Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa
mgodi mara baada ya kuwasili eneo la mgodi wa urani katika mradi wa mto
mkuju wilaya ya namtumbo mkoa wa ruvuma Oktoba 21,2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua mgodi wa urani mkoani Ruvuma jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelekezo mara baada ya kuzindua mgodi wa urani mkoani Ruvuma jana.
5 comments:
Hongera Baba Tanzania ni tajiri yenye rasimali za kumwaga ila tunahitaji viongozi waadilifu na makini wa kuzisamamia ujio wa Dk Magufuli inaonyesha namna gani mungu anavyoiwekea Tanzania mazingira mazuri ya kupiga hatua ya kimaendeleo . Mwenyezimungu ni mwenye kupenda amani na humuongezea nguvu mtu yeyote mwenye kuhubiri na kudumisha amani hapa duniani na vilevile humzoofisha na kumtia katika mithani mikubwa yule yeyote asieitaka amani hata mtu huyo anamali au utajiri wa aina gani basi kwa kutochagua kutokuishi kwa amani utajiri wake hautakua na maana yoyote. Ile misemo ya kipumbavu ya kusema kama amani na ipotee tumechoka kuishi kwa umasikini huo ni ujinga kwani matekeo ya maneno kama hayo baada ya amani kupotea ni mawili la kwanza upotevu wa maisha ya watu na mali zao. La pili ni kuongeza hali ya umasikini kwani kama kulikuwa na vyanzo vya mtu kujinasua na umasikini vyanzo hivyo vitakuwa vimetoweka baada ya amani kupotea kwa hivyo ni matumaini yetu watanzania mabadiliko ya maendeleo yaendane na amani hata kama kuwadhibiti wachache wenye nia ya kuleta vurugu na kuunusuru umma uishi kwa amani . Suala la kulinda amani kwa watanzania sio suala la kumuonea mtu sitarajii kuona nchi yangu tunaletewa vikosi vya usalama vya kulinda amani tukifika hapo basi tumekwisha ingawaje dhahiri kuna dalili zote wapo watu wanataka taifa kilipelekea katika hali hiyo tumuombeni mungu atuepushie na hali hiyo Amen
Hivi faida ya urani nini? Kwa nini wageni wanakuja kuchimba na kuvuna urani wetu' kama vile wanavyofanya kwa chuma na makaa ya mawe yetu; na malighafi nyinginezo?
Kwa nini tusiongezee faida chuma yetu na kuuza vyuma na vyuma vya pua?
Kwa nini tusitumie urani wetu kuzalisha au kufua umeme bila kutegemea hali ya hewa kuwa nzuru mvua inyeshe ili mabwawa yetu yajae - teknolojia ya enzi za mapinduzi ya viwandani karne hizo huko Uingereza.
Mdau wa @4:29 PM, ebu tuelimishane kidogo. Urani (uranium) kama madini nyingine tulizonazo vinahitaji utaalamu (Technical know-how) ambao we lag behind. Investors wenye know-how ndo solution kwa sasa, as long as Taifa linachukua asilimia ya mapato. Nothing is wrong with investments from foreign countries. Wachina wanazo investments Ulaya na Marekani, and that doesn't mean nchi hizo hazitaki au hazina uwezo wa kujiendesha wenyewe.
UCHIMBAJI WA MADINI YA URANI NI WA HATARI SANA.UNAWEZA KULETA ATHARI KUBWA MNO YA VIFO NA KUNYAUKA KWA WATU NA MAZINGIRA.KWA UJUMLA NI KAMA KULIFUKUA BOMU.MIMI SIWAAMINI HATA KIDOGO HAWA WAWEKEZAJI.NAAMINI HII NI DEAL KANJANJA.MCHAKATO UMEHARAKISHWA MNO KWA MASLAHI BINAFSI.KUNA WATU HUMO WANA COMMISION ZAO NZURI SANA BILA KUJALI USALAMA WA UCHIMBAJI,TECHNOLOGY NA KAMPUNI AU SHIRIKA HUSIKA.NASIKIA KABLA YA KAZI KUANZA ILE KAMPUNI ILIYOSHINDA TENDA [ISIYO NA UWEZO WALA RASLIMALI] ILIKWISHA UZWA KWA MWEKEZAJI AMBAYE CREDIBILITY ZAKE ZINATIA SHAKA.JAMBO HILI TULIKEMEE KABLA YA MAAFA. LIANZISHWE UPYA KUJADIRIWA KWA UNDANI KWENYE BUNGE LETU JIPYA LITAKALOINGIA MJENGONI NOVEMBA 2015.KWA TAMAA,TUSIIKARIBISHE HATARI NA MAAFA, WALIMWENGU WATATUCHEKA.NCHI YA MA-DEAL.EPA BADO,ESCROW BADO,SASA URANI-HATARI!
Anonymous wa October 23, at 2:48 AM - Mbona ufisadi na Richmond hukutaja?
Post a Comment