ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 2, 2015

MOTO WA MWIGULU NCHEMBA WATUA MAJIMBO 5 YA MOROGORO,HAKIKA MORO NI NGOME YA CCM

 
Mamia ya Wananchi wa Kata ya Dumila Jimbo la Kilosa wakisikiliza sera za Mwigulu Nchemba alipokuwa akiinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi hii leo."Wananchi wa Dumila,Mchagueni Mbunge huyu wa CCM,Ni Mchapa kazi na ameshaanza kufanya kazi za maendeleo hata bila kuwa Mbuge,Hakikisheni anashinda kwa kishindo iliakaungane na timu ya kazi ya Magufuli"Mwigulu akizungumza Dumila.Mwigulu Nchemba akiondoka viwanja vya Mkutano Kata ya Dumila.Mwigulu Nchemba akiwasili kata ya Kilombero Jimbo la Mikumi hii leo.Mwigulu akiwahutubia Wananchi wa Kilombero hii leo,Kubwa amewaomba waendelee kuwa na Imani na Chama cha Mapinduzi hasa Mgombea Urais Ndg.J.Pombe Magufuli,Ilani ya CCM inatambua changamoto za Wananchi wa kilombero ambao asilimia kubwa ni wakulima wa Miwa na mnategemea kipato chenu kutokana na Kiwanda cha SUkari cha Kilombero,Uongozi Ujao wa magufuli unakwenda kufanya kazi ya kuhakikisha Wanakilombero wanafaidika na kiwanda hiki."Mwigulu.Mbunge Mtarajiwa wa Jimbo la Mikumi Bw. NKya akizungumza na Wananchi wake wa kata ya Kilombero,Amesisitiza kusimamia hazi za wakulima wa miwa na Uboreshaji wa miundombinu ya Barabara.Wananchi wa Kilombero wakionesha ishara ya Umoja ni Ushindi kwa Chama cha Mapinduzi.Mwigulu kwa wanakilombero "Mandeleo ya kweli yanaletwa na Chama cha Mapinduzi,Hakikisheni mafiga matatu yanapatikana(Rais,Mbunge na Madiwani wa Chama cha Mapinduzi),Umoja huu ni kiungo kizuri kwenye ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo.Mwigulu Nchemba ambaye ni Mjumbe ya timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Ifakara Ndg.Abubakar Assenga."Nawaombeni tufanye Uchaguzi wa Amani,Kila Chama kiheshimu uwepo wa Chama kingine"Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Ifakara Mjini hii leo.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Ifakara Mjini."Wanaifakara mmeshawekewa Ujenzi wa barabara ya Rami kutoka Kilombero hadi hapa kwenye Ilani ya CCM,Nawaomba mchagueni Magufuli ambaye hata hapa Ifakara amefika wakati wa Kufungua Kivuko ,Na sasa anakuja kufungua Ujenzi wa barabara hii ilikufungua shughuli za Kiuchumi kwa huu mji".Sehemu ya Maelfu ya Wananchi wa Ifakara wakisikiliza hoja za Mwigulu Nchemba akiwaambia wamchague Magufuli kwakua ni Mchapakazi,Muadilifu na Mfuatiliaji.Comrade Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Gairo ndg,Shabiby mapema hii leo alipokwenda kumuombea kura za Urais,Ubunge na Udiwani.Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Mrimba Ndg.Kunambi akiwaeleza Wananchi wa Mrimba kuwa anasifa za kutosha kuwa muwakilishi wao kwenye Bunge la Jamhuri,Hivyo anawaomba wamchague kwa kura nyingi iliabadilishe taswira ya maeendeleo kwa Jimbo la Mrimba.Wananchi wa Mrimba wakisema "Hapa Kazi tu"Mwigulu Nchemba akimnadi Bw.Kunambi mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Mrimba.Wananchi wa kata ya Mashariki mwa Jimbo la Ifakara wakifuatilia Mkutano wa hadhara wa kampeni wa Mwigulu Nchemba hii leo.Mwigulu Nchemba akiwasihi Wananchi wa Jimbo la Ifakara kumchagua Assenga Abubakar kuwa Mbunge wao kwakua anamjua namna alivyomfuatiliaji wa shughuli za maendeleo hata akiwa ndani ya Chama pale UVCCM Makao Makuu.
Picha na Sanga Festo Jr.

No comments: