ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 22, 2015

DK. JOHN MAGUFULI AOMBA KURA KUPITIA SIMU

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimezidi kujitengenezea mazingira mazuri ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka unaotarajiwa kufanyika Jumapili, Oktoba 25 baada ya kubuni mkakati mpya
wa ushindi ambapo mgombea wa nafasi ya urais Dk. John Magufuli kuwapigia simu wananchi akiomba wampigie kura. Ujumbe huo unaokwenda kwa watumiaji wa simu za mitandao mbalimbali humfikia mmiliki wa simu kupitia namba +255622333333 na mara baada ya simu hiyo kupokelewa husikika sauti ya Dk. Magufuli akiwaomba watanzania kumpigia kura ili aweze kushinda na hatimaye aweze kuwa rais. 
 Hatua hiyo ni moja ya njia muhimu za kuwafikia watanzania wote bila kujali itikadi zao na zaidi wale baadhi ya wananchi waliokosa fursa ya kusikia mambo yapi yatafanywa na mgombea huyo endapo kama atafanikiwa kuwa rais. Ukiacha utaratibu wa kampeni za moja kwa moja majukwaani, mabango, mahojiano katika televisheni, hatua ya Chama cha Mapinduzi kubuni njia ya kutuma ujumbe huo kwa wananchi utawasaidia kujiongezea kura katika uchaguzi huo unaonekana kuwa na ushindani mkubwa. 

 Pengine hili ndio bao la mkono lililowahi kusemwa kipindi cha nyuma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Nape Nnauye kutokana na hatua hiyo kuwa muhimu hususani wakati huu ambao watanzania wengi wanamiliki simu za mkononi. Kutokana na hatua hiyo ina maana kuwa watanzania wengi wataweza kumsikia mgombea huyo akiwaomba kura mbali na maeneo mengine waliyozoea kusikia sauti yake ikiomba kumchagua katika uchaguzi huo unalenga kumpata rais wa awamu ya tano wa taifa hili. Chama cha Mapinduzi CCM kimemsimamisha Waziri huyo wa Ujenzi kushika kijiti kinachotarajiwa kuachwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete siku chache zijazo.

11 comments:

Anonymous said...

Siiiipendi CCM Kama Hitler

Anonymous said...

Oombe kila kona wetu Lowassa tu

Anonymous said...

Kura anaomba apewe yeye huko Ikulu anaenda na mke yupi au huyu Mgombea mwenza ndio wamempa kama mke. WaTanzania watakuwa wapum.. kama walivyokwishaambiwa kwa hilo. Ikulu inahitajika kuwa na first lady anayejulikana na tangu kuanza hadi kumalizika hakfuna anayemjua sisi kina mama tutakuwa wapi hapo baadae!! Jiulize na uamue sahihi.

Anonymous said...

Itabidi kuanzia leo muanze kufikiria mtakuwa wapi baada ya kura kutolewa na Dk. John Pombe Magufuli kutangazwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anonymous said...

Huipendi CCM kama hitler ? CCM inakupenda na ndio maana wao CCM waliwawekea wazee wako mazingira mazuri ya kukutengeza wewe la sivyo usingekuwepo hivi sasa .

Anonymous said...

Anonymous@2:32PM yaelekea hujaelimika kwani CCM is a political party and Hitler alikuwa kiongozi na siyo chama. How do the two related? Nawe mdau @4:59PM, sielewi kama ni ushabiki au facts. What makes you think that Lowasa will win? Utafiti umeonyesha kwamba 80% ya umati unaohudhuria mikutano ya Lowasa hawakujiandikisha kupiga kura, and the majority were paid teenagers for photo ops! And that is the deficit Lowasa and Ukawa won't be able to overcome come Sunday October 25, 2015. CCM is on the cutting age of Technology, Ukawa mpo shocked kuona hata nyanya zetu vijijini watapokea ujumbe kutoka kwa Dr. Magufuli kwa cellphones!

Anonymous said...

cheza na teknolojia wewe hapa kazi tu## ukawa wasubiri tuwaalike kuja ktk kumuapisha magufuli.

Anonymous said...

Ulimsikiliza ktk mahojiano na BBC? Tafakari zaidi. .

Anonymous said...

HATA UHANGAIKE VIPI MAGUFULI CHAGUO LA WATANZANIA WALIO WENGI NI EDWARD LOWASSA.SASA HIVI CCM INAMWAGA PESA KAMA VILE INAOKOTWA.WAMEENDELEA KUIKAUSHA HAZINA.ANAPEWA KILA MHITAJI,BENDERA,FULANA NA 20,000.MRADI TUU USEME CCM OYEE.HUU NI UWENDAWAZIMU WA KIASHIRIA CHA KUSHINDWA.TEENA,CCM MTAANGUKA VIBAYA MNO.

Anonymous said...

Tanzania hatuhitaji kiongozi mzungumzaji tunataka kiongozi mtendaji
Wazungumzaji wapo CCM miaka 54 no changes , ilani ile ile sera zile zile
Lowassa it's our choice no way

Anonymous said...

Kama unaichukia CCM hama nchi utafute mahala pengine pa kukaa kwani chama hiki kinachukua ushindi tena tarehe 25/10/2015.