Mungu huyo wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa anayejulikana kwa zaidi ya majina 125 (Ganpati Bappa Morya) mwenye sura ya tembo akiwa amewekwa juu ya gari maalumu wakipita mitaa kadhaa ya jiji la Dar es Salaam jana mchana akipelekwa Baharini ili kuungana na mungu wa kike waliopo kwenye mito mitatu mikubwa mitakatifu iliyopo nchini India.
Wanawake wa madhehebu hayo ya kihindu wakicheza wakati wa kuadhimisho siku hiyo.
Hapa ni furaha tupu ya maadhimisho hayo.
Maandamano yakiendelea.
Hapa ni furaha tupu kwa wanawake, wanaume, wazee na watoto.
Watoto wakifurahia maadhimisho hayo.
Hapa wakiwa juu ya magari kuelekea kumsindikiza mungu wao huyo.
Hapa wakiwa kwenye magari kuelekea baharini.
Ni furaha tupu ndani ya gari.
Safari ya kwenda baharini ikiendelea.
Na Dotto Mwaibale
WATANZANIA wenye asili ya India wa dhehebu la Hindu (Baniani), jana wameadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mungu wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa (Ganpati Bappa Morya) na mwenye sura ya tembo.
Mungu huyo hufanyiwa sherehe baada ya kufanyika kwa ibada ya siku tisa ambapo siku yake ya kuzaliwa alipelekwa baharini kwaajili ya kuungana na Mungu wa kike walio kwenye mito mitatu mitakatifu iliyopo nchini India ambayo ni Sarasgad, Amba na Raigad.
Sherehe hizo zilianza kwa ibada ambapo pia walitumia fursa hiyo kuiombea amani ya nchi hii katika maadhimisho ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa iliambatana na utoaji wa sadaka za vyakula mbalimbali na maombi hupelekwa baharini kwa ajili ya kuungana na Mungu kike.
Katika sherehe hizo jijini hapa zilianzia katika nyumba zao za ibada ambapo kulikuwa na msafara mkubwa ambao ulihusisha na magari yaliyobeba Mungu huyo huku wanawake wakijipamba kwa mavazi mazuri huku wakitembea na kucheza kwa furaha kumsindikiza wakipita barabara kadhaa za katikati ya jiji la Dar es Salaam zikiwemo za Azikiwe na Kivukoni hadi Baharini.
Baada ya kufanyika kwa sherehe hizo pia baada ya miezi miwili kutakuwa na maadhimisho ya mwaka mpya ambao ni Diwali ambapo mwaka ujao wataadhimisha tena sherehe hizo.
Mungu huyo ambaye pia hujulikana kwa majina zaidi ya 125 na ndiye Mungu mdogo na mwenye daraja kubwa zaidi.Baadhi ya majina hayo ni Ganesh Chaturthi, Vinayaka Chaturthi
Inaaminika kuwa unapoomba kitu chochote kutoka kwake unafanikiwa. Ambapo mungu huyo ambaye ni mwanaume aliyetengenezwa kwa aina ya udongo maalumu huyeyuka anapowekwa baharini ikiwa na maana ya kwenda kuungana na Mungu wa kike waliokatika mito hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
1 comment:
Napenda Tanzania, inatoa uhuru kila mtu aabudu anavyotaka, na hiyo ni tabia ya Mungu
Post a Comment