Mwanasheria wa Chadema, John Mallya, aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwa barua hiyo waliituma UN jana.
Mallya alisema lengo la barua ni kumshtaki Rais Kikwete kwa mataifa mengine kutokana na kauli yake ya kuwatisha Watanzania aliyodai aliitoa Oktoba 14, mwaka huu ya kuwataka wapigakura kuondoka kituoni baada ya kupiga kura na endapo watakiuka watashughulikiwa.
Mallya alisema kauli ya Rais Kikwete ni kinyume cha Sheria ya Uchaguzi inayomtaka mpigakura kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura.
“Kwa sababu Rais Kikwete hatuwezi kumshtaki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, ziko mamlaka ambazo tunatumia kumshtaki kama tulivyofanya kuiandikia barua UN na kupeleka nakala Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika, Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai na kusainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari,” alisema Mallya.
Kuhusu wananchi kukaa mita 200, Mwanasheria huyo wa Chadema alisema jambo hilo ni kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1985 kifungu cha 104 inayomruhusu mpigakura kukaa nje ya mita hizo.
“Mwananchi haruhusiwi kukaa maeneo hayo akiwa na sare, nembo za vyama au kufanya alama zozote za kuashiria kampeni, lakini ukiwa nje ya mita hizo 200, unaweza kufanya jambo lolote hata kampeni,” alisema Mallya.
Akizungumzia suala la kuhamasisha amani wakati huu wa kuelekea kupiga kura na kutangazwa kwa matokeo, Mallya alisema chama hicho kinahubiri amani, lakini hakiwezi kukaa kimya endapo kutakuwapo uvunjifu wa sheria.
“Serikali na Tume, ifuate sheria kwa kuwapa wananchi wake haki ya kupiga kura na kulinda kura zao. Chadema kinahubiri amani na kinalinda amani, lakini hatutakaa kimya kama sheria zitavunjwa,” alisisitiza.
CHANZO: NIPASHE
3 comments:
Hii yakura kulindwa na wanachi wao chadema wameiona wapi ? Hao mawakala wao wanawowakilisha wamewapeleka kule kwa kazi gani? Chadema wanachokifanya sasa hivi ni kujaribu kuutibua uchaguzi ama usifanyike au hata ukifanyika ufanyike kwa mizengwe waje kutoa sababu ya kwamba uchaguzi haukuwa wa haki na kuiingiza nchi katika machafuko. Na hii yote inatokana na chadema kukata tamaa kuhusu suala la kushinda uchaguzi kwa hivyo katika kuonyesha kuwa chadema hawaitakii mema nchi wameamua kuweka mikakati ya tukose sote. Jengine hizo za kwenda UN na kwengiko wanakokujua wao ni ushauri wa Maalim Seif pamoja mafisadi wenzake wasioitakia mema Tanzania na Zanzibar kwa ujumla. Seifu alizunguka dunia zima kuwaangukia wahisani wasitoe misaada kwa Zanzibar na wanzibari. Na kwa kipindi chote cha ufitini wa seif juu ya Zanzibar katika jumua za kimataifa wananchi wanyonge wanzanzibar ndio waliokuwa wakiteseka . Chadema wanachokifanya sasa ni kuishiwa na kubwa kwao watakalojisifia ni kuichafua na kuipaka matope Tanzania na kikwete kwa sababu za kipumbavu kabisa kama wao kweli wanachungu wa sheria na demokrasia kwanini walipo tafuta mgombea wao wa uraisi hawakutumia njia za kidemokrasia kwanini hawakuwapa wagombea wao wengine kutathminiwa uwezo wao wakampitsha mgombea wao kidikteta ? Utaona hapa chadema na ukawa hawakwenda UN kutaka haki ya kulinda kura bali wamekwenda UN kuichafua na kuipaka matope Tanzania, Shame on them. Hawa watu hawana nia njema na taifa watanzania wafahamu hivyo.
Sallenn Marlon, nakuunga mkono yote uliyosema ni kweli. Hawa Chadema wameshaona matokeo yao yakuwa mabaya sana.
Mdau- Boston USA
Mfa maji haishi kutapatapa. Chadema tayari wameshaona maji yamekuwa marefu na hivyo wanajaribu kila aina ya uovu ili wavuruge shughuli za uchaguzi. Jambo hili la kitoto na lisilo na msingi halitawapeleka kokote. Siku zao zimefika na chama chenyewe kitafutika katika orodha ya vyama hivi karibuni.
Siyo mara ya kwanza Chadema kukimbilia Umoja wa Mataifa. Hapo nyuma wameshafanya hivyo pia. Yote haya yaliishia katika kudhalilisha chama hicho na pia harakati za kujenga msingi imara wa kidemokrasia nchini.
Post a Comment