ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 31, 2015

BALOZI WA TANZANIA OTTAWA-CANADA, Mhe. JACK MUGENDI ZOKA, AMBAYE PIA NI MWAKILISHI WA TANZANIA NCHINI CUBA, AWASILISHA NAKALA ZA HATI ZA UWAKILISHI

Kuanzia tarehe 16 hadi 21 Septemba, 2015 Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka alifanya ziara nchini Cuba kwa lengo la kuwasilisha nakala za Hati za Uwakilishi (Letters of Credence) kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba.

Aliwasilisha Hati hizo tarehe 18 Septemba, 2015 kwa Mhe. Ana Teresita Gonzalez Fraga, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba aliyezipokea kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Bruno Rodriguez Parrilla.

Matukio katika picha.
Pichani ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe Ana Teresita Gonzalez Fraga (Mwenye gauni nyekundu) akisalimiana na kumkaribisha Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka (Mwenye tai ya kijani)mara baada ya kuwasili Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba. Aliyesimama nyuma ya Mhe. Balozi Jack M. Zoka ni Afisa wa Mambo ya Nje, Bw. Paul James Makelele.
Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akikabidhi nakala za Hati za Uwakilishi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe Ana Teresita Gonzalez Fraga (Mwenye gauni nyekundu)
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe Ana Teresita Gonzalez Fraga (Mwenye gauni nyekundu)akimpa mmoja wa maafisa wa Wizara ya mambo ya Nje wa Cuba (hayupo pichani) nakala za Hati za Uwakilishi mara baada ya kuzipokea rasmi kutoka kwa Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka.
Mara baada ya kukabidhi hati, yalifuata mazungumzo ya pamoja kuhusu ushirikiano wa nchi za Tanzania na Cuba. Kutoka kushoto ni Afisa wa Mambo ya Nje, Bw. Paul Makelel, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Afisa wa Mambo ya Nje wa Cuba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe Ana Teresita Gonzalez Fraga na Afisa wa Mambo ya Nje wa Cuba.
Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo ya pamoja kuhusu ushirikiano wa nchi za Tanzania na Cuba wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe Ana Teresita Gonzalez Fraga (kulia) na Afisa wa Mambo ya Nje wa Cuba (katikati)wakisikiliza kwa makini.

No comments: