Advertisements

Thursday, September 3, 2015

MKE HALALI WA NDOA WA DK.WILBROD SLAA, MBUNGE ROSE KAMILI AMLIPUA DR SLAA


Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chadema,Rose Kamili,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo jioni kuhusiana na tuhuma alizozitoa mume wake kwamba waliishi kwa maisha ya kula mihogo na familia yake ili kuhakikisha chadema inastawi na kuimarika jambo ambalo si la kweli walikuwa na maisha mazuri ya kawaida tu na kusema kuwa Dk.Slaa anapaswa awaombe radhi wataznzania kwa kufafanisha kula mihogo kuwa ni umaskini na kuongeza kwa kusema mbona ukienda katika mahoteli makubwa mihogo na viazi ipo na watu wenye pesa zao wanakula kama kawada.
akizungumzuia kuhusu matamshi aliyasema Dk.Slaa kwamba haongei na waziri mkuu mstaafu,Sumaye,mama rose kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita waziri mkuu huyo mstaafu aliomba namba za dk.slaa akampatia wakaongea vizuri bila shida yoyote ila anamshangaa juzi aliposema mbele ya waandishi wa habari kwamba hazungumzi na sumaye.
akizungumzia kuhusu kuja kwa lowassa chadema mama huyo alisema kuwa Dk.slaa alikuwepo katika kumkaribisha waziri mkuu mstaafu,Edward Lowassa kujiunga na chama hicho ni jambo la kushangaza akizungumza kwamba hakushiriki na pia wakati chokochoko hizo za kustaafu ukatibu wake alisema kuwa viongozi waandamizi wa chama cha mapinduzi walimfuata na kumshawishi kutoludi kwenye ukatibu mkuu wake huo atapewa ubunge wa kuteuliwa na rais atakayeapishwa na kupewa uwaziri katika serikali ya awamu ya tano.

Kamili alimaliza kwa kutoa rai kwa watanzania wote nchini kutomsikiliza Dk.Wilbrod Slaa na kuwasihi kuendelea kuwa na matumaini na mgombea wa urais wa Chadema,Edward Lowassa aliyesimamishwa na chama chao pamoja na umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa) ili kukiondoa madarakani chama tawala.
Linus Slaa.
Emiliana Slaa.
Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kushoto ni mtoto wake aliyezaa na Dk.Slaa aitwaye,Emiliana Slaa.
Mama Rose Kamili akizungumza kwa hisia kali.kulia ni mtoto wake, Linus Slaa.
waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini leo
Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Rose Kamili, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mume wake Dk.Wilbrod Slaa kuzungumza wakati akiwa Katibu mkuu wa chadema familia yake ilikula kwa shida kwa sababu ya kujenga chama hicho jambo ambalo si la kweli. Wengineo ni watoto wake, Linus Slaa (kulia) na Emiliana Slaa.
SOURCE:HABARI TANZANIA

17 comments:

Anonymous said...

Shame on you, tofauti zenu na Slaa ni personal.Si busara kuzifanya kuwa ni Public issue.

Anonymous said...

si mke wa slaa, sasa wewe mwenye blog unaharibu siku ya mtu. walishaachana siku na inabidi uwe mwangalifu na sharia ya mtandao.

Anonymous said...

Mwendawazimu huyo mwanamke kutumia issue personal kama shida ya taifa.

Ujinga kabisa kuchuku wanao kwenda kusema vibaya baba yao. No wonder alikuwacha!

Na hii hata kwa wababa wa kibongo wanao tumia watoto kukomoa wakina mama wote mlaaniwe!

Anonymous said...

Halafu wewe Dj Luke embu acheni kupotosha uma! Huyo SI MKE HALALI WA DR. WALISH achana na wanataka halali kabisa. Kuwa muangalifu you can be sued for defamation!

Anonymous said...

Hana hoja huyu mama wala sijui ameongea nini? Mchumia tumbo.

Anonymous said...

Wasomaji n8 vyema mkasoma alichosema mbona alichotamka Dr. Sl. Mmekielewa? Hakuna hata mmoja wenunkati ya mnaokataa mliomegewa ile $ laki tanonaliyokabidhiwa mkewe na akamlaza nje.. Ukweli ndio huo nani kakuambia Dr anaweza kula.mihogo anayokula mlala hoi. Acheni ukubali usiokuwa na njia. Mnamlaumu Dj wa blog hii kwani amepotosha kitu gani sheria ya mtandaomsiomkwa kitu kama hiki acheni yako yenyewe someni. Ameripoti kilichotendeka na waandishi wa habari kwani hakuwa mke wake wa halali hadi walipoachana. Dr. Ana matatizo hata hawa watoto aliwatupa sembuse chama!! Basi tungojee apewe huo ubunge tuone atapita kwa wananchi wepi!!

Anonymous said...

Kabisa huyu mama ameamua kuuza utu wake na familia yake kwa vijisenti vichache na nyinyi chadema na ukawa kama mnafikiri mnamokomoa dk slaa kwa kumtumia huyo mwanamke asie jitambua ili amtukane mzee mwenzake hiyo laana itakurejeeni na kukuadhibuni. Na huu ni mfano mwengine m'baya unaavyoonyesha jinsi gani lowasa alivyo tayari kwa njia yeyote ile kutumia pesa zake chafu kukimbilia ikulu hata kwa kuisambaratisha familia mtu hii ni hatari.

Anonymous said...

WEE bibi ebu nenda kwa bit kisungura ukafundwe ,unatoleteaje apa mambo ya chumbani eboo? apa tunataka sera za maana sio mabishano ya chumbani .mume ndio kashasema mlikua mnakula mihogo sasa cha ajabu nini ,afadhali angesema mnalilia kitanda cha fit 4 kwa 4 ningekuelewa shame on you .

Anonymous said...

Kumbe kweli kwamba mwanamke mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe!mama ni wivu tu umekutawala!huba jipya!waache wenyehoja zao wajibu tuhuma zao wewe endelea na yako

Anonymous said...

mihogo ni chakula cha kimaskini. hapa duniani vipo vyakula wanakula matajiri kikawaida kwa ughali wake lakini mihogo wengi wanaokula ni maskini

Anonymous said...

HIZO NDIO SIASA, NA HUYU MAMA NI MWANASIASA/MBUNGE PAMOJA NA KUWA ALIWAHI KUWA MWANA SIASA. KABLA HATUJAMNYOOSHEA KIDOLE, TUKUBALI KUWA HUYU MAMA ANAHAKI KAMA MWANASIASA KUTOA DUKU DUKU LAKE, PAMOJA NA KUELEZEA KWA KINAGA UBAGA DR SLAA NI NANI. YAANI KABLA HATUJAMUAMINI DR. SLAA, TUMTAMBUE TABIA ZAKE NA KWANINI ANABADILIKA KAMA KINYONGA.

Anonymous said...

Wote hapo juu unaweka ujumbe kwa jabzi ya u-CCM. Sina chama lakini na judge facts Huyu mama ni mke wa ndoa wa slaa na anawatoto naye hivyo status yake bado ni mke. Slaa ametengana na mke wake hawajaacha. Hilo nimoja ndoa za wakristo huwa wanatengana the most. Hao watoto ni wakubwa Sana unawezakuta na wao wana watoto pia hivyo kuwepo kwao hapo is just to support their mom due to their dad rubbish ness hawakulazimishwa sababu wana ufahamu wa mema na mabaya. Kuhusu tuhuma kwamba anaongea mambo ya familia hilo naona ameanzisha Slaa kwa kuudanganya umma na wa TZ anakula muhogo na familia wakati yupo Serena hotel kwa kutumia mamillion ya Tsh ambazo mdhamini hajulikani na hataki kumtaja. Kuwaita MP Sumaye Mr. Zero ni upungufu wa hekima. Slaa la hawala yake Josephine ( anaishi na Slaa bila ndoa)!waliukamia Sana urais walitaka kumtumia Lowasa Kama Kiki ya yeye kuingia ikulu wenzake wanamzidi akili ndiyo maana anakuwa na jazba.hivyo basi DJ Luke yupo sawa kumwita huyu mama mke. Na mama kazungumza sahihi na nadhani amekuwa mstaarabu Sana maana angekuwa mwanamke mwingine amemwacha uchi huyu Slaa.

Anonymous said...

Mama ana haki ya kile alichokisema. Kwanza amesema kwa heshima kubwa. Nadhani kazi ipo kwa Dr. Slaa sasa kuja kuyakataa aliyosema huyu mama.
Ndio ni siasa lakini ni ukweli pia. Wanaolalamika labda watueleze yafuatayo;
Ni haki kwa Slaa kuongea personal issue lakini si haki kwa mke wake?
Hii inaonesha hekima ya vyama vinavyotaka kuitawala Tanzania. Slaa katumia usalama wa taifa, Mwakyembe na mamillion ya pesa kuharibu lakini wenzake wametumia fraction of that amount ku strike back. What does that tell you? Be smart.
Slaa ataumbuka zaidi. Kuna mambo yataanza kuja live atashindwa kuyaongelea.

Anonymous said...

Jamani, mama huyu anahaki kama vile sisi wote tulivyo nayo hata kuandika hapa. Kitu cha kujiuliza ni huyu Dr. Slaa ambaye alishindwa u-padre; akashindwa maisha ya ndoa na kuishia kutelekeza familia yake ikiwa pamoja na watoto wazuri kabisa ambapo kuna watu wengine hata hawana uzazi, badala yake akachagua kuishi na kimada. Sasa ameshindwa siasa, ambayo pengine aliingia pasipo kuijua vema. Huyu bwa Dokta, Padre na sasa ex-politician kusema kweli hana uvumilivu. Maisha ni uvumilivu; iwe u-padre; ndoa; na hata siasa. Huyu ni wale watu hujifanya "Holier than thou" yaani wao ni wasafi wasiokuwa na dhambi, ila wengine wote ndiyo wana dhambi. Kila binadamu ana mapungufu. Anahitaji kuongea na mtu anayemuona kwenye kioo anapochana nywele, ajitafakari vema. Kwanza kuingia kwake Chadema ni kwamba alikataliwa CCM...na sasa hao hao kina Mwakyembe wanamrubuni wakati wao wanaishi na wake zao...! PEOPLE, LET'S DO THE RIGHT THING, NOW. Wakati ni huu.

Anonymous said...

Wewe ndo utafiti facts zako kabla ya kuandika ujinga wako hapa.

SLAA ALISHA ACHANA NA HUYU MAMA NA ANA TALAKA KABISA HATA UKISIKILIZA HOTUBA YA DR SLAA YA JUZI AMELIZUNGUMZIA HILI.

MTU AMBAYE AJAPATA TALAKA NI JOSEPHINE KWASABABU ZA KISASA MME WAKE ALISHIRIKIANA NA WANASIASA KUWEKA PINGAMIZI ASINGE NDOA NA DR. NA PIA HUYO X-HUSBAND AMEKAA KUSIGN TALAKA.

Anonymous said...

Hivi mtu akitelekeza familia yake anatawezaje ku keep in touch with you?? Anabadili number ya simu ambayo hataki kuwasiliana na mtu lakini anampa huyu mwanamke ambaye anadai amemtelekeza; inaingia akili ni hiyo? Kwanini akeep mawasiliano kama kweli nia yake na kutelekeza??

Halafu mtoto mkubwa hiyo labda wao ndo hawataki kuwasiliana na baba yao kutokana na chuki ambazo wamepandikizwa na mama yao?? Acha ujinga wa kutetea ushenzi huu!

Anonymous said...

Lakina huyu mama bila kutambua yeye kuwa ni kioo cha jamii!!! Ata afanye yasiyopendeza mbele ya umma jamani!!!!!!!

Zaidi ninasikitika ata watoto nao!!! Sawa inawezekana wanashinikizwa lakini ni wakubwa wanajitambu wanaweuwezo wa kuchanganua kuwa hili halifai/linafaa.

Dr.ni baba yao hawezi kubadilika kwao.
Ninawasii sana watoto hawa kutofungamana na mawazo potofu kutoka kwa mama yao.