ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 30, 2015

BALOZI ZOKA AWASILISHA HATI ZA UWAKILISHI KWA MAKAMU WA RAIS WA CUBA



Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka pamoja na ujumbe wake wakiwasili katika Ikulu ya Makamu wa Rais ijulikanayo kama Revolutionary Palace.
Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akikabidhi Hati za Uwakilishi kwa Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ikulu ijulikanayo kama Revolutionary Palace.

Balozi wa Tanzania nchini Canada na Cuba Mhe. Jack Mugendi Zoka aliwasilisha Hati za Uwakilishi kwa Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ikulu ya nchi hiyo ijulikanayo kama ´Revolutionary Palace´.

Mhe. Balozi aliambatana na Mama Balozi Bibi Esther Zoka na Afisa wa Ubalozi Bw. Paul Makelele. Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba, Mhe. Balozi Miguel Lamazares Puello na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ofisi ya Makamu wa Rais.

Baada ya zoezi hilo, Mhe. Balozi Zoka alipata fursa ya kuwa na mazungumzo na Mhe. Makamu wa Rais. Baada ya zoezi la kuwasilisha Hati na mazungumzo, Balozi alitembelea eneo la kumbukumbu - Memorial Square ijulikanayo kama Jose Marti ambapo aliweka Shada la Maua, kutembezwa na kupewa maelezo ya historia kuhusu ukombozi wa nchi hiyo inayomtambua Jose Marti kama shujaa na muasisi wa ukombozi wa Cuba.
Mara baada ya kukabidhi hati, yalifuata mazungumzo ya pamoja kuhusu ushirikiano wa nchi za Tanzania na Cuba. Kutoka kushoto ni Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa, na maafisa wa Ikulu ya Cuba.
Picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa, Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka na mshauri wa Makamu wa Rais wa Cuba.
Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akiweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu (memorial square) kwa heshima ya mwanamapindizu, Jose Marti, shujaa na mhasisis wa Cuba.
Picha ya kumbukumbu mara baada ya kuweka shada la maua. Kutoka kushoto ni askari wa Cuba mwenye mkumbulu, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Afisa wa Mambo ya Nje, Bw. Paul James Makelele na mshauri wa Makamu wa Rais wa Cuba. Wa nyuma ni maaskari wa Cuba.

No comments: