HOJA ya UKAWA: ELIMU Bure mpaka chuo kikuu! Tanzania ina Vyuo vikuu 54. Tusidanganyike kama Watoto wadogo haiwezekani hata kidogo!!
TAFAKARI: tutathmini tu watu wa Shahada ya kwanza! Mwaka 2014/2015 TCU inatarajia kudahili wanafunzi 48, 000.
Kwa mwanafunzi mmoja chuo kikuu fani ya Sayansi ya asili (Natural Science) kwa mwaka mmoja anahitaji kiasi kisichopungua Tshs 5,500, 000 (tuition fees, stationary, meal and accommodation, field, Equipments n. k).
Kwa mwaka huu 2014/2015 TCU kwa sayansi asili inatazamia kudahili wanafunzi 15000. Kwa maana hiyo
itahitaji Tshs Billion 82,500,000,000/=
Upande wa pili ni Sayansi ya Jamii ambapo inakadiriwa wanafunzi 33000 watadahiliwa katika vyuo vikuu mbalimbali. Wastani wa mwanafunzi mmoja ni Tshs 3,500,000/=. Hivyo itahitajika jumla ya Tshs 115,500, 000, 000/=.
Hivyo basi kwa mwaka wa kwanza tu Wizara ya Elimu itahitaji Billion 198, 000, 000, 000/=. Hapo sijagusa mwaka wa pili, tatu, Nne na tano.
Pia sijagusa wanafunzi wa Shahada ya uzamili (Masters degree) na Uzamivu (PHD) maana pia ni sehemu ya chuo kikuu. MA mwanafunzi mmoja mpka kumaliza anahitaji wastani wa Tshs 15,000,000/= kwa upande wa PHD wastani wa million 50.
Upande mwingine sijagusa Wanafunzi wa certificate, diploma, Elimu ya sekondari, mishahara ya walimu, Nyumba za walimu, Mafunzo kwa walimu, Vifaa mashuleni na vyuoni, Likizo za walimu, Madaraja ya walimu.
Bajeti hata haifikiriki, katika ulimwengu huu wa utandawazi hakuna nchi duniani inayosomesha wanafunzi chuo kikuu Bure Badala yake hua kuna unafuu wa ada na michango!!
Ni ukweli usiopingika kwamba, kwa uwezo wa serikali, Elimu Bure inaweza kutolewa mwisho kidato cha Nne au Sita.
Tuwe macho na hawa watu!!
Twende na MAGUFULI,
Umoja ni USHINDI!

15 comments:
What a simple mind! Huna hoja zaidi ya ushabiki!
Ndugu mwandishi elimu bure inawezekana kabisa gari aina ya vx inagharimu dollar 150000 kwa gari moja ambazo ni sawasawa na shilingi 315,000,000 kwa gari moja mawaziri, wakuu wa mikoa, wabunge, wakuu wa wilaya, makamanda wa jeshi, Polisi, na taasisi mbalimbali za serikali wanatumia haya magari kama nchi inauwezo wa kuwapatia hawa magari haya huwezi kuniambia haina uwezo wa kutoa elimu bure. Kuna magari zaidi ya 7000 ya aina hii bado hatujaangalia sehemu nyingine ambayo serikali inafuja hela za Watanzania kama safari za watumishi wa serikali zisizo na kichwa wala miguu, madini, mbuga za wanyama, bandari, mlima, na kodi kwa hivyo inawezekana kabisa acha mawazo ya kizamani
Nchi nyingi duniani zinatoa elimu bure kwa raia wake. Lakini kama sio raia lazima ulipie gharama za elimu hasa elimu ya juu. Najua nchi kama Norway, Denmark, Sweden, Germany n.k. Elimu ni bure kwa ngazi zote. Kitu muhimu ni vipi unapanga vipaumbele vyako. Je kipaumbele chako wabunge wapewe marupurupu makubwa na mishahara minono au wananchi ambao babu zao na wazazi wao wanaolipa kodi na madeni ya nchi watoto wao wapate elimu ya bure?
Nape, hii sio Tanzania aliyoiacha baba yako. Fungua macho!
Endelea kutetea wezi wako kwa kusema haiwezekani mbele ya Lowassa hakuna kitakachoshindikana. Hata kama haitawezekana hamna mtu atakayebadilishwa na maneno ya kipumbavu.
Ama kweli mwandishi in CCM
Ila inawezekana kuiba mabilion ya fedha na watoto wa vigogo wa CCM kusoma nje
Na kupata Kazi zote zenye masilahi manono inchini
Tumechoka tunamtaka huyu huyu tutajuwa moja
Miaka 50 it's enough
Bye bye CCM 25 October
Pamoja na "hesabu uchwara" ya hapo juu, bado namba ulizoweka hazifikii pesa ya ku-John walking.... Pole January
Elimu bure hadi kidato cha sita inawezekana tusidanganyane. Frdha zipo zinaingizwa mikononi mwa wajanjanna waloo na nafasi tu. Kwani mbunge analipwa kiasi gani kwa sasa hivi! Vikao wanavyokaa havina hata mwelekeo ni malumbano tu. Huu sio wakati wake.
SAWA SAWA MTOA HOJA,WEWE AU NYINYI MNASEMA ELIMU BURE NI NDOTO,NADHANI HII INATOKANA NA NDOTO ZENU POTOFU KABISA KUWA CCM ITARUDI TENA MADARAKANI BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA HUU 2015.NASEMA NI NDOTO KWA SABABU KIILA AINA YA TAFITI HURU,UHALISIA WA MWENENDO WA KAMPENI,UAMUZI WA WATANZANIA WALIO WENGI,UNAMPA MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA USHINDI WA WAZI,TENA WAZI KABISA WA KITI CHA URAIS TENA KWA ASALIMIA NYINGI 82 KWA 15 ZA MAGUFULI.TATIZO LA UONGOZI WA TANZANIA YETU NI MATUMIZI MABAYA TENA YA KUFURU YALIYOMO NDANI YA BAJETI YETU.JEE MMEIONA RIPOTI YA MHE.MBATIA KWAMBA SAFARI ZA NJE ZA MHESHIMIWA RAIS KIKWETE KWA MIAKA YAKE 10 YA UTAWALA[2005-2015]AMETUMIA TRILLION NNE[4]PESA AMBAYO INGEWEZA KUTOA ELIMU BURE KWA MIAKA 20,KUJENGA VYUO VIKUU VIPYA VYA SERIKALI 82.WANANCHI TUNA HASIRA KUBWA MNO NA GHARIKA HILO LA UFUJAJI NA NDIYO MAANA TUMEAMUA KUMPA KURA ZETU ZA VEMA TELE TELE MHESHIMIWA LOWASSA.CCM KIFO CHENU CHA MENDE KIMEWADIA.
Kama unataka kuona mabadiliko basi soma maoni yote hapo juu. Inaonesha ni jinsi gani Watanzania wanaotaka mabadiliko wanavyoona na kutambua tactics au mbinu mbovu za ccm. Nawapa heko wote mliotoa hayo maoni mazuri hapo juu. Mambo ya danganya toto ya ccm tusitishiwe nayo. Tuzidi kuyapiga chini kila mbinu wanayokuja nayo. ccm mwaka huu hamtatuweza. Kwa kifupi, ELIMU YA BURE, HUDUMA YA MATIBABU YA BURE TANZANIA INAWEZEKANA SINCE 1961. ccm wasitutishe kuwa haiwezekani. Kwao haiwezekani kwa sababu watakosa ULAJI. Asilimia 99.99% ccm wanatoa uongo mtupu.
Kama unataka kuona mabadiliko basi soma maoni yote hapo juu. Inaonesha ni jinsi gani Watanzania wanaotaka mabadiliko wanavyoona na kutambua tactics au mbinu mbovu za ccm. Nawapa heko wote mliotoa hayo maoni mazuri hapo juu. Mambo ya danganya toto ya ccm tusitishiwe nayo. Tuzidi kuyapiga chini kila mbinu wanayokuja nayo. ccm mwaka huu hamtatuweza. Kwa kifupi, ELIMU YA BURE, HUDUMA YA MATIBABU YA BURE TANZANIA INAWEZEKANA SINCE 1961. ccm wasitutishe kuwa haiwezekani. Kwao haiwezekani kwa sababu watakosa ULAJI. Asilimia 99.99% ccm wanatoa uongo mtupu.
Endelea kudanganyana.
Muendelee kudanganya umma. Ukweli ni kuwa haiwezekani elimu kutolewa bure kwa shule zote hadi vyuo vikuu. Mpeni kura huyo Lowassa wenu tuone kama hizo hela za serikali pamoja na za ufisadi zitatosha kulipia gharama hizo. Acheni ushabiki. Kuna mambo ya kukubali na kuna mambo mengine yasiyo wezekana na ni lazima tukubali. Hivi hizi nchi zenye pesa na zinaitwa zimeendelea na ambazo kuna wananchi wake kibao hawajasoma mpaka vyuo vikuu shauri ya kukosa ada na zenyewe zinahitaji mabadiliko kama haya mnayosema ili serikali zake ziweze kutoa elimu bure?
TUNAJARIBU KUANGALIA UNACHOPINGANA NACHO KUHUSU SERIKALI YA UKAWA KUTOA ELIMU BURE [YOUR TANGIABLE ARGUMENTS] HATUKIONI,HUELEWI,HUELEWEKI.TUKUTANE TAREHE 26 OCTOBA 2015 JIONI TUKITEGEMEA POLL RETURNS ZA VITUO VYOTE TANZANIA VITAKUA VIMESHAFANYA SUBMISSIONS ZAO NA MHESHIMIWA LOWASSA ATAKUA ANAANDAA HOTUBA YAKE YA KWANZA YA KIUTAWALA BAADA YA KUAPISHWA KUWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.HAPO NDIPO MACHO NA MASIKIO YAKO YATAFUNGUKA UPYA SASA,KATIKA ,TANZANIA MPYA BILA UTAWALA WA CCM,TANZANIA YA MAENDELEO BILA ULAGHAI NA LONGOLONGO.
Post a Comment