Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kada wa CCM, Balozi Juma Mwapachu (kulia) akikabidhi kadi kwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mtaa wa Mikocheni A Sudi Odemba (kushoto) katika ofisi za chama hicho kata ya Mikocheni, Dar es Salaam leo. Picha Nuzlack
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kada wa CCM, Balozi Juma Mwapachu leo amerudisha kadi ya uanachama katika ofisi za CCM Kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Amesema anajiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kwamba baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 atatangaza chama anachojiunga miongoni mwa Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vinavyounda umoja huo.
Mwapachu amesema haoni sababu ya kutaja chama hicho sasa kwa vile lililo muhimu kwao hivi sasa ni umoja miongoni wanamabadiliko si kujipambanua katika imani ya chama cha siasa hakuwezi kuwa na tija kwa umoja huo.
Amesema Lowassa anakwenda kuwa Rais wa Wanaukawa wote, hivyo watu wote wanaoamini katika mabadiliko ndani ya vyama hivyo wanapaswa kuwa wamoja kwa kuuwezesha umoja huo kuibuka na ushindi.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba amesema chama chake hakitapata madhara yoyote kutokana na hatua ya Balozi Mwapachu kijiengua na kutangaza kujiunga Ukawa.
Amesema Mwapachu hakuwa mwanachama aliyejitoa kukisaidia chama katika siku za karibuni na kwamba hajawahi kushiriki mikakati thabiti ya kukipatia CCM ushindi katika ngazi ya mtaa japo chama hicho kiliweza kuibuka na ushindi wa kishindo.
Jumanne wiki hii, Balozi Mwapachu alitangaza kujitoa CCM akikituhumu kukiuka misingi ya kidemokrasia wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais Julai mwaka huu ambapo Dk John Magufuli alichaguliwa huku mgombea anayeamini kuwa na maono ya kiuongozi kwa Tanzania ijayo, Edward Lowassa akikatwa.
4 comments:
Aibu kwako balozi, baada ya kutajirishwa na CCM sasa unatuachia kinyesi chako? All that has to do with greed, because you know deep inside, Dr. Magufuli hawezi kukupa kazi. Unfortunately, Lowasa hatakuwa Rais, jee utafanya nini?
Funga domo lako wewe utawafuata wenzio akhera
Aibu gani
Kila Mtu ana maamuzi yake ,wapo wengi Kama yeye wengine ni waoga lakini maamuzi Yao yako Kama yake watayafanya kwenye sanduku la kura
It's Lowassa Lowassa aliyesemwa mgonjwa Na Kila mwana CCM , mungu anaonyesha uwezo wake hata kabla ya uchaguzi
Kuondoka kwake CCM ni auheni na CCM itashinda hata bila ya watu kama hawa kuwepo ndani ya chama. Kwanza uelewe huyu bwana anawakejeli kwani ajenda yake ambayo siyo vigumu kuifahamu. Ni ndumila kuwili. Anarudisha kadi CCM ili CCM wamuone kuwa yeye ni muungwana na hivyo Ukawa anakotarajia kupewa cheo wakishindwa uchaguzi ajirudi. Tumeona wengi wanaohama vyama na wakifanya hivyo wanatoa kadi zao kwenye uongozi wa vyama vyao vipya kama kielelezo hasa wakati huu wa kampeni la sivyo wanavitelekeza tu. Sasa huyu mwenzetu bado ana muda tena wa kwenda kujipendekeza kwenye chama ambacho anaona hakina thamani kwake!!!
Post a Comment