Advertisements

Tuesday, October 13, 2015

BALOZI JUMA MWAPACHU KUJIVUA RASMI UANACHAMA CCM KESHO

NAJIVUA UANACHAMA WA CCM
Ndugu zangu,
Kesho ni siku muhimu katika kalenda ya Taifa letu. Tunamkumbuka marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetutoka miaka 16 iliyopita. Nadhani ni siku mwafaka kwangu kufanya maamuzi magumu katika maisha yangu ambayo yanahusu uanasiasa wangu. Mimi ni mwanachama wa CCM tangu mwaka 1967 wakati nilipojiunga na TANU Youth League. Nimepata fursa ya kuwa kiongozi ndani ya Chama hiki. Lakini kuanzia kesho mimi si mwanachama wa CCM tena. Natoa maelezo yafuatayo:

Kwa kipindi chapata mwezi na nusu hivi sasa mmekuwa mkisoma makala zangu kuhusu msimamo na mwelekeo wangu katika masuala ya siasa za hapa nchini hususan kuhusu uchaguzi mkuu na mstakabali wa demokrasia nchini mwetu. Nyote mnatambua kwamba kuanzia mchakato wa kumpata mgombe wa Urais ndani ya CCM kule Dodoma, ambako nilipiga kambi, sijayumba katika msimamo wangu kwamba Edward Ngoyai Lowassa ndiye chaguo langu katika kampeni za kumpata Rais mpya wa Taifa letu.

Chaguo langu si ndoto wala mlipuko wa mapenzi juu ya Lowassa. Nimemfahamu Lowassa tangu miaka ya 90 nikiwa cadre wa Chama cha Mapinduzi kwa mahusisho katika majukumu ya Kichama. Lowassa amejaaliwa nuru na uwezo wa kuongoza na wa kupendwa na watu. Ni msikivu pamoja na kwamba ni kiongozi asiyependa ukiritimba na utovu wa nidhamu, iwe kwa upande wa watumishi au wananchi wenyewe. Kubwa kwake ni ucha Mungu wake ambao unamsaidia sana katika uongozi unaojali na kuheshimu utu, ukweli na uwazi. Wanaodhani au kutaharuki kwamba eti anaweza au ana hulka ya kulipiza kisasi kwa jambo lolote lile ni waongo; wanajilinda.

Lowassa ni chaguo la wengi na CCM, katika busara yake ya kumuengua katika mchakato wa kumpata mgombea wa Urais, kimedhihirisha kutokuwa Chama kinachoendeshwa kwa misingi ya demokrasia. Dalili za Chama hiki kupoteza lengo la kuwa Chama cha watu, na kuwa cha viongozi wachache zilianza siku nyingi na hasa katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. CCM kimebadilika na kuwa Chama cha makundi na migawanyiko yakupambana, si kwa malengo ya itikadi na ujenzi wa Chama, bali ya kumalizana na kutaka kufukuzana.

Lowassa angeweza kufukuzwa miaka mingi tu iliyopita! Aliweza kushinda vita hivyo kutokana na kupendwa na wengi ndani ya CCM. Hivyo, kujitoa kwake uanachama wa CCM hivi karibuni ni sahihi kabisa kwasababu CCM si Chama tena cha watu. Kimetekwa. Na mimi nakubaliana na msimamo wa Lowassa na hao waliyofuata kutoka nadani ya CCM.

Niliwahi kuandika makala katika ukurasa huu nikimnukuu mshairi mmoja wa Uingereza aliyeandika kwamba, ‘there comes a time when the door opens and allows the future in’. Mlango huo sasa umefunguka usoni mwangu na huu uamuzi wangu maana yake ni kukubali kwamba wakati mpya umewadia; ni wakati wa mabadiliko. Kuendelea kujihisi kwamba ningali mwana CCM wa kadi ni kukubali kujidanganya mwenyewe. Si sawa. Kama marehemu Baba wa Taifa alivyowahi kusema, ‘CCM si mama yangu’.

Hivyo ndugu zangu, kuanzia kesho mimi si mwana CCM tena. Nitarejesha rasmi kadi yangu kupitia ofisi ya CCM ya kata yangu Mikocheni, Dar-es-Salaam. Kwa sasa sijaamua kujiunga na Chama kingine.

Mwenyezi Mungu anilinde.

11 comments:

Anonymous said...

Je,mzee Mwapachu anatambua kuwa utaratibu wa kumpa Lowasa nafasi ya kuwa mgombea ndani ya Chadema ulinajisiwa ?
Yeye aeleze kuwa ana mapenzi na Lowasa asiongelee swala la kukiukwa taratibu..

Anonymous said...

Kaji shtukia kaona atapigwa ridandasiii ya ukwelii kaamua kusepa mapema ,,, na bado watahama wengiii

Anonymous said...

Wakina Mwapachu, wakina Kingunge na wengine ambao bado mnatangatanga mnajua kitakachofuata baada ya Magufuli kuapishwa kuwa Rais , ni vizuri sana maana mnajua hakuna lelemama tena Tinga Tinga likishaingia kazini ni 'KAZI TU' Asante Baba wa mbinguni Kwa kutupatia Rais anayefuata nyayo. Za Baba wa Taifa Marehemu Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Endelea kumpumzisha Kwa Amani!!

Anonymous said...

huyu mzee si alikuwa mpiga deal na Mohamed Hassan diria za unga, sasa anasema kitu gani tena hanyamaze. mafisadi utawajua tu,ondokeni nendeni chadema ndio kuna nafasi zenu mkaendeleze ufisadi. wewe nani asiyekujua ulikuwa mmojawapo wa mafisadi katika serikali ya awamu ya pili, wote magufuli atawashughulikia subirini muone. upenzi wako kwa lowasa usituletee sisi watanzania oooh, eti utaratibu haukufuatwa acha kupotosha watanzania mzee mzima huna aibu, majina matano yalipelekwa nec kama katiba ya ccm inavyosema, yakapigiwa kura yakapelekwa yakapatikana matatu yakapelekwa mkutano mkuu na mkutano ukapiga kura wakampata Magufuli, sasa utaratibu gani unaousema na kwa katiba ya chama ipi???!!! huyo fisadi mwenzako huko chadema kachaguliwa na nani na kwa utaratibu gani, wazee mnazeeka vibaya na mnajivunjia heshima zenu.kaa nyumbani cheza na wajukuu hatutaki kusikia ujinga na upotoshaji wako hapa. luka usiibanie hii ni katika kuelimisha na kuweka mambo sawa.

Unknown said...

Ni kwel mtu kama unampenda inauma lakini watanzania tujifunze kuvumiliana na kuheshimiana kwani tumeumbwa na utashi tofauti. ninachoshukuru kipindi hiki ni nikizuri kwamba mambo haya yanatokea wakati nchi imekua kiutawala na demokrasia imekua kiasi kwamba kwa matukio yote haya watanzania tutaendelea kutofautiana kiitikadi lakini hatutagombana tutaendelea kuwa wamoja. Hongera kwa awamu zote nne ambazo zimepita kila mmoja ametimiza wajibu wake . Atakayeshika kijiti atamalizia yaliyosalia bila kulipiza kisasi chochote
akijua nafasi hiyo ya juu ni Mwenyezi Mungu amampa kupitia kura za wananchi.

Unknown said...
This comment has been removed by the author.
Unknown said...

Raisi kikwete baada ya kuona CCM imevamiwa na majambazi waliokuwa wakikitafuna chama hicho hadi kufikia watanzania kutamka wazi kwamba watakihama chama hicho kwa kuwa kina mafisadi waliojenga mtandao wa ufisadi ndani yake. Kikwete aliwataka wale wote walio na sifa chafu ya ufisadi wajivuwe gamba, lakini kwa bahati mbaya hawakufanya hivyo walibakia ndani ya chama hicho badala yake mafisadi hao walitengeneza mikakati ya kuhakikisha moja ya mafisadi hao anapita kuwa raisi na kukiteka chama cha na vnchi kwa ujumla. Kwa hivyo mkakati wao wa kwanza ulikuwa kutotii amri ya mwenyekiti wao wa chama kwa kutojivua gamba kwa kujua mwenye kiti huyo hana muda madarakani na wao katika kundi lao la mafisadi kuna uwezekano mkubwa wa kumuweka mwenyekiti wao ili kuwalinda mafisadi wengine. Kwa wanaefanya kazi wanasema watanzania itawachukuwa muda kupata raisi wa watu, makini, muadilifu, mtaalamu wa mambo ya nchi za nje na mtu mwenye hisia za kibinaadamu na huruma kama kikwete, lakini tatizo hiyo huruma ya kikwete kwa watendaji wake, mafisadi walichukulia advantage kuendeleza ufisadi wao. Sasa katika mikakati ya mafisadi kuhakikisha wanapitisha mgombea wao kwa ticketi ya uraisi mkakati waliouweka ni kuingiza wagombea wengi miongoni mwao kwa maana ya kwamba mmoja wao lazima atapita katika kinyangiro hicho na walikuwa wameshamchagua nani kati yao bali wengine walikuwa ni escort wake tu kumsafishia njia. Kama mungu magufuli alipotokea hakukujulikani wapi mtu ambae mafisadi kwao ni sawa na kuangukiwa na maafa makubwa wasiyatarajia, Sasa kilichotekea kwa mafisadi hao ni kuanza kutimka hovyo kutoka CCM kwa kisingizio cha ufisadi ndani ya CCM kumbe wao ndio mafisadi wakijua fika juu ya uongozi wa magufuli jinsi atakavyo pambana na ufisadi ndani ya chama hicho lazima patachimbika sasa wanajaribu kuunganisha nguvu zao za ufisadi kupitia upizani ili kumkabili magufuli wakijua fika magufuli anapozungumza kwamba ataunda mahakama ya kushughulikia mafisadi mara tu atakapochaguliwa kuwa raisi hatanii bali sheri itafuata mkondo wake. Kwa hivyo Mapachu, Sumaye, lowasa na washirika wao ni watu waliokuwa wanakitafuna chama cha mapinduzi kwa ufisadi na kuondoka kwao CCM ni kama mgonjwa aliendokewa na maradhi mazito yaliokuwa yakimtesa kwa muda mrefu sana na sasa anaanza kupata nafuu . Tunaimani Tanzania na CCM ya magufuli itakuwa na manufaa kwa watanzania wote.

Mungu ibariki Tanzania.Amen

Anonymous said...

Nakubaliana na yote yaliyosemwa hapo juu. Siku za mafisadi zimefika na wala kiota chao wanachokikimbilia hakitawasaidia. Tunachotaka ni haki kwa Watanzania wote. Hapa Ni Kazi Tu.

Anonymous said...

Hana chochote huyu bwana kazi yake ilikuwa kujikomba kwa wakubwa tu hivyo kuondoka kwake ni kuwafuata hao aliokuwa anajipendekeza kwao. Kwa ajili anapenda vyeo anafikiria kuwa hao jamaa zake wakivuka daraja watampatia cheo huko. Bahati mbaya Ukawa hawaingii Ikulu hivyo alie tu.

Anonymous said...

kweli umelipwa kama yote ni kweli mbona katiba inayosema kuwajibisha hao wakubwa ccm wameikataa na kiwango cha elimu cha mbinge kiongezwe pia kimekataliwa.
Raisi miaka kumi kashindwa kuwatoa hao mafisadi kama alikuwa anauchungu kweli. Pia uwezo anao ...ila tunaona watu kuteuliwa na kama hii no democracy basi nchi iko pabaya.
Huyo Raisi mpya atakuja na wanachama ni wale wale na system ile ile kwa vile ni wimbo tulishausikia siku nyingi tu.
Sidhani kama kuna jipya maana hauhitaji new President kutekeleza maadili ya kuwatoa mafisadi.
Raisi mpya akishindwa mtasemamwingine afanye isnt that the same song we heard in 2004.
wasomi wengi and its time for change its better to try than to have same apples planted and hoping to get beans.
Kama unabisha i am sure una watoto please take them to the same school uliyosoma and see if wataweza pata elimu.
Change is coming hata mseme nini.

Anonymous said...

Alikuwa mwenyekiti wa TYL (Vijana wa TANU) Mlimani wakati wa Enzi zao. Lakini wanachama wa TYL waliupiga vote of no confidence uongozi wake na kumpindua huyo Juma Voltare Mwapachu kutokana na kujipendekeza kwa viongozi wa TYL/TANU hapo Makao makuu Lumumba, ikiwa ni pamoja na ufisadi wa kutumia kombi ya TYL kwa maslahi ya ubinafsi.Na tokea hapo hakuwa na uongoozi wa TYL au TANU.