ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 22, 2015

LOWASSA ALITIKISA JIJI LA TANGA KWA MARA NYINGINE TENA

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja wa Indian Ocean, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni,  Oktoba 21, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa akiwahutubia wananchi wa jiji la Tanga waliofurika katika viwanja wa Indian Ocean, katika Mkutano wa Kampeni,  Oktoba 21, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa jiji la Tanga waliofurika katika viwanja wa Indian Ocean, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, Oktoba 21, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, Mussa Bakar Mbarouk, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye viwanja vya Indian Ocean, Jijini Tanga, Oktoba 21, 2015.  

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwanandi kwa wananchi, Wagombea wa nafasi ya Udiwani, Jijini Tanga leo.















7 comments:

Anonymous said...

Sijui kama hao aliowatikisa walipata wasaa wa kumsikiliza mgombea huyo katika mahojiano yake na BBC swahili...

Anonymous said...

Hata kama watakuwa wamemskiliza sijui kama watakuwa wamemuelewa au kuyatilia maanani yale aliyokuwa anaeleza maanake mengi haya na msingi !!!!!!!!!!!

Anonymous said...

samahani bbc ni nini,ni kuku au ni mbuzi,sijakuelewa,lowassa keshafanya mikutano ya hadhara ya wananchi tanzania nzima zaidi ya 1500.bbc? nakuuliza tena ni nini? jee ni mayai ya kukaanga?huna hoja ni vema ukakaa kimya.lowassa ndiye rais wetu mtarajiwa.

Anonymous said...

Koma wewe Kwani BBC ni kigezo cha uraisi
We need president without No bla bla from central comitee CCM
Rais anayefanya maamuzi magumu siyo kina kinannna , makamba, mnauye wakandaji wa serikali ya CCM
Hivi CCM hamna vikao kujadiriana rais kaziba maskio mawaziri wengi shemeji zake Kama Hawa Bin Ghasia mtoto mdogo Na shungi lake kisa mdongo wake Salma

Anonymous said...

Anaeongelewa hapa ni Lowasa.kinana,Kikwete ,Ghasia hawako kwenye ballot.

Anonymous said...

Mahojiano ya BBC swahili ndio yaliyotoa nafasi ya nadra kwa watanzania kutathmini uwezo wa Lowasa.Kwani wakati wote Ukawa wamekuwa wakitafuta kila mbinu kufichua udhaifu wake kwa kumpa 5 minutes ya kuongea.
Only with Ukawa,Uraisi agombe lowasa hotuba za kampeni atoe Sumaye!

Anonymous said...

Kwa kuwakaribisha majeruhi na wakimbizi kutoka CCM, Ukawa wameruka tope wakakanyaga ...., pole zao sana. Kama wataendelea kuwa chama tukutane tena uchaguzi ujao. Kwa wakati huu ni CCM tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!