ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 25, 2015

TASWIRA,CCM YARUSHA JESHI LA ANGA,MWIGULU AONGOZA KIKOSI...WAIMARISHA USHINDI WA KISHINDO MAJIMBO YA NZEGA HII LEO

Chama Cha Mapinduzi hii leo kimerusha Helcopta yake ya kwanza kwenye kila pembe ya Nchi kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu kwenye nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais.Kazi ya kupasua anga hilo linaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Ndg.Mwigulu Nchemba ambaye katika Jimbo lake la Iramba kwa asilimia 98 amejihakikishia Ushindi wa kishindo hapo Tar.25.10.2015
Vijana Imara wa Chama cha Mapinduzi Fieldmarshall Mwigulu Nchemba na Hamis Kigwangalla wakipiga Push-Up kuonesha sapoti kwa Mgombea wao J.Pombe Magufuli aliyefanya tukio hilo siku si nyingi kwenye Jukwaa la Kampeni.
Picha na Sanga Festo Jr.

Mwigulu Nchemba ambaye ni Mjumbe wa kamati ya CCM ya Ushindi na Mgombea Ubunge Jimbo la Nzega Vijijini Ndg.Kigwangalla akiwasili kwenye Ufunguzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Nzega Mjini hii leo.Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi Comrade Mwigulu NChemba ambaye hii leo ameanza safari za Anga kwa Anga kusaka kura Nchi nzima,Hapa akizungumza na Wananchi wa Nzega namna CCM ilivyosimamisha Mgombea Bora wa Urais ambaye sifa yake kuwa ni KAZI na rafiki yake Mkubwa ni TANZNAIA.Mwigulu amesema,Uchaguzi wa mwaka 2015 ni mwepesi sana kwa chama cha Mapinduzi kwakuwa wagombea wote ni zao la CCM na wanawajua vizuri.Pia wagombea wengine wa vyama vya Upinzani wanazungukwa na makundi ya Ubadhilifu wa mali za Umma wakati Magufuli yeye anazungukwa na Watu wa kazi.
Hivyo Uchaguzi huu ni DILI vs KAZI,Hivyo kazi mbayo ni J.Pombe Magufuli itashinda kwa kishindo.
 Mbunge Mtarajiwa wa Nzega Mjini Mh.Bashe akizungumza na Wananchi wake wakati wa Ufunguzi wa kampeni kwa Jimbo la Nzega Mjini hii leo.Bashe amewaomba Wananzega kumpatia Ridhaa ya kuwambunge wa Jimbo hilo ili aweze kusimamia vyema shughuli za Maendeleo kama Uimarishaji wa Huduma za Afya kwa Hospitali ya Nzega,Kusimamia haki za Bodaboda na Mamantilie wa Nzega,Kusimamia shughuli za Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa Ufanisi.Pia amesisitiza yeye ni TEAM MAGUFULI na anaamini Maendeleo ya kweli na ya kasi yataletwa na Magufuli kwa awamu hii ya tano ya Uongozi wa Taifa letu.Wananchi wakifurahia jambo kutoka kwa Mbunge wao mtarajiwa Mh.Hussein Bashe.Mbunge Mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Jimbo jipya la Nzega Vijijini Mh.Hamis Kigwangala akisalimiana na Wananchi wa Nzega mjini alipokwenda kusapoti Ufunguzi wa kampeni za Mgombea Jirani Ndg.Hussein Bashe."Ndani ya CCM ni Raha na
Furaha"Kigwangalla na Bashe wakiwasalimia Wananchi wa Nzega Mjini ikiwa ni ishara ya Wazi kuwa CCM ni Moja na Wamejipanga kwa Ushindi.Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taiga Ndg.Mwigulu Nchemba na Comrade Emmanuel Nchimbi wakiteta jambo wakati wa Ufunguzi wa kampeni Jimbo la Nzega Mjini hii leo;.Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg.Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Nzega Mjini wakat wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge kwa jimbo hilo,Nchimbi amewasisitiza wananchi wa Nzega kuendelea kuwa na Imani na Chama cha Mapinduzi kwakua ndio chama pekee chenye Mgombea anayeweza kupambana na kasi ya maendeleo tunayoyahitaji.Pia amesisitiza kuwa CCM haijafanya kosa kumsimamisha Mh.J.Pombe Magufuli kwenye nafasi ya Urais,Chama kilizingatia Ubora wa wagombea na hatimaye Magufuli alikuwa Bora kupeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi mkuu ngazi ya Urais.
Mbali na hilo Nchimbi amewaomba Wananchi kufanya siasa za kistaarabu na kujitokeza kwa wingi siku ya Tar.25.10.2015 kwenye vituo vya kupiga kura wakiwa na vitambulisho vyao.Wananchi wakifuatilia MkutanoMwigulu,Nchimbi na Bashe wakisuka Mkakati wa kuhamasisha Wananchi kujitokeza kuipigia Kura CCM siku ya Uchaguzi.Comrade Emmanuel Nchimbi na Mwigulu Nchemba wakimnadi Mbunge mtarajiwa wa Nzega ndg Bashe kwa Wananzega.Wananchi wa Kata ya Ndala Jimbo la Nzega Vijijini wakiwa wamembeba Mbunge wao mtarajiwa Ndg.Hamis Kigwangala hii leo mara baada ya Mkutano wa kuomba kura kwa wananchi ili aweze kushinda nafasi ya Ubunge kwenye Uchaguzi mkuu wa tar 25/10/2015.KIgwangala akiomba Kura kwa Wananchi wa kata ya Ndala.Mwigulu Nchemba na Hamis Kigwangalla wakiagana na Wananchi wa kata ya ndala mara baada ya Mkutano wa kampeni wa chama cha Mapinduzi jimbo la Nzega Vijijini.Wananchi wa kata ya shimbo wakifuatilia Mkutano wa Chama cha Mapinduzi wa kampeni za Ubunge wa Mh.Kigwangalla hii leo kwenye Kata ya Shimbo.Wananchi wa kata ya Shimbo wakionesha Ishara ya kuwa KURA zao zote ni kwa J.Pombe Magufuli,Ubunge kwa Kigwangalla na Madiwani wa CCM kwa jimbo la Nzega Vijijini.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kata ya shimbo juu ya Umuhimu wa Kuichagua CCM kwa maendeleo ya Nzega na Jimbo jirani jipya la Igunga Kusini.Mwigulu,KIgwangalla,Gulamali na Diwani wa kata ya Shimbo wakionesha Uimara wao wa kiafya  "Wanamuunga MKono Magufuli kwa Push Up"Sehemu ya Maelfu ya Wananchi waliofika kwenye mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge jimbo la Nzega Mjini hii leo.

6 comments:

Anonymous said...

Kazi mtaiweza ya kumlinda rais wetu Lowassa
Ajira mnayo vijana

Anonymous said...


Mambo yakiwa magumu unahitajika kuwa mbunifu. na nilazima uende kwa mganga akupe masharti na ubunifu wa kufanya viroja ukawa kituko mbele ya mkeo na wanao na kadamnasi ya wadanganyika. Zifuatazo ni staili tofauti zinazotumika na wanaCCM kuomba kura tena kwa wananchi. Wanatia huruma sana. Staili hizi za push up huwezi kuzikuta Ukawa.


masharti ya mganga sometimes yanakuwa noma sana;watu wana pigishwa push up kama mazezeta.mganga oyeeeeeee. je kama mkiwaa na mkono wa suweta itakuwaje mbele ya hadhara yote hii.

kweli maccm weupe kichwani.

kwani uraisi umesikia ni ubondia au uwana riadha mtu lazima uwe unapiga push up.

mwaka huu tutaona mengi na kuyasoma mengi na watatulia tu. na kuisoma number mziki wa mr white hair si wa kitoto wanaweweseka na kupiga mapushap kama waa masumbwi.

mr white hair hebu waone huruma wenzako kwi kwi kwi kwi. nasikia wana lala na viatu kwa mziki wako mr white hair.kwi kwi kwi.

masharti ya mganga yana waadhiri kwi kwi kwi.

Anonymous said...

BADO SIKU ISHIRINI NA NANE,NAANDIKA HIVVYO LEO JUMAMOSI TAREHE 26 SEPTEMBA 2015 KUIFIKIA SIKU YA SIKU YAANI SIKU YA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA MNAMO TAREHE 25 OCTOBA 2015 NILIPOYASOMA MAANDISHI HAYA NA KUWASHUHUDIA HAWA MACHIZI WAWILI WA CCM WAKIPUSH ARDHI HUKU WANAJAMBA KWA NGUVU,MARA NIKAREJEA USEMI KWAMBA MTOTO WA LAANA NI LAANA,NIMEKAGUA UPYA KADI YANGU YA KUPIGA KURA AL-MAARUF KICHINJIO-KINAWEKWA MBAALI SANDUKUNI.TENA HUMO KWENYE BAHASHA NDOGO,KWENYE MFUKO,KWENYE POCHI.MTU WANGU,MTU WETU N YULE YULE CHAGUO LA WATANZANIA WALIO WENGI JABALI LA SIASA KIBOKO WA KIKWETE,MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA.NI YEYE LOWASSA PEKEE,NI YEYE LOWASSA RAIS;NCHEMBA ANAJUA,BABA YAKE ANAJUA,KIGWANGALA ANAJUA MAGUFULI ANAJUA.UKOMBOZI WA WATANZANIA UPO OCTOBA 25,2015.KISHA CCM,MTAKAA MKAO WA KULIWA-MLIWE.

Anonymous said...

Mbona mmeshaanza kutishia kujitoa kwenye uchaguzi kama kweli mna uhakika wa kushinda. Mmeona mambo ni magumu ndiyo maana mmebaki mnatapatapa ovyo. Tunangojea hiyo tarehe 10/25 kipenga cha mwisho kitakapo pulizwa tuone nani ana pumzi zaidi.

Anonymous said...

Unless we ni mpenzi wa ccm but this is idiotic.

Anonymous said...

Anonymous of September 26, 2015 at 6:53 PM

You can suggest anything and whether you like it or not the whistle on October 25 will signal the "grand finale" and there is nothing idiotic about it.