Advertisements

Friday, October 16, 2015

KAMISHENI YA HAKI ZA BINADAMU YA UMOJA WA MATAIFA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akizungumza siku ya Alhamis Usiku, muda mfupi kabla ya kuonyeshwa kwa filamu ya "the Boy from Geita" ambayo inaelezea uovu wanaotendewa watu wenye ulemavu hususani watoto Nchi Tanzania. Katibu Mkuu Msaidizi wa ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Bw. Ivan Simonvic wapili kutoka kushoto alitambua mchango wa serikali katika kuukabili uovu dhidi ya watu wenye ualibino na akahidi Taasisi hiyo na nyingine za Umoja wa Mataifa ushurikiano na Serikali. wa Kwanza ni Bw. Peter Ash mwanzilishi na Mkurugenzi wa Asasi ya Unter the Same Sun na karibu na Balozi ni mwakilishi kutoka Uwakilishi wa Kudumu wa Canada katika Umoja wa Mataifa
Mwandaaji wa mwongozaji wa filamu ya "the Boy from Geita Bw Vic Sarin akizungumza machache kuhusu kwanini aliamua kutengeneza filamu hiyo.
Sehemu nyingine ya waalikwa ambao pia walipata nafasi ya kuuliza maswali baada ya filamu hiyo.
Sehemu wa wageni waalikwa waliofika kuangalia filamu ya "the Boy from Geita" iliyonyeshwa Alhamisi usiku hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
Balozi akiteta jambo na Kijana huyu ( jina halikupatikana) raia wa Marekani mwenye ualibino



Na Mwandishi Maalum, New York


Siku moja baada ya Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kuelezea kwa waandishi wa habari juhudi zinazofanywa na serikali dhidi uovu wanaofanyiwa watu wenye ualibio.Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHR ) imesema itashirikiana na Serikali ya Tanzania katika juhudi hizo za kuukabili ouovu unaofanywa dhidi ya jamii hiyo ya watanzania.

Kauli hiyo imetolewa Alhamisi usiku na Katibu Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu, Bw. Ivan Simonovic muda mfupi kabla ya kuonyeshwa kwa filamu ya “ the Boy from Geita”.

Bw. Ivan Simonovic amesema, ushirikiano huo ni katika kutambua juhudi zinazofanywa na serikali katika siyo tu kwa kuhakikisha tatizo hilo linatoweka lakini pia kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaohusika na ukatili huo.

“Tofauti na nchi nyingine, Serikali ya Tanzania imeonyesha ujasiri na uthubutu wa kukabiliana na uovu unaofanywa dhidi ya watu wenye ualibino. Ni kwa kutambua juhudi hizo tutashirikiana na serikali katika kukomesha uovu huu” akasema Bw. Simonovic.

Kauli ya Bw. Ivan Simonovic ya kutambua juhudi hizo za serikali, kumetokana na shuttle diplomacy iliyofanywa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako Manongi ya kuonana na wakuu wa Idara ambazo zimefadhili kuonyeshwa kwa filamu hiyo hapa Umoja wa Mataifa, pasipo kuushirikisha wala kuujulisha Uwakilishi wa Tanzania.

Aidha maelezo ya awali kuhusu filamu hiyo yanaupotoshaji wa baadhi ya mambo hali iliyomfanya Mwakilishi huyo wa Tanzania katika Umoj wa Mataifa kuchukua fursa ya kuyatolea ufafanuzi.

“Usiku huu ninapenda kutambua juhudi zinazofanywa na Moja ya nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania, ambayo Mwakilishi wake Wakudumu Balozi Tuvako Manongi yupo pamoja nasi. Siyo tu kwamba Tanzania imeonyesha ujasiri na uthubutu wa kutambua ukubwa wa tatizo linalowakumba watu wenye ualibino lakini pia imefanya juhudi za kuwaelimisha wananchi wake huku ikuchukua hatua muhimu” akasema Bw. Ivan Simonovic

Akaeleza zaidi kwamba kama watakavyoona kwenye filamu hiyo. Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda amekuwa msemaji na mtetezi wa haki za watu wenye ualibino kwa kufanya ziara za kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi kuhimiza na kuelimisha wananchi kuachana na ukatili huo

“Kujituma kwake na namna anavyolichukulia tatizo hili kwa uzito wa aina yake, ni ushahidi wa namna gani Tanzania inavyokabiliana na changatomo hii. juhudi hizi zimeleta matokeo chanya ambapo hakuta taarifa za matukio ya kuvamiwa watu wenye ualibino katika miezi ya hivi karibuni.

“ Ofisi ya Haki za Binadamu inakaribisha na kutambua juhudi hizo za serikali ya Tanzania katika kukabiliana na Ubaguzi. Mfumo mzima wa Umoja wa mataifa upo tayari kuwaunga mkono” akasema katibu Mkuu Msaidizi.

Alipopewa nafasi ya kuzumgumza mbele ya hadhara hiyo. Balozi Tuvako Manongi kwanza, alimshukuru Katibu Mkuu Msaidizi kwa kutambua mchango wa serikali, na pia kumpatia fursa ya kuja kuzungumza na kutoa fafanuzi kwa niaba ya serikali yake.

Balozi Manongi, alirejea kauli aliyoitoa mbele ya waandishi siku ya jumatano, kwamba, Tanzania haikatai na wala haipingi kwamba kuna tatizo kwa watu wenye ualibino.

Akasema pamoja na kukiri kuwapo kwa matukio ya uovu dhidi ya watanzania hao, lakini angependa pia kuweka rekodi sawa na hasa kufuatia maelezo ya upotoshaji ambayo yametolewa kwenye vipeperushi vinavyoitangaza filamu hiyo.

Baadhi ya mambo ambayo Balozi ameyatolea ufafanuzi ni lile linaloelezwa na waandaji wa filamu hiyo kuwa eti ualibino ualianzia Tanzania miaka 2000 iliyopita jambo analosema halijathibitishwa kisayansi.

Akafafanua pia kwamba, Watanzania ni waumini wa dini ya kiislamu au wakristo , kwa hiyo kusema kuwa sehemu kubwa ya watanzania wanaamini katika uchawi halina mashiko.

Akasema kwamba si sahihi pia kueleza kwamba wazazi ni washirika katika kutenda maovu dhidi ya watoto wao wenye ualibino. Amefafanua pia kuwa neno zeruzeru ni tafsri ya Kiswahili ya neno alibino na kwamba tafsri inayotolewa na waandaji hao ni upotoshaji.

Balozi Manongi pia amekanusha taarifa zilizoelezwa na waandaji hao kwamba Asasi ya Under the Same Sun, ilipokuja Tanzania mwaka 2007 haikukuta chama chochote cha kuwasema watu wenye ualibino si kweli. Kwani chama cha Tanzania Albinism Society ( TAS) kimekuwapo tangu mwaka 1978 na kimekuwa kikiendesha shuguli zake kwa kushirikiana na serikali.

“ Mashambulizi dhidi ya watu wenye ualibino nchini Tanzania, ni makosa ya jinai, yanayofanywa na watu binafsi ambao wamejawa na mawazo uovu ambayo yanaweza tu kuthibitishwa na vyombo yha sheria” akasisitiza Balozi

Na kuongea kwamba Tanzania inaheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria na kwa kuheshimu huko haiwezi kutoa hukumu kiholela bila ya kufuata mkondo wa sheria.

Akifafanua Zaidi kwa takwimu Balozi Manongi amesema watu bilioni moja au Zaidi wenye aina mbalimbali za ulemavu, asilimia 80 wanatoka nchi zinazoendelea. Na kwamba kwa mujibu wa sensa ya watu iliyofanyika nchini, watu 2.6 milioni sawa na asilimia 5.8 ya idadi yote ya watu wana aina moja ama nyingine ya ulemavu. Kati yao 16,477 au 0.04 asilimia wana ualibino.

Wakati wa kipindi cha majibu na maswali baadhi ya watizamaji walihoji sababu ya waandaji wa filamu hiyo kuionyesha Marekani ili hali kwamba katika Marekani yenyewe pia kuna vitendo vya ubaguzi wa hali ya juu yakiwamo matukio ya watu kuuwa.

Wengine walitaka kujua ni watu gani wanaonunua viungo vya watu wenye ualibino swali lililojibiwa na waandaji wa filamu hiyo kuwa ni ni matajiri wakiwamo wanasiasa kiuhalifu. Wakasema pia kwamba ni watanzania wachache ambao bado wanaimani potofu dhidi ya watu wenye ualibino, huku wakibainisha uhuru wa vyombo vya habari nchi Tanzania imechangia kwa kiasi kikubwa kufahamika kwa madhila wanayofanyiwa watu wenye ualibino.

No comments: