Haya ndiyo Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu (Ajenda 2030) ambayo leo Ijumaa Wakuu wa Nchi na Serikali wanayapitisha katika Mkutano wao wa Kihistoria Unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani. Anjenda 2030 ambayo utekelezaji wake unaaza mwakani inachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Millenia( MDGs) ambayo yamefikia ukiongoni mwaka huu. Upitishaji wa Ajenda 2030 utatanguliwa na hotuba ya Baba Mtakatifu Francis
.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza wakati wa mkutano ulioandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani na Mashirika ya Kimataifa kama vile Mpango wa Chakula Duniani, Mkutano uliokuwa ukijadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na uhusiano wake na usalama wa chakula, lishe na afya. Mkutano huu ulifanyika siku ya alhamis katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ujeruman katika Umoja wa Mataifa
Na Mwadishi Maalum, New York
Leo Ijumaa, Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali zaidi ya 150 kutoka mataifa mbalimbali duniani, watapisha ajenda na malengo mapya ya maendeleo endelevu ( Ajenda 2030) kuchukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Millenia yanayomaliza muda wake mwishoni mwa mwaka huu.
Katika mkutano huu wa kihistoria unaofanyika miaka kumi na tano tangu MDGs zilizopitishwa, utatanguliwa na hotuba ya Baba Mtakatifu Francis.
Baada ya kupitisha ajenda 2030 na ambayo imejikita zaidi katika kuutokomeza umaskini na ulinzi wa mazingira pasipo kumwacha yeyote nyuma,Viongozi hao Wakuu wa Nchi na Serikali kila mmoja wao atapata fursa ya kuelezea matarajio ya serikali yake katika utekelezaji wa ajenda hiyo yenye malengo 17.
Tayari Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wamekwisha kuwasili Jijini New York , yaliko Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaongozwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Siku moja kabla ya kupitishwa kwa ajenda 2030, baadhi ya viongozi ambao wameambatana na Mhe. Rais wameshiriki katika mijadala mbalimbali na ambayo maudhui yake yanashabihiana na ajenda nzima ya Maendeleo Endelevu.
Akiwakilisha ujumbe wa Tanzania katika mikutano hiyo ya pembezoni, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, alishiriki katika majadiliano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na uendelevu wa usalama wa chakula, lishe na Afya
Balozi Mulamula alikuwa kati ya wanajopo watano katika majadiliano hayo ambayo yaliandaliwa na Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani na Mashirika ya Kimataifa .
Katika majadiliano hayo ambayo yalijikita katika kuangalia ni namna gani utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu unavyoweza kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na hususani katika maeneo yanayomgusa mwananchi wa kawaida kama vile usalama wa chakula, lishe na afya.
Aidha wanajopo hao walitakiwa kujibu hoja mbalimbali zikiwamo ni kwa namna gani kwa mfano Tanzania imejiandaa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na ambayo kwayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuleta au yanasababisha matatizo katika eneo kama kilimo na lishe.
Akijibu hoja hiyo pamoja na nyingine, Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula aliwaeleza washiriki wa majadiliano hayo kwamba kwa nchi kama Tanzania mabadiliko ya tabia nchi ni jambo lililo dhahiri na si nadharia.
Akatoa mfano kwa kusema kwamba, kuna baadhi ya maeneo ya nchi, ambapo wakulima wanashindwa kutambua msimu halisi wa kuanza kulima na kupanda tofauti na miaka ya nyuma.
Aidha akasema, maeneo mengine mvua zinanyesha kupita kiasi na wakati maeneo mengine yana kumbwa na ukame wa kupindukia na hivyo kuathiri shughuli za kilimo na hatimaye ukosefu wa chakula na chakula chenye viini lishe ambavo ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo hususahi ya watoto chini ya miaka mitano.
Mfano mwingine ambao anasema ni wazi umechangia kwa namna moja ama nyingine katika ubaribufu wa mazingira ni pamoja na matumzi yasiyo endelevu ya ardhi, ukataji wa holela wa miti na ile hali ya mito mikubwa kupingukiwa maji na hivyo kufanya mabwana makubwa yanatuyotumika kuzalisha umeme kukosa maji ya kutosha.
“Nilipokuwa mdogo tulikuwa tunakatazwa sana na wazazi wetu kung’oa miti michanga, na wakati huo hatukuelewa kwamba wazee wetu walikuwa wanatufundisha utunzaji wa miti” akasema Balozi
Akielezea ni mikakati gani ambayo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inachuka katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na hiyo kuwa na uhakika wa usalama wa chakula, na upatikanaji wa lishe bora.
Katibu Mkuu, ameeleza kwamba serikali imejiwekea mipango madhubuti ikiwamo ya uhamasishaji wa wananchi kuwa na matumizi bora na endelevu ya ardhi, misitu, kilimo cha umwagiliaji pasi kutumia maji mengi na uhifadhi wa misitu.
Akasisitiza kwamba mipango yote iwe ile inayoandaliwa na Umoja wa Mataifa Mashirika ya Kimataifa n ahata Serikali ili tekelezeka na kuwa endelevu inapashwa kumilikiwa na wananchi ambao hasa ndio waathirika wakubwa lakini pia wanamchango mkubwa wa kuleta mabadiliko ili mradi wawezeshwe.
Akatahadharisha kwa kusema kama wananchi hawatahusishwa kwa namna moja ama nyingine basi utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu unaweza kuishia kwenye makabrasha.
Wanajopo wengine wakichangia katika majadiliano hayo akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa Mapango wa Chakula Duniani, walieleza kwamba suala na usalama wa chakula na lishe linapashwa kupewa mkazo wa kipekee kwa kile walichosema, takwimu zinaonyea kwamba idadi kubwa na watu duniani wanathirika kwa ukosefu wa chakula lakini kubwa Zaidi vyakula vyenye virutubisho na viini lishe.
Wakatoa mfano kwa kusema kuwa wakati bei ya vyakula aina ya nafaka ikushuka, bei ya matunda na mboga mboga, vyakula vitokanavyo na wanyama na ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa watoto chini ya miaka mitano vinazidi kupanda bei maradufu na wanaoathirika ni watu maskini.
Na kwa sababu hiyo wakasisitiza kwamba kuna uwiano mkubwa kati ya mabadiliko ya tabia nchi, tatizo la usalama wa chakula na lishe duni mambo ambayo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zinatakiwa kushirikiana na kuikabili changamoto hii ambayo athari zake ni kubwa.
.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza wakati wa mkutano ulioandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani na Mashirika ya Kimataifa kama vile Mpango wa Chakula Duniani, Mkutano uliokuwa ukijadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na uhusiano wake na usalama wa chakula, lishe na afya. Mkutano huu ulifanyika siku ya alhamis katika Uwakilishi wa Kudumu wa Ujeruman katika Umoja wa Mataifa
Sehemu ya washiri wa mkutano kuhusu uhusiano wa mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa usalama wa chakula, lishe na afya wakimsikiliza Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula ambaye alikuwa kati ya wanajopo watano waliozugumza katika mkutano huo
Sehemu ya washiri wa mkutano kuhusu uhusiano wa mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa usalama wa chakula, lishe na afya wakimsikiliza Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula ambaye alikuwa kati ya wanajopo watano waliozugumza katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment