ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 27, 2015

LOWASSA: TUME YA UCHAGUZI INAMPE-NDELEA DK. MAGUFULI


Brighton Masallu

MGOMBEA wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Ngoyai Lowassa, amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeonesha dalili za kumpendelea mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli katika matokeo ya nafasi ya urais.


Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Ngoyai Lowassa.
Lowassa aliyasema hayo mkoani Arusha jana, alipolazimika kuita vyombo vya habari na kuonesha wasiwasi wake dhidi ya tume, muda mfupi baada ya kutangazwa matokeo ya awali, asubuhi.

Katika malalamiko hayo, Lowassa aliishutumu tume kwa kutangaza matokeo hayo, kwa kile alichokiita ‘kutowaandaa wananchi kisaikolojia’.Lowassa alililaumu jeshi la polisi kwa kitendo cha kuwakamata baadhi ya vijana katika maeneo ya Kinondoni na Mwananyamala jijini Dar na kuwaweka selo.

“Tume wanatangaza matokeo kwa kuonesha dalili ya kuipendelea CCM na mgombea wake, Magufuli kwani bila kuwaandaa wananchi kisaikoloji, hatashinda.“Pili, nimesikitishwa sana na kitendo cha polisi kuwakamata vijana kiholela, pale Kinondoni na Mwananyamala,” alisema Lowassa.

MAGUFULI ALIVYOKIMBIZA

Katika majimbo ambayo Nec ilitangaza na kuonesha wazi ushindi wa Dk. Magufuli dhidi ya Lowassa ni kama ifuatavyo;


Dk. John Pombe Magufuli.

Jimbo la Nsimbo mkoani Katavi, Dk. Magufuli alishinda kwa kura 4,229 sawa na asilimia 83.14 huku Lowassa akipata jumla ya kura 6,042, sawa na asilimia 9.9.Katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara, Dk. Magufuli aliibuka kidedea kwa kujinyakulia jumla ya kura 33,699, sawa na asilimia 62.34 huku Lowassa akiambulia kura 19,017, sawa na asilimia 35.18.

Huko Kaskazini Unguja kwenye Jimbo la Donge, Dk. Magufuli alipata kura 5,592 ikiwa ni asilimia 83.39 na Lowassa akajikusanyia 1,019 sawa na asilimia 15.2.Katika Jimbo la Kiwengwa, Nec ilitangaza kuwa Dk. Magufuli alipata jumla ya kura 3,317 ikiwa ni sawa na asilimia 73.30 huku Lowassa akiambulia kura 1,104, sawa na asilimia 24.40.

Katika Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, Dk. Magufuli aliibuka kidedea kwa kura 35,310, sawa na asilimia 80.25 ambapo Lowassa alipata kura 7,928, sawa na silimia 18.01.Kwenye Jimbo la Kibaha Mjini mkoani Pwani, Dk. Magufuli alipata jumla ya kura 34,604, sawa na asilimia 57.15, huku Lowassa akipata kura 25,448, sawa na asilimia 42.05.

Katika majimbo yote matatu yaliyotangazwa na Nec awali, asubuhi katika Jimbo la Makunduchi, Dk. Magufuli alipata kura 8,606 na Lowassa akapata 1769.

Kwenye Jimbo la Lulindi, Dk. Magufuli alipata kura 31,602 huku Lowassa akiambulia 11,545 na katika Jimbo la Paje visiwani Zanzibar, Dk. Magufuli alipata kura 6,035 dhidi ya Lowassa aliyeapata kura 1,899.

15 comments:

Anicetus said...

Hapa ni namba tu. Watanzania wemesema kwa uhuru wao na heshima yao kwa viongizi wanaowataka.

Unknown said...

Hiyo tume mna wawakilishi wa ukawa na hata hayo matokeo yanakotoka yamehakikiwa na wawakilishi wote wa vyama vyote vya siasa kabla ya kuwasilishwa NEC. Kwa hivyo Lowasa kusema tume inampendelea magufuli ni moja kati kasumba za viongozi wa kiafrika ya kutokukubali ukweli kila inapotokezea kushindwa uchaguzi vile vile matamshi kama hayo ni hatari kutolewa na moja ya kiongozi kama lowasa hasa katika wakati kama huu. Jambo moja tuwe wa kweli kuhusu tume kuchelewesha matokeo ni aibu ni kama vile walikuwa hawajajiandaa . Kila unapochelewesha matokeo ya uchaguzi ndipo unapokaribisha matatizo kwani binadamu anakikomo cha kuhimili presure. Tumezowea hapa Marekani siku hiyo hiyo ya uchaguzi matokeo siku hiyo hiyo kwa kwetu angalau ingechukua siku tatu tungewaelewa ile tume haifai wawatafute watu wengine baada ya uchaguzi huu.

Anonymous said...

Mheshimiwa Lowassa anakosea. NEC haimpendelei Dr. Magufuli, wao kazi yao ni kutoa Matokeo. Nadhani waliompendelea Dr. Magufuli ni WANANCHI WALIOPIGA KURA. Hivyo Lowassa awalaumu wapiga kura waliomkataa, simple and clear.

Anonymous said...

This look very fishy man put democracy first Tanzania.

James Bond said...

Acheni unafiki hakuna asiyefahamu hapa NEC imeteuliwa na Kikwete bila ya parliamentary approval..hat a waangalizi wameona kasoro nyie milo hapa US mna ushahidi gani wa kutetea tume? Tunafahamu nyie ni CCM lakini Kama mnaishi hapa lakini hamuoni kasoro za mfumo mzima wa uchaguzi Tanzania muwanafiki wa kutupa...

Anonymous said...

Ananymous of October 27, 2015 at 4:35 PM

Democracy in this regard refers to giving people the opportunity to elect a candidate of their choice and this is exactly what they were given and used it effectively. If Lowassa did not get the votes he wanted he has nobody else to blame but to blame himself. He had all the time to entice voters to vote for him during the campaigns but he spent much of his time showing off with his helicopters and spending little time on the campaign stages. Sorry but this is the reality and he now he has to "reap what he sowed".

Anonymous said...

Wewe james bond kama unaishi hapa Marekani basi hapakufai bora urudi bongo. Bush na Algore uchaguzi wa utata inasemekana Algore alishinda nani anajua lakini maamuzi ya tume ni Bush ndie alieshinda sasa uliwahi kumsikia Algore kuitisha maandamano? Ukaja uchaguzi mwengine kati ya john Kerry na Bush vile vile utata mkubwa ukaibuka lakini maamuzi ya tume yakaamuru Bush mshindi wamerekani wakaheshimu maamuzi ya tume. Sasa leo ukawa baada ya kukosa cha kukosoa kutoka kwa wasimamizi wa ndani na wa nje wanaitengenezea mizengwe tume ya uchaguzi. Waafrika ni waafrica kwa kweli serikali ya Tanzania ilijitahidi sana kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru na wa haki lakini ni wao wapizani ndio walioanza na mchezo mchafu si shangai baadhi ya nchi za kiafrika zinaamua kuwa za kidikteta kwa upumbavu kama huu wakina mbowe.

Anonymous said...

Walikuwa wanadanganyika na wing wa watu kwenye kampen. Walisahau wengine wahuni tu. Na ukizingatia baadhi ya maeneo ata kumuona hawajamuona. Vipi leo aipe lawama NEC !!? wakati wananchi ndo wamechagua !!!

Anonymous said...

Wananchi ndo wamechagua vipi itupiwe lawama NEC !!! Hujui kama baadhi ya maeneo ata kukuona hawajakuona.

Anonymous said...

Kuwa mwana-CCM na kuishi hapa Marekani au nchi nyingine yoyote nje ya nchi yetu siyo kuwa mnafiki. Kuna sababu nyingi zinazomfanya mtu akae nje ya nchi yake na bado akabaki na mapenzi, siyo ya nchi yake tu, bali na chama chochote cha siasa anachokipenda ikiwa pia CCM, na bado mtu asiwe mnafiki. Kitu kinachoongelewa hapa ni mzozo wa viongozi wanaotaka kutuletea balaa kwa kutoa kila aina ya uongo pale NEC inapotangaza matokeo ya kura zilizopigwa na wananchi.

Lazima tujue kuwa NEC haisimamii uchaguzi na kuhesabu kura zinavyopigwa huko vituoni. Kazi ya NEC ni kupokea na kutangaza matokeo kama yalivyotoka huko vituoni. Hivyo NEC inapopokea kura kutoka vituoni kazi yake ni kutangaza matokeo ya kura hizo jinsi ilivyoyapokea na kwa kufuata utaribu wa kituo gani kimepeleka mwanzo. Kwa kufanya hivyo sioni ukweli wa hoja ya Ukawa kudai kuwa NEC inampendelea mgombea wa CCM kwa kutangaza kwanza matokeo ya kura anazoshinda yeye. Kama matokeo hayo yaliyopelekwa NEC yametoka sehemu ambayo wapiga kura wengi wamemchagua Magufuli wana Ukawa walitaka NEC ifanye nini? Isubiri mpaka na yale yanayoonyesha Lowassa kashinda ndiyo atangaze? Ikumbukwe oia kuwa vyama vyote viliiomba NEC kuto matokeo haraka kama inavyoyapokea. Sasa kwa kutanga mara apokeapo bila kujali matokeo yanamweleo ya ushindi wa mgombea yupi anafanya makosa? Ama kweli ni vigumu kumridhisha binadamu. Waswahili walisema “tenda wema wende zako, usingoje shukurani”.

Pili matokeo hayo yanayotolewa vituoni kuna na wawakilishi wa kila chama na pia wasimamizi wa uchaguzi ambao wanaangalia taratibu zote zikifuatwa ikiwa ni pamoja na mahesabu ya kura zilopigwa. Kabla ya matokeo ya kura hayajawasilishwa ofisi za NEC wawakilishi wa vyama vyote wanaweka sahihi zao kwenye hayo makaratasi kujiridhisha na kuhakikisha kuwa idadi ya kura iliyoandikwa hapo ni sahihi. Sasa kama Ukawa wana idadi tofauti na iliyoko NEC idadi yao hiyo wameitoa wapi? Je wawakilishi wao wanawapelekea idadi tofauti na zile walizosaini na kupelekwa ofisi za NEC? Kama ndivyo hivyo nani mnafiki hapa?

Anonymous said...

democracy in what regard,hivi kweli wewe umeenda shule au mzamiaji muhuni tuu.unashindwa kwenda ndani kiini cha malalamiko.wananchi wamejitokeza tena kwa wingi sana,wamepiga kura zao,zoezi limekwisha,kura zimehesabiwa,mawakala wamesaini,matokeo yamebandikwa.simama hapo,jee tuko pamoja?hesabu za matokeo zimepelekwa jimboni.mpaka hapo sawasawa.sasa msimamizi wa jimbo anapeleka matokeo TUME MAKAO MAKUU.KAZI YA TUME MAKAO MAKUU NI KUWEKA TAARIFA HIZI ZA MATOKEO KWENYE MFUMO WA KUTANGAZIKA KWA MLOLONGO MZURI.KINACHOFANYIKA,WIZI MKUBWA UNAANZIA HAPO.MAAFISA WA TUME UPANDE WA INFORMATION TECHNOLOGY[IT] WAKIONGOZWA NA MKURUGENZI WA TUME BW.KAILIMA WAKISHIRIKIANA NA CCM-IT WIZARDS[KAMA VIONGOZI WA CCM WANAVYOJIGAMBA NAO] CHINI YA JANUARY MAKAMBA,WANAANZA KU,RE-EDIT TAARIFA HIZI ZA MAJIMBO,WANAFANYA MAJOR MANIPULATIONS BILA KUJALI UWIANO[WAPIGA KURA WANAZIDI AU WANAPUNGUA SANA,KURA ZA WAGOMBEA URAIS ZINAZIDI ASILIMIA 100,NA MADUDU MENGINEYO KIBAO].BAADA YA HAPO KAILIMA ANAMKABIDHI MWENYEKITI WAKE ATANGAZE,I MEAN ASOME.MZEE LUBUVA SI MWIZI HATA KIDOGO,NI VERY DISSENT LAKINI BILA KUGUNDUA AU KUJIJUA ANAKUA OUTWITTED NA KAILIMA NA ILE TIMU YA WAHALIFU WAKUU WA CCM,WAKIOMGOZWA NA JANUARY MAKAMBA.HIVI NINAVYOANDIKA HESABU ZOOOTE ZA MATOKEO YA UCHAGUZI HUU TAYARI WANAZO CCM.KINACHOENDELEA SASA NI UHUNI TUU,ZUGA,ULAGHAI,CHANGA LA MACHO.ILA TUNASEMA MUNGU YUPO UPANDEWA WANAOONEWA NA KUKANDAMIZWA.TUNANYANYASIKA,TUNAKAMATWA.TUNAFUNGULIWA MASHTAKA YA UONGO TUPU.NI CCM HIYO.WEWE FEDHULI UNASEMA,WE ARE REAPING WHAT WE SOWED,STUPID IN ITS LIMIT HEIGHTS.

Anonymous said...

You're a lunatic SOB in urgent need of a psychiatrist! Do you know that there are so many places (especially urban areas, Arusha, Kilimanjaro and Pemba) where Lowasa outperformed Magufuli by big margins and the announced results show that? You cannot force victory for your corrupt and unwanted candidate!

Anonymous said...

Wewe huna lolote unalotuambia hapa. Vituoni wanakopigia na kuhesabu kura kuna maajenti wa vyama vyote na ambao wana hakiki na kusaini makaratasi yenye idadi ya kura kabla hayapelekwa kwenye ofisi za Tume. Zikifikishwa ofisi ya Tume pia kuna maajenti wa vyama vyote ambao nao wanapitia na kuridhia hayo makaratasi waliyoyapokea toka vituoni ili kujiridhisha kuwa idadi ya kura zilizopigwa ziko sawa. Baada ya kuridhika sehemu zote hizi mbili ndiyo Mwenyekiti wa Tume anatoa matangazo sasa hayo makelele yenu yanatoka wapi?

Tunajua tatizo lenu kubwa ni ubishi, kulalamika kusikoisha na matusi tu lakini hiyo haitawasaidia kwani wananchi walishaamua na Dk. Magufuli anatangazwa kesho kuwa mshindi. Sasa wewe na kisomo chako, sijui una PhD ngapi, hata hivyo uliee tu na sisi wajinga tufurahie. Pamoja na hayo yote "you still will reap what you sowed" upende, usipende.

Anonymous said...

sasa nimeelewa.tatizo halipo kwenye majimbo.wasimamizi wa majimbo wanawakilisha vizuri hesabu zao nec-makao makuu.pale mkurugenzi wa tume ramadhani kailima ndipo anapoanzia kufanya usaliti wa ukweli.kwamba matokeo yale ana share na watu wa information technowledge wa chama cha mapinduzi na kazi ya kuupindua ukweli inaanzia hapo,simple and clear.ni uhalifu mkubwa sana na mbaya kweli-kweli.taarifa sahihi za majimbo zinapinduliwa.kwa watu wenye uelewa finyu na elimu ndogo na pia waliobahatika kusoma lakini wakabaki bado wapuuzi utaalamu huu wa kihalifu wa mitandao umewapita kushoto,hawauelewi wala huwezi ukawaelimisha,ni wajinga wa maisha.hawa ni pamoja na anonymous 10.42pm,3.17am,4.07am na 'baba lao'11.46 am.hili hatulionei ajabu watanzania tuliopo nyumbani tanzania,kwa sababu tunayaelewa mengi kuhusu baadhi yenu mnaojiita 'tanzania diaspora mlipo nchini marekani, kwamba mlipelekwa na watu au taasisi zipi na mnafaidika vipi kwa mfumo huu wa ukandamizaji wa chama-dola ccm.mbona ni rahisi tuu,tunawaoneni,mnajitangaza kwa maana nyingine mnajilengesha.

Anonymous said...

Ananymous wa October 29, 2015 at 12:28 AM

Mwenzetu umesoma sana mpaka akili zimekuruka. Pole sana. Kwa akili yako timamu utatuambia pia kuwa hata hizo sahihi za maajenti wenu zinazoonekana kwenye makaratasi yaliyo pelekwa NEC amezisaini au amezigushi Ramadhani Kailima. Kwa akili zako pia utatuambia hata hao viongozi wa vyama 6 vya upinzani waliokubaliana na hesabu zilizopelekwa NEC na kukubali matokeo kuwa ni sahihi kwa kadri wajuavyo wamefanya hivyo kwa ajili ya ufinyu wao wa kuelewa watendalo. Ama kweli Waswahili walisema "akili nyingi huondoa maarifa". Kama kuwa na akili nyingi maanake ni ndiyo hivyo afadhali ni baki na ungumbaru wangu.