Monday, October 26, 2015

Polisi wavamia kituo cha kukusanya matokeo Ukawa

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama
By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Polisi jijini hapa jana usiku walivamia kituo cha kukusanya matokeo ya nchi nzima cha Chadema kilichopo Kijitonyama na kuwakamata watu wote wanaokiendesha.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene (pichani) alisema tukio hilo lilitokea saa nne usiku wakati vijana hao wakiendelea kukusanya matokeo hayo.

Alisema kituo hicho kilichokuwa kikiendeshwa na vijana 800 na wengine maelfu waliokuwa mikoani wakituma matokeo, kilianza kazi hiyo jana asubuhi kikilenga kukusanya matokeo yote, kuyajumlisha na kujua mshindi kabla ya matokeo ya jumla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Kituo chetu kinafanya kazi ile ile kama inayofanywa na kituo cha CCM kilichopo maeneo ya Mlimani City, tunashangaa polisi kuwakamata watu wetu,” alisema Makene.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema kwa sasa polisi wanafanya operesheni nyingi na watu mbalimbali wanakamatwa, hivyo asingeweza kujua kama watu hao pia wamekamatwa katika operesheni hiyo.

3 comments:

Anonymous said...

Kuruhusu vyama kuwa na hizi tallying centres ndio kukaribisha vurugu.NEC wanapaswa kuvifunga vyote ccm/ ukawa.
Mfano mzuri angalia kinachoendelea sasa hivi huko Zanzibar, ya ni bila mamlaka yoyote kisheria Seif Sharifu amejitangaza mshindi.Huu ni uvunjifu wa sheria na kukatisha uvunjifu wa amani.

Anonymous said...

Come on ccm pressure tayari,bao la macho hilo tulisema,change you can't take it

Anonymous said...

Ukawa wanaelezea vipi uwapo wa mamluki wakikenya na wazungu katika hicho kitengo chao cha IT? Kila uhuni una mwisho wake..