Advertisements

Sunday, October 11, 2015

STARS UNITED YAFUNGWA 6-1 NA DURHAM ALL STARS

 Manahodha wakipata picha na makocha.
 Timu ya Durham All Stars
 Timu ya Stars United
Picha ya timu zote mbili baada ya mechi

Timu ya Stars United inayoundwa na wachezaji mchanganyiko kutoka majimbo tofauti nchini Marekani ambao pia ndio mabigwa wa kombe la Afrika Mashariki, siku ya Jumamosi Octoba 10, 2015 ilipata kichapo cha goli 6-1 kutoka kwa timu inayoundwa na wachezaji mchanganyiko wa Durham, Durham All Stars katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa South Durham uliopo Durham, NC.


Katika kipindi cha kwanza Stars  United ilikianza kwa kasi na halimanusla ijipatie bao la kuongoza lakini mchezaji Seif Ndossa alipiga mpira nje akiwa amebaki yeye na mlinda mlango baada ya kosakosa hiyo mpira ulibadilika Durham All Stars walianza kutandaza soka ya uhakika na kuwazidi Stars United kwenye kiungo. Ukilinganisha mechi mbili za Stars United zilizopita mechi iliyochezwa Atlanta na mechi za kuwania kombe la Afrika Mashari, Stars walishindwa kipindi cha kwanza kutawala mpira na kuruhusu mashambulizi kutokana na kiungo wake kupoteana uwanjani na kusababisha mabeki kupiga mipira mirefu mbele badala ya kupitishia kwenye kiungo na kuweza kuruhusu magoli 3 katika kipindi hicho cha kwanza.

Tofauti na mechi hizo ambayo Stars United ilicheza mpira mkubwa sana lakini siku ya jana ilicheza mpira wa kiwango cha chini na kufanya timu hiyo kupoteana hasa  kipindi cha kwanza

Kipa wa Stars United Mwana Njenje ndiye aliyekua nyota wa mchezo licha ya kufungwa goli hizo kwani umahiri wake wa kuokoa mipira ya hatari kutoka kwa fowadi wa Durham All Stars ambayo iliundwa na vijana wadogo wenye kasi ya ajabu walioikimbiza beki ya Stars United kwa kutumia pasi ndefu zilizoiletea usumbufu kwa walinzi hao.

Kipindi cha pili Stars ilianza kuelewana kwenye kiungo baada ya kufanya mabadiliko na kuwezesha kupata goli la kufutia machozi, lakini baada ya goli hilo Durham All Stars ilianza kukimbiza tena beki ya Stars United kwa mipira mirefu iliyotumiwa na fowadi hiyo ipasavyo kwani wachezaji wake walitumia mwanya wa kukimbizana na na mabeki hao uchezaji walioutumia kipindi cha kwanza. Sifa kubwa iwaendee mabeki Dulla na Liga uimara wakisaidiana na wachezaji wengine wa Stars United uliwezesha kuipunguza kasi Durham All Stars.

Wachezaji wa Stars waliowakilisha timu hiyo kwenye mechi hiyo walikua ni Simon, Inno, Geofrey, Mundo, Seif, Owen, Dulla, Mohammed, Dennis Geofrey, Denese Mabs, Ben Kessy, Feisal, Kelvin, Mude, Ibrahim, Liganga, Baloteli

No comments: