Waendesha baiskeli kutoka Malawi wakiwasili kwenye mpaka wa Tanzania na nchi
hiyo tayari kwa kukabidhi kijiti cha kampeni hiyo kwa wenzao wa
Tanzania.
Mmoja wa waendesha baiskeli Tanzania ambaye pia ni Ofisa Miradi wa Norwegian Church Aid, Tanzania, Gilbert Mworia.
Meneja
Miradi
wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina Mosha akizungumza jambo
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya
tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli.
Waendesha baiskeli wa Tanzania wakiwa katika mji wa Kyela Mbeya
Mama Mosha akiwa na baadhi ya waendesha baiskeli wa Tanzania
Balozi
wa kampeni ya We Have Faith nchini Malawi, Father George Buleya
(kushoto) akiwa na Mratibu wa Vijana kutoka YouthCAN Tanzania, Francisca
Damian wakati wa hafla ya kukabidhiana kampeni hiyo iliyofanyika kwenye
mji wa Kasumulu, Mbeya.
Na Dotto Kahindi
Kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi
kupitia uendeshaji wa baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika imeingia
Tanzania Octoba 17 kwa waendesha baiskeli 21 kutoka Tanzania kuwapokea wenzao
kutoka Malawi.
Kampeni hiyo ambayo imeanzia Msumbiji, Afrika Kusini, Botswana,
Zimbabwe, Zambia, Malawi na hatimaye Tanzania na itatia nanga Kenya mapema
mwezi novemba mwaka huu.
Msafara huo wa waendesha baiskeli kwa Tanzania umeanzia
kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu ambapo unataratia kwenda mpaka
Namanga watakapoukabidhi kwa waendesha baiskeli wa Kenya.
Kwa mujibu wa Meneja Miradi wa shirika la Norwegian Church
Aid, Augustina Mosha lengo la msafara huo ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya
mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia vijana kutoka kwenye taasisi za kidini
nchini.
Anasema msafara huo utahusisha pia uchukuaji wa saini za
wananchi ili kuweka imani zao kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye
mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika Desemba
mwaka huu huko Paris, Ufaransa.
Mama Mosha anasema kuwa wameamua kutumia uendeshaji wa
baiskeli kama njia ya kuhamasisha jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa
sababu chombo hicho ni rafiki wa mazingira na hakichangii uzalishaji wa hewa
ukaa.
Picha zote na tabianchi blog
No comments:
Post a Comment