ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 12, 2015

MCHANGO WANGU WA MAWAZO KWA WA TANZANIA WAKATI HUU WA UCHAGUZI WA 2015.

Kwa viongozi wa ngazi zote, kwa wanasiasa, waumini au washilika wa madhehebu mbali mbali, wafanyakazi wa ngazi zote,wakulima,wafanyavyashala,wanafunzi,watu wa lika zote,wagombea viti mbali mbali n.k. Ndugu na lafiki zangu wa Tanzania, mimi naitwa CHARLES M.KAROLI wa Canada.Kama mtu ambaye niliwahi kuishi Tanzania kama mkimbizi zaidi ya myaka 15 na kukaa katika kambi tofauti mikoani ya Kigoma na Kagera na kutembea ktk mikoa mbali mbali pamoja na kujifunza mambo mengi kwa wa Tanzania ndugu na rafiki zangu hata kuzidi rafiki zangu wa nchi yangu ya kuzaliwa,nimetumia muda wangu huu kwa kuomba serikali na magazeti yote kupitisha ujumbe wangu kwenye magazeti yote kama rafiki wa Tanzania na wa Tanzania.

Tangu mlipoanza kujiaanda na uchaguzi wa mwaka huu 2015 hadi sasa ni lazima kila wakati niangalie shughuli za uchaguzi zinaendaje katika mikoa na sehemu mbali mbali.Kwanza nawatakia uchaguzi mzuri na wa amani.Tanzania inajulikana kama nchi ya amani na ni ukweli,pia ni nchi ya makimbilio kwa wale ambao hawana amani.

Kipindi hiki cha uchaguzi,nikifuatilia kampeni za wagombea tofauti na wafuasi wa vyama mbali mbali ingawa ni wachache,baadhi yao naona kama wanaotaka KUBIPU MACHAFUKO,VULUGU,UGOMVI,UZUSHI n k... katika nchi ya amani kama Tanzania,watakuwa wanataka UKIMBIZI UWAPIGIE NA SIJUI WATAKIMBILIA WAPI!Nashukulu uongozi wa wilaya ya Kasulu jinsi juzi juzi walivyoita watu wa mikoa jirani kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani humo,kwa kujionea wenyewe hali ya wakimbizi,ili waende kuwaeleza wananchi wao kuepukana na shughuli zozote za uvunjaji wa amani wakati huu wa uchaguzi.

Lengo langu ni kuwashauli wa Tanzania kudumisha amani kila mmoja katika sehemu yake alipo,anapofanyia kazi,anaposafiri,anapojinadi,anaposikiliza sela za mgombea,anaposhabikia,yeyote akumbuke kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea na utaendelea kuwa Mtanzania pamoja na kushi pamoja na yule mliokuwa mnatukana au mnagombana wakati wa uchaguzi.

Mjifunze na yaliotokea katika nchi jilani zenu na yanayotokea kwa sasa.Mimi mwenyewe nikiwa mkimbizi hapo Tanzania,nilizunguka katika kambi kumi tofauti,hii ikifungwa nahamishiwa nyingine na kuanza maisha upya.Katika mzunguko huwo kuna mabaya na mazuri,ndiyo maana nawashauli kutolewa amani mlionayo na anayetaka kulewa amani ya Tanzania ajiulize,ajifunze kwa mifano nilioyitoa.Yule ambaye ni mgumu kuelewa atembelee kambi za wakimbizi wanaokimbia kwa sasa ajionee jinsi anavyojitabilia.

Nimalizie kwa kuwaomba wale wote wanaozungumza majukwani kwenye kampeni,kwenye radio,kwenye midahalo,kwenye shuguli zozote zinazohusu uchaguzi wa hivi karibuni,kujiepusha na maneno ya kuwashawishi wananchi kugomea viongozi wao wa selikali na kutotii amri yoyote ya uongozi.

Baadhi ya wananchi wanaingizwa kwenye shida na wanasiasa bila kujua,baadhi yao unakuta ni vijana wa vijiweni ambao hawajafikisha umri wa kuchaguwa.Wanasiasa,fanyeni kampeni za kuunganisha wa Tanzania,wakuu wa madhebu mbali mbali,wiki hizi za kuelekea uchaguzi, na baadhi ya viongozi wa dini walianza kufanya hivyo,fundisha waumini wenu jinsi ya kuheshimiana kama watu wanaomjua Mungu,kila mpigakura achaguwe yule ambaye ana uhakika naye wa kumvusha mahali anapotaka kufika.

Kwa yule ambaye anapingana na ushauli wangu huu,atakuja kusema yake,wote wanaofuata shuguli za uchaguzi Tanzania kupitia mitandao tofauti watakuja kunisaidia kumjibu.UCHAGUZI MWEMA 25/10/2015 Mungu ibaliki Tanzania,Mungu ibaliki Afrika.Asante. WENU MPENDWA. CHARLES M.KAROLI CANADA.Mnisamehe kwa mandishi yangu mabaya ya lugha ya kiswahili.

No comments: