ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 16, 2015

SHINE WITH SHINA ANNUAL GALA GREENBELT, MARYLAND

 Wahusika wa Shine with SHINA wakihakiki majina ya wageni waliohudhuria Annual Gala iliyofanyika katika hoteli ya Hilton iliyopo Greenbelt, jimbo la Maryland nchini Marekani. Mada ilikua ni ya kuzungumuzia changamoto za wageni wanazo kutananazo kwenye nyanja mbalimbali hususani utamaduni na malezi ya watoto na hasa unapokua muAfrica wa kutoka Afrika unayezungumuza kiingereza cha kiafrika. Changamoto za watoto wanaozaliwa na wazazi wanaotokea Afrika, changamoto zilizoelezewa kwa ufasaha na watoto wa wazazi kutoka Afrika waliozaliwa Marekani. Waielezea pamoja na kwamba wamezaliwa Marekani lakini wanapokua shule hukosa amani kutokana na tamaduni tofauti wanapokua nyumbani kwa wazazi wao hutumia na kulelewa na tamaduni za wazazi wao na wanapokua shule hutumia tamaduni za kimarekani na wasipozifuata watoto wenzao huwaita majina mbalimbali. Waliongezea kwa kusema wanakua na wakati mgumu lakini kitu muhimu ni kujua malengo yako yaliyokupeleka shule.
Bango la SHINA kama linavyojieleza.

 Mshereheshaji Tuma.
Mmiliki wa SHINA Jessica Mushala akiongea jambo.

Kiongozi aliyewakilisha wazazi Dr. Secelela Malecela akichangia mada.

Bi. Heriett Shangarai akiongelea changamoto za jumuiya za kiafrika inazokutana nazo.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi



No comments: