ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 30, 2015

AUDIO : LEMBELI AELEZA HATMA YAKE BAADA YA KUUKOSA UBUNGE, AJIBU TETESI JUU YAKE IKIWEMO YA KUUZA REDIO YAKE


Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama Mjini, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.

Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.

Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.


Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.


Kuhusu afya yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa.

BONYEZA PLAY HAPA CHINI

3 comments:

Anonymous said...

Blah blah blah! Umeshindwa ubunge simple sema umeshindwa na kumpongeza alie kushinda uchaguzi kwisha habari. Hivyo mbona hawa watu wa chadema/ukawa kwanini wanakuwa watu wa hovyo sana? Mabadiliko gani wanayotaka kutuletea Tanzania ? Mabadiliko ya mtu akishindwa uchaguzi kukataa matekeo?

Unknown said...

annon hapo juu naunga hoja, sijui waafrika wamelaaniwa? kukubali matokeo ngumu sana kwanini?? mbona wenzetu chaguzi zao zinaisha kwa amani na maisha yanaendelea?? CDM kubalini matokeo then mjipange upya!

Anonymous said...

Ngw'wanaLembeli humulaga lulu Mami.
Uriruka mkojo sasa umekanyaga nini? Ukamfanyia vibaya Maige na sasa nawe yamekupata huna la kufanya sasa.