ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 19, 2015

LOWASSA AUNGURUMA TUNDUMA NA KYELA, KAMPENI ZA UKAWA KUSITISHWA

Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Vyama vya Ukawa, Edward Lowassa, akihutubia mkutano wa kampeni huko Tunduma mkoani Mbeya leo Oktoba 19, 2015. 
Kampeni za UKAWA, zitasimama kwa muda Oktoba 20, ili kutoa fursa kwa viongozi kushiriki ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa UKAWA, marehemu Dkt. Emmanuel Makaidi, itakayofuatiwa na mzishi yake yatakayofanyika Sinza jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Fidelis Feix na Othman Michuzi)
Mh. Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka(kulia) katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma katika mjini wa Tunduma mkoani Mbeya leo Oktoba 19, 2015.
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru, akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Mgombea urai wa Chadema anayeungwa mkono na Vyama vya Ukawa, Edward Lowassa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma katika mjini wa Tunduma mkoani Mbeya
Mh Lowassa akihutubia Kyela
Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Vyama vya Ukawa, Edward Lowassa, akiwasili kwenye mkutano wa kampeni huko wilayani Kyela leo Oktoba 19, 2015

2 comments:

Anonymous said...

Watanzania wenzangu amkeni - hawa viongozi wote wanaojitia UKAWA washaiba na bado wanataka kuzidi kuiba. Naomba mjiulize huyo mgombea Urais kupita Chadema kwanini anunue njia ya kuingia Ikulu. Chagueni viongozi na sio watawala. Baba wa Taifa alisema mjihadhari na viongozi wanaotumia hela kuingia Ikulu - hizo pesa wamezipata wapi na kama wamekopa jee watazirudishaje. Amkeni Watanzania wenzangu. Jee akiingia Ikulu atafanya nini? Na livyokuwa CCM alifanya nini na jee CCM isingemtema angekuwa wapi? Mungu Ibariki Tanzania na Wabariki Watu wake.
Mwenyezi Mungu tujaalia uchaguzi wa AMANI - Amina.
P.S. Tafadhalini msikilizeni Hayati Baba wa Taifa - RIP

https://www.youtube.com/watch?v=6TuNQOm4NFc&feature=youtu.be

https://www.youtube.com/watch?v=fvkWbhmYYxU

Anonymous said...

CCM itashinda.