ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 30, 2015

RAIS KIKWETE AAGA UMOJA WA MATAIFA (UN)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana jumanne amelihutubia kwa mara ya mwisho Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mtaifa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba ya Mhe. Rais na ambayo iligusia mambo mengi ya kisiasa, kiuchumi, na maendeleo akitumia pia fursa hiyo kuwaanga viongozi wenzie na kuwashukuru kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake, iliwasisimua wajumbe wa mkutano huo kiasi cha kukatishwa mara kwa mara kwa makofi.

Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazomwonyesha Mhe. Rais katika Matukio mbalimbali Moja wapo likiwa ni hafla ambayo Rais wa Marekani, Mhe Barack Obama aliiandaa kwaajili wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Picha kwa hisani ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Barack Obama na Mkewe Michelle Obama wakati wa hafla ilioandaliwa na Rais wa Marekani kwaajii ya Viongozi wa Wakuu Nchi na Serikali wanaohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ( Picha hii ni kwa hisani ya Ofisi ya Itifaki ya White House)
Mhe. Rais Kikwete akiwa na Mhe. Sophia Simba, Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula na mwanamitindo Flaviana Matata muda mfupi mara baada ya kulihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa
Mwakilishi wa Kudumu wa Antigua na Bermuda Balozi Walton Alfonso Webson ambaye ni mlemavu wa kutoona akimwongoza Mhe. Rais Kikwete kwenda kuonana na Waziri Mkuu wake, Mhe. Gaston Alphoso Browne aliyekuwa na mazungumzo wa Mhe.Rais mara baada ya Mhe. Rais kulihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa.

  Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Mhe. Gaston Alphonso Browne, wengine katika mazungumzo hayo ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa kudumu wa Antigua na Barbuda, Balozi Walton Webson mwenye miwani myeusi na Mkurungezi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestin Mushy

1 comment:

Anonymous said...

Dr kikwete amesema anajiandaa kurudi kijijini kwake akalime mananasi akisha staafu lakini sidhani kama nafasi hiyo ataipata. Namuona kikwete huko aendako katika maisha yake ya kustaafu kuwa mtu mmoja muhimu zaidi katika taasisi ya umoja wa mataifa hasa kuwa kiungo muhimu zaidi katika masuala yanalolihusu bara la afrika simuoni kiongozi mwengine yeyote wa Africa anaekubalika duniani kwa sasa zaidi ya kikwete na ndio maana washauri wa kisiasa wa Marekani walimshauri obama ili kuijijijengea heshima katika kazi yake wakati anaingia madarakani itakapkuja wakati wa kukutana na viongozi wa Africa basi asije akafanya kosa isipokuwa kiongozi huyo wa Africa lazima awe kikwete wenzetu taasisi zao za kijasusi zinafanya kazi za aina mbali mbali si usalama wa taifa pekee yake. Vile vile tunampongeza mheshimiwa kikwete kwa hutuba yake nzuri kabisa, hutuba ambayo imesimamia sifa na msimamo wa Tanzania kuwa taifa lisilo egemea upande wowote katika kusimamia haki za mataifa mengine. Suala la wapalestine na waizraili linataka ujasiri kutamka wazi kwamba wapalestine wanastahiki kuwa na taifa lao. Kwa kweli kuna mataifa makubwa yana nguvu yakifika katika suala hilo yanuufiata kabisa hata hao ndugu zao wa kiarabu wakifika pale katika suala la wapalestine wanumunyamunya au wanaufiata kabisa. Nina baadhi ya rafiki zangu wa kimisri walishangazwa kabisa na jinsi kiingozi wetu kuenda pale umoja wa mataifa na kuzungumza suala zito kabisa kama lile bila woga wanasema wanaiheshimu Tanzania sana kutokana msimamo wake huo lakini vile vile ni aibu kubwa kwa mataifa ya kiarabu kuona kuwa kijinchi kama Tanzania kinakuwa na kauli yake wao wakishindwa kufanya hivyo. Vile vile suala la kiuba ni moja ya suala ambalo mataifa mengi yakihofu kusema chochote kuhusiana na suala hilo kwa kuihofu marekani lakini tumeona Tanzania suala hilo limekuwa likizungumzwa na viongozi wetu kabla na kwa kweli faraja ilioje kwa dunia kuona kuwa marekani wameamua kulitafutia ufumbuzi suala hilo kwa njia ya mazungumzo kwani imezoeleka marekani kuwa na falsafa ya kutumia nguvu zaidi kuliko dialogue kama mueshimiwa kikwete alivyo ainisha na kusisitiza kwamba marekani wanapaswa kuwaondoshea wakiuba vikwazo vilivyo bakia kwa kweli ni kauli nzito kutolewa na kiongozi wa nchi kama tanzania hongera sana mheshimiwa.