Wednesday, September 9, 2015

USHIRIKI WA LOWASSA VITANI WAIBUA GUMZO


Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania, Mwl. J.K Nyerere na makamanda wa Jeshi.
Katika mkutano wa kumnadi mgombea wa chama chake, Makamba alidai kuwa anashangazwa na madai ya Lowassa kuwa alikwenda vitani, wakati aliyeandikisha majina ya askari waliokwenda huko wakati huo alikuwa ni Rais Jakaya Kikwete ambaye hakuwahi kuorodhesha jina hilo.
Wakizungumzia suala hilo, watu mbalimbali waliopiga simu chumba chetu cha habari, walisema ni vyema kama Lowassa angejitokeza na kuthibitisha madai hayo, kwani akikaa kimya, ataonekana ni mwongo, kitu ambacho ni kibaya kwa kiongozi anayeomba kuwa rais wa nchi. 

“Maneno kama haya niliwahi kumsikia akiyasema Makongoro, kwamba hakuwahi kumuona Lowassa mstari wa mbele, leo Makamba anasema jina lake halikuandikwa na Kikwete, ni vizuri akajitokeza ili athibitishe kama kweli alienda au la!” alisema Shauri Shamim, aliyedai kupiga simu akitokea Tanga. 

“Hili ni jambo kubwa, siyo dogo kama inavyoweza kudhaniwa, tunajua kuwa Lowassa aliwahi kuwa askari, ajitokeze na kuzijibu tuhuma hizi za wanajeshi wenzake ili tujue kama ni propaganda za kisiasa au la!” alisema Jane Jarome wa Masasi. 

Mei mwaka huu, wakati wa mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine, Lowassa alisema alikuwa miongoni mwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki vita vya kumng’oa madarakani kiongozi huyo wa Uganda aliyeivamia Tanzania.

8 comments:

  1. Jamani hebu tujadili issues za msingi kwani kuhusu vita ni nchi yote ilikuwa vitani na siyo waliokuwa mstari wa mbele tu. Hata sisi tulipigana kivyetu kwa kuunga mkono kwa hali na mali, na mwisho wa vita ni Watanzania wote walioathirika. Let's put aside mediocrity and grow up as season politicians.

    ...kazi kweli kweli hapa...

    ReplyDelete
  2. Alikuwa hakuwa tunachojua ni kuing'oa ccm ilioshindwa kuleta maendeleo kwa zaidi ya miaka 30 bali kuongeza umaskini na manyanyaso kwa raia wa Tanzania

    ReplyDelete
    Replies
    1. Can you pause and use your brain for a second? Where did UKAWA flagbearers come from? Their failed leadership within CCM is what locked the country in the current state of poverty. If they had an extremely poor performance under CCM, there's no reason to believe that they'll have a stellar performance under UKAWA. ....Are you seriously counting on the most corrupt elements (Lowasa and his mob family) to move the country forward? You probably need a psychiatrist!

      Delete
  3. Maneno mengi hatutaki mlimwona hafai Leo hii anawatoa jasho. Hata mseme nini haturidi nyuma. Lowassa tu ndiyo nguzo yetu.

    ReplyDelete
  4. Wewe mdau unaetoa hoja zako kwa lugha ya Kingereza umepotea ilibidi uzipeleke kwa Tramp na Clinton huko ndio kuna wanaoongea na kuandika lugha kama hiyo

    ReplyDelete
  5. na wewe anonymous wa 12:37 kama huelewi kiingereza kajifunze uelewe usiwakataze wenzio kukitumia. kiingereza ni moja ya lugha rasmi za Tanzania(official language)

    ReplyDelete
  6. Makamba angaika na mwanao
    Mwatumu aliyekudaganya nyumba ile ilikuwa yake mkasoma hadi maulidi
    Kumbe si nyumba yake mtu mzima wewe
    Ulifukuzwa kazi ya ualimu kisa kumpa mimba wanafunzi wako sijui in mama wa January au Mwatumu
    Leo unaleta hapa wewe una nini kaaa tegeta yako tuache Lowassa it's our choice
    Tunaichukia CCM Kama hitler

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake