 comments:

Anonymous said...

Huna mana wala hujui mana
Mtu mzima ovyo

Anonymous said...

Mh. Warioba kazi yako ni nzuri daima ila tu unasahau kuwa waTanzania wanahitaji mfumo mbadala na wewe ndiye ulikuwa kiongozi wa kukusanya maoni ya katiba. Hakuna kilichoonekana sana sana ni kuingiza yao wanayoitaka kulinda maslahi yao binafsi kama vile kuteua wagombea kulivyofanyika! Kikubwa hapa unatarajia ninintofauti atakachokitenda mtarajiwa hapo pembeni yako kwa kuilinda ilani ya kulindana. Nadhani ingelikuwa jambo la busara ahadi za neema zikaachwa kwani kama ni neema ilitakiwa kuwepo tangu ukiwa waziri mkuu wewe hapo! Leo hii shillingi inadidimia kwa kasi huku tukiahidiwa neema! Ipi hiyo!? Tuna shida kila kona bado zilizoliwa haziwahusu wananchi. Bado wataendelea kubeba kwa viroba. Aliyetoa na aliyepokea wotw wameendelea kuneemka waache kurudia. Hiyo ndoto. Kuna matajiri lukuki mjini na wasioweza kulinganishwa na hao mnaowaona matajiri mbona hawazungumziwi. TATIZO KUBWA CHAMA KIMEKUWA CHA DILI TUPU. DILI DILI TUUH!!!!!.

Anonymous said...

Sababu kubwa inayosababisha CCM ishindwe ku deliver ni unafiki wa viongozi wake. Mzee wangu tall rasimu ya katiba ilipokuwa inajadiliwa na yeye akiwa mtaani anaganga njaa alianza harakati thabiti za kuisimamia rasimu ya katiba waloipeleka bungeni ipite. Walohodhi CCM wakambughudhi na kumuita kila majina, mbaya zaidi wakamtuma Makonda na wenzie wakamchapa vibao kwenye kongamano pale Ubungo hotelini, makonda hakuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria na muda mfupi walomtuma wakamzawadia cheo cha DC.
Kiongozi wa nchi akaendeleza kejeli na hata kwenye hotuba moja akasema kuwa hatapenda yamkute kama yalokukuta wewe, bila hata ya ku laani kitendo cha wewe kula kichapo. Leo wenzio wanaojitambua wanachukua hatua sahihi unawashangaa. Nadhani ni Aibu kwako mzee. Na nini hasa wamekwambia watakupa?
Maintain your self esteem mzee, dont lower yourself.
You are standing in a wrongful side. Hawapo na wewe hao, wanakutumia kuonyesha kuwa kuna umoja.
But all of you mtaanguka vibaya mwaka huu.
Pole sana mzee.

Anonymous said...

Uncultured SOB!

Anonymous said...

Hujitambui! Lowasa na wapiga dili wenzake ndio unategemea wakuletee mfumo mbadala? Labda upigaji dili wa kisasa zaidi, ambao utaliweka taifa zima rehani!

Anonymous said...

Mheshimiwa Warioba ana amini kabisa msemo wa Waswahili kuwa, "Zimwi likujualo halikuli likakumaliza" ndiyo maana hataki kuwaunga mkono hao viongozi wenu laghai na ambao ni chui waliovaa ngozi za kondoo.

Anonymous said...

Warioba ni mtu wa mabadiliko kweli na haifai kumbeza isipokuwa ameona mabadiliko atakayoleta magufuli ni ya kweli kabisa na yanawezekana kuliko lowasa. Mabadiliko ya lowasa ni ya kukimbilia ikulu na papara za wapinzani kushika dola basi hawana sera ya aina yeyote ya mabadiliko zaidi ya kelele .