ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 28, 2015

Lowassa: Hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi NEC

12 comments:

Anonymous said...

Ukawa hamuwezi kukataa matokeo kwa sababu hayakukamilisha matakwa yenu. Wananchi tumepiga kura na kuamua nani ni muadilifu, mchapa kazi, na asiye na dosari ambaye atatutoa kwenye umaskini wetu. People have spoken, and please, respect their will. Mnataka kusema Watanzania tumewaonea kwa kutompa Lowasa kura zetu?

Anonymous said...

Wananchi hamuamui chochote, ccm na nec yake ndiyo inayoamua. Na hapa tutailaumu ccm kwa kuiletea na kuingiza Tanzania katika vurugu na aibu kutokana uroho wa madaraka.

Anonymous said...


Mabadiliko ya kweli yatatoka ndani ya CCM. Lowassa na timu yako mneondoka ndani ya CCM, wananchi wamefanya mabadiliko ya Viongozi ndani ya CCM. Sasa mabadilko yatatokea serikalini na uongozi mpya. Wananchi wamemkubali Dr. Magufli kama president wa awamu ya tano kufuata utaratibu wa katiba 1977.

Anonymous said...

You made the wrong choice!

Anonymous said...

Sumaye usijidanganye na kudanganya watu kuwa nchi itaingia kwenye matatizo. Atakaye ingia kwenye matatizo ni wewe na watu wako. Nina ni aliwaambia kuwa ushindi ni kwaajili ya upinzania tuu?? Mimi si mwana CCM lakini nikiangalia mtririko wa matokeo inaonyesha wazi kwamba UKAWA iling'anga'nia mijini kumbuka watanzania wengi wako vijijini kazi amabayo Maguguli aliifanya vizuri sana ya kukutana na wananchi uso kwa uso kila mahali. Siasa ni sayansi. Mlidanganywa na mafurriko ya mijini ambayo yalikuwa ya kijaa wapinzani na wasio wapinzani. Pole Lowassa, Sumye, Kingunge nk. Imekula kwenu. Next time mjifunze kutokurupuka. Upinzani ni muhimu kwa nchi lakini upinzani wenu ni wa uchu wakutawala. Mngewaachia wapinzani halisi wakaendelea na juhudi zao. Sumaye, Lowassa, your time is over. Kapumzikeni kwa amani msitafute matatizo uzeeni. Msiwadanganye hawo vijana wa bodaboda, watasota magereza nyie mukipulizwa na air condition kwenye used Land Cruisers.

Anonymous said...

duuuh hata kusoma walichomwandikia kinamshinda sasa ndio angekuwa rais huyu, poor papa el

Unknown said...

We nyamaza haki ikiendeka kotekote hamna kwenye tatizo. Cz wanaiba mpaka wanajidahau sis wananchi hatuna tatizo. Ila uwazi kwenye kuhesabu ndo inaleta shida
Kuna mpole a see

Anonymous said...

Tulitoa maoni na tutaendelea kuchangia maoni hapa vijambo na hongera sana kwa kuwa pamoja katika kipindi chote cha uchaguzi. Mchango wangu wa maoni ya leo ni kuhusu ukawa. Lowasa ni mroho wa madaraka tena hata kuhakikisha damu za watu zinamwagika lakini yeye anaingia ikulu. Mungu bariki Tanzania ni nchi yenye vyombo vya usalama vya uhakika na visivyotawaliwa na utabaka wa aina yeyote ile la sivyo tungekuwa tunazungumza mwengine sasa hivi . Ukawa na propaganda zao dhidi ya CCM sawa sawa na kelele za fisi mbugani zidi ya simba dume. Tulikuwa tunazumza hapa jinsi magufuli alivyotumia uchapa kazi wake kujitafutia ushindi nchi zima. Ushindi wa magufuli ni ushindi wa wawananchi. Mtu yeyote anaetafuta kazi hata ya kuosha dishi au hata kazi yenye kuhitaji elimu zaidi licha ya viambatananizo vya kuthibitisha kama wewe umesoma lakini cha msingi zaidi ni jinsi utavyojielezea katika maombi yako ya kazi lowasa kashindwa kabisa kujielezea mbele ya watanzania wamarekani wanasema you don't ask it you don't get it. Sasa leo lowasa nini kinachomtia wazimu kukataa matekeo ni kitu yeye alifikiri ile mihemko ya maandamano ndio kura? Licha ya tume kuchelewesha matokeo baadae nimekuja kuwafahamu kwanini walifanya vile, ni bora njia walioitumia ya kutoa matekeo taratibu kuonesha kwa uhakika kila mgombea kavuna nini kutoka kila jimbo kwa kweli ni matokeo yanayotolewa kwa uwazi zaidi . Na inaimani kama tume isingetoa matokeo kwa staili ya sasa yaani wangetoa matokeo ya pamoja bila ya kuonyesha wapi yanatoka basi kungekuwepo na malalamiko na vurugu zaidi. Hongera tume kwa kazi kubwa na hongera watanzania wanaopenda amani. Karibu magufuli.

Anonymous said...

We ulomchagua Rais wako basi maliza utaratibu, kuna nini tena?
Ujinga wa ulowachagua ndo umetufikisha hapa tulipo. Haya sasa utatafuta ubuyu wa ku...

Anonymous said...

Masikitiko ni kwamba Ukawa hawataki kujielimisha. Badala ya kupiga kelele, wangekaa chini kujiuliza what went wrong in their campaign, so that corrective actions could be taken to help get different outcomes come October, 2020! Mnasahau hata hii methali yetu ya kiswahili isemayo "Maji yakimwagika hayazoleki"? Wake-up and grow UKAWA folks!

Anonymous said...

Tatizo kubwa la Ukawa ni ile kujifanya wenyewe wamesoma sana na Watanzania wengine wote wajinga! Hata ukisoma wanavyochangia kwenye hizi blogs utaona wanavyomwaga matusi bila kutoa hoja za maana na hata kufikiria kuwa hao wanaowatukana wengine ni ndugu zao hususan Watanzania wenzao. Lakini hili halinishangazi maanake hata kwenye kampeni hawakuwa na sera ya kuwaeleza wananchi ndiyo maana wananchi wakawastukia. Waswahili walishasema "asiye sikia la mkuu, huvunjika guu". Kama mwenendo wao utaendelea kuwa hivi nina uhakika kabisa hivi karibuni tutashuhudia kutoweka kwa Chadema na Ukawa yao kitu ambacho kitakuwa siyo kizuri kwani tunahitaji upinzani kuendelea ili kudumisha demokrasia yetu.

Huyo aliyeandika kuwa CCM inaiingiza nchi kwenye vurugu na kuiletea aibu shauri ya uroho wa madaraka sijui haya mawazo anatoa wapi! Wasimamizi wa uchanguzi wa ndani na nje ya nchi wametoa maoni yao na kuelezea kuwa uchaguzi ulikuwa shwari asili mia 96 wakati wakupiga kura hadi kuhesabu. Pamoja na kuwa awali kulikuwa na vurugu za hapa na pale ambazo zilihusisha Ukawa pia Ukawa hawa hawa wamehusika na vurugu tena baada ya matokeo kuanza kutolewa. Wote tunajua ni nani waliohusika na kufunga mabarabara na kuchoma matairi ya magari huko Mbeya. Pia tunajua ni nani waliochoma moto ofisi za CCM. Pamoja na haya yote tunajua pia jinsi Ukawa walivyoingiza nchini bila vibali mamuruki wao wanaowaita wataalam wa IT ambao ndiyo walianza kughushi matokeo bahati nzuri usalama wa taifa ulivyo makini ukagundua njama zao kabla hawajafanya madhara na sasa watu wao hao wako ndani wanangojea wavune walichopanda.

Poleni sana Ukawa. Hata hivyo mjue tu kuwa jahazi limeshaondoka bandarini na hali rudi numa. Hata hivyo Tunawashukuru Watanzania wengi wanaopenda na wanoitakia nchi yetu amani kwa kukataa kata kata kurughubiwa na njama za kibinafsi za waioitakia mema nchi yetu. Tunawashukuru pia viongozi wa vyama 6 vya upinzani walio saini karatasi kukubali matokeo ya uchaguzi na kuashiria kuwa yalikuwa ni ya kweli kama NEC ilivyotangaza. Kwa hawa viongozi kukubali ukweli ulivyo inaonyesha kuwa wamekomaa kidemokrasia na ni washindani wa kweli siyo wale wasio kubali kushindwa hata kama ni dhahiri. Pongezi nyingi zaidi zimwendee mgombea kwa tiketi ya ACT ambaye baada ya matokeo kutolewa alichukua simu yake na kumpigia Dk Magufuli na kumpongeza kwa ushindi wake huo halali. Huku ndiyo nakuita kukomaa na viongozi wetu wote wanatkiwa kuiga mfano wake. Panapokuwa na mashindano ni lazima wote tukubal kuwa ni mmoja tu ndiyo atakayekuwa mshinda na wanaoshindwa badala ya kulalamika wanatakiwa wampongeze aliyeshinda. Waswahili walisema “asiye kubali kushindwa si mshindani”. Kwa kukataa kushindwa hata pale matokeo ni dhahiri Ukawa wameonyesha kweli kuwa wao siyo washindani. Na yote haya yandhihirisha jinsi viongozi wao walivyo na uchu na uroho wa madaraka na kuweka maslahi yao mbele zaidi kuliko maslahi ya Watanzania na nchi yetu kwa ujumla. Viongozi hawa pia wameshindwa kuelewa kuwa wananchi waliamua kumchagua mgombea mwingine mgombea huyo alionyesha kuwa na sifa nyingi walizo amini ndiyo zinatakiwa kwa kiongozi kuiendesha nchi kitu ambacho hawakukiona kwa viongozi wa Ukawa.

Anonymous said...

Eti humo ndani ya UKAWA namo kuna professors. Najiuliza, hivi hao wachumia tumbo walipataje huo u-professor? Kama u-professor wenyewe ndiyo huo, basi bora kuishia form four, kwa sababu tayari utakuwa na uwezo kama huo ambao professors waliomo ndani ya UKAWA wameuonesha!