CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu
masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa
Watanzania.
Kufunga Kampeni
CCM
itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo. Kampeni za CCM
zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano.
Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na
wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi watakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:
1. Mwanza
– Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli,
Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
2. Tanga –
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
3. Mbeya –
Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
4. Mtwara –
Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5. Kigoma – Ndugu
Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6. Kilimanjaro –
Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7. Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa
Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu
Kati
ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa
sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya
vituo vya televisheni vitano na vituo vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria
katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo
Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt.
Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanja vyote hivi
saba.
Namna
hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya
CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika
maeneo mbalimbali nchini. Lakini pia tutaweka historia katika tasnia ya
utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja
matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa
upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za
Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23
Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika
majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao
kwa namna mahsusi.
Tathmini ya Kampeni
Kama
Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya
changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa,
na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. Wamekuwa barabarani kwa siku 57
wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku.
Imani yetu ya ushindi
inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa
washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kubwa
ya kampeni waliyoifanya.
Kutokana na kazi kubwa na nzuri
iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani,
CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69.
Uchaguzi wa Amani
CCM
haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama chama
kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya
uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi,
washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
Kauli
za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya
vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura wabaki vituoni
kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
Kwa
utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura zake ni
kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga kura na wenye
nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, kuanzia kupiga kura,
kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo.
Kura zinapigwa na kuhesabiwa vituoni
mbele ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Mawakala wa vyama na Waangalizi wa Uchaguzi wa
ndani na nje ya nchi. Mawakala wa vyama na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaweka
sahihi kwenye fomu za matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa
kwenye kituo.
Kwenye kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa
vyama pia huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za
vituo vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila
kituo.
Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au
kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote
zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha fujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu
wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama
vizuie hili jambo kwa sababu halina nia njema.
Mkakati
wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya
mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza
kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na
usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi
na baada ya uchaguzi.
CCM
haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwa sababu tu
ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
Siku
ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku
kabla ya Uchaguzi, siku ya Uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga
simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya
kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa Uchaguzi.
Kupokea Matokeo
CCM
imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia Mawakala wake moja kwa moja
vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na matokeo ya Uchaguzi
nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya Uchaguzi, tarehe 25 Oktoba
2015.
Imetolewa na:
January
Makamba
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI
22 OKTOBA 2015
15 comments:
Ni mchezonwa kuigiza na vichekesho kwani watu kuangalia luninga ni jambo la kawaida kama mpira wa miguu wa Ulaya. Maamuzi yanabakia yaleyale!!
CCM ndiyo italeta uvunjifu wa Amani Tanzania kwa kukwapua kura za watu. Hii ni dhahiri kabisaa.
Fungeni fungeni
Hata Akhera Watanzania hutuwataki hadi kiyama
Wetu Lowassa
Asante kwa taarifa msemaji mkuu wa ccm january makamba kuhusu utaratibu wa ccm kufunga kampeni zake za uchaguzi mkuu 2015.siku hiyo ya kufunga ndipo mtakapogundua kifedha kwamba ccm "imeifilisi hazina ya taifa "The Treasury".watalipia kwa siku nzima coverage ya vituo vitano vya televisheni,[wastani million 36 kwa kituo,wakitumia million 180].pia wataajiri siku hiyo,Radio 67 wastani ule ule wa million 36 kwa kituo yaani jumla 36x67= million 241,200,000 ukijumlisha 180,000,000 Za Tv unapata matumizi ya televisheni na redio peke yake kuwa MILLION 421,200,000/=. acha usafiri wa ndege na magari,hoteli,posho inaweza kufika Billion 2 kwa hesabu ya chini. Wanatafuta nini ccm katika hili? 1.ubabe wa pesa 2.kujifufua 3.kuwashawishi wapiga kura 4.kuwaaga watanzania kwamba sasa wanaondoka 5.kuwahadaa watanzania 6.kuwapiga changa la macho wapiga kura 7.kujionyesha kwamba hawajiamini hata kidogo 8.kuwatambia watanzania kwamba wao ndiye akina "fedha chafu" 9.kumtishia"nyau" mheshimiwa lowassa na,10.kulewa madaraka ya chama-dola?.wanatafuta nini,wanijibu,watujibu.CCM FANYENI LOLOTE LILE MTAKALOWEZA KUFANYA LAKINI MWISHO WA SIKU SISI WANANCHI TUMEKWISHA AMUA KWAMBA KURA ZETU JUMAPILI TAREHE 25 OCTOBA 2015=TUTAMKABIDHI MHESHIMIWA LOWASSA NCHI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MWINUE MPENDWA WETU MHESHIMIWA LOWASSA,MWANGAZIE HEKIMA KUU,MOYO WA AMANI NA UJASIRI WA MATUKIO.
KWAHERI CCM,KWA HERI YA KUONANA na wala hatushangai mlivyoamua kuaga kwa kishindo,tena sio dar-es-salaam ila mpo rock-city Mwanza.kwa mara ya kwanza ccm wameshindwa kumalizia kampeni zao katika uwanja maarufu kupita viwanja vyote kisiasa nchini tanzania VIWANJA VYA JANGWANI-dar-es-salaam.Hili ni pigo kubwa sana la siasa za ccm hii ni nambari moja.Maana yake nini,tokea uanze mfumo wa vyama vingi nchini tanzania mnamo mwaka 1995.mara zoote nane[8] yaani 1995[2] 2000[2] 2005[2] na 2010[2]ni na hufunga kampeni zao hapo hapo jangwani, ccm hufungua kampeni zao jangwani na hufunga kampeni zao jangwani.Huu ni ushindi wa kwanza wa kihistoria wa Chadema-ukawa.Kilichotokea mpaka ccm wakaikosa Jaangwani siku ya kulalia uchaguzi mkuu yaani tarehe 24 octoba 2015 Wanakijua vizuri wao wenyewe CCM.POLENI SANA CCM,sasa,waombeni UDP wawakaribishe Benchi la wapinzani.BYE our long time foes in tanzania political arena.
Oops eti Leo kutuambia ukomo WA rais
Why this year and not 2010,what's going on CCM
Watanzania siyo vipofu au wiziwi, tumesikia toka intelligence yetu Ukawa !
Jakaya jakaya acha utani
It's Lowassa Lowassa that's all
Vijimambo – 10/21/2015
Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka CCM kuhusu kufunga kampeni
Mwalimu alisema, "kupanga ni kuchagua". CCM wanapanga mambo yao na wala hawakurupuki kama vyama vingine. CCM kukaa kimya muda mrefu bila kutanganza wapi wanamalizia kampeni zake na sasa kuelezea kuwa watakuwa huko Mwanza watakuwa walipanga kusudi kabisa kufanya hivyo ili kuepukana na vitendo vya wagomvi wanaong'ang'ania viwanja hata pale wenzao walikuwa wamekwisha kikodi. Kufanya hivi kote ni kuonyesha jinsi CCM walivyo waungwana na wastaarabu. Kwa muungwana na mstaarabu yeyote swala la kiwanja gani afanyie au amalizie kampeni zake siyo swala kubwa au lenye utata kwa vile anakubalika mahali kokote na hivyo hata akifanyia kampeni zake chini ya mwembe bado wengi tu watamfuata na kumsikiliza. Pamoja na haya yote, CCM ni chama chenye msingi na mizizi yake nchi nzima kwa hiyo kutofunga kampeni zake katika viwanja vya Jangwani haiimanishi kuwa chama hiki kimepoteza dira au nguvu zake. Ikumbukwe tu kuwa CCM ina wanachama, wapenzi na mashabiki wake nchi nzima na hata huku ughaibuni tuko kibao.
Pamoja na kuwa CCM ni chama cha kisiasa, ikumbukwe pia kuwa CCM inawekeza fedha zake zitakanazo na michango ya wanachama wake katika miradi mbalimbali za kitega uchumi. CCM ina viwanja vyake mikoani, ina miliki majumba pamoja na vitega uchumi vingine vingi. CCM siyo kama vyama vingine ambavyo vina shamiri kwa michango ya wanachama au ruzuku peke yake.
Kwa kutumia luninga na vyombo vingine vipya vya mawasiliano katika kufunga kampeni zake, CCM haifanyi mchezo wa maigizo wala kuchekesha. Ingawa CCM inatumia vyombo hivi mara ya kwanza, kwa vile hapo nyuma aidha hatukuwa navyo au pale vilipokuwepo vilikuwa havijasambaa kiasi cha kufikia uma wa Watanzania wengi, ukweli ni kuwa nchi nyingi duniani zenye vyombo kama hivi vimekuwa vinatumia kwa hiyo Tanzania siyo ya kwanza kufanya hivyo. Na kwa haya yote kufanyika leo nchini kwetu inaonyesha jinsi gani tumesonga mbele kimaendeleo chini ya utawala wa TANU na Afro Shiraz Party na hatimaye CCM pamoja na kuwa Upinzani wanakanusha kuwa hatujapata maendeleo yoyote kwa miaka yote tangia tujitawale. Wenzetu wa upinzani sijui wako Tanzania gani! Ama kweli "shukurani za punda ni mateke"! Hata mtoto mdogo mwenye akili timamu ukimuuliza tofauti ya Tanzania ya leo na ya jana atakuambia jinsi gani kila mwaka nchi yetu imekuwa inabadilika kimaendeleo.
Mwisho kabisa, ushindi wa CCM kwenye uchaguzi huu ni dhahiri na tarehe 25/10/2015 wananchi watatoa hukumu yao. Hapa ni kazi tu na CCM Oyeeeee!!!!!!
Acheni mchecheto na kama chadema na ukawa mnapagawa hata mambo bado hiyo ndio CCM bana. Inaviongozi wake asilia sio mamluki kama akina Sumaye na lowasa. Hata wakisema wanapeleka kiongozi mmoja kila mkoa uwezo huo upo . Kwa hivyo mtaropokwa sana lakini mkubali tu kuwa mume wa mama ndo baba hata kama humpendi na magufuli ndie raisi wa nchi hilo halina shaka.
Poleni sana wanaChadema/ukawa, Technology imekwisha wapiga panga. Chama tawala ndicho kimeleta Technology Tanzania, and now is the time to display how Technology can benefit the country. Mnalia foul kwa sababu ya technological edge CCM has? Huyo lowasa ambaye mmembeba ndiye alikuwa FISADI aliyekula sana pesa enzi zake pale CCM, kwa nini hampigi kelele? Muulizeni pesa ngapi za CCM amekula kabla ya kuja kuwadanganya eti yeye ni msafi? Mnalia nini sasa, hamjui hii ni 21st century, and Technology rules. Siyo kukopi ulaya kama baadhi ya wadau hapo juu wasemavyo isipokuwa katika karne hii, moodern campaigns goes parallel with Technology. Kumbe Chadema/Ukawa mlikuwa mmelala? Too bad, mmechelewa kuamka, but stay tuned for LIVE CCM broadcasts!!!
Ndio shida ya akili za kukariri na kuishi kwa mazoea.Tambua kuwa siasa ni sayansi na inabadilika kutokana na muda & mazingira. Tuongee 26/10/2015
Ni kweli nyie wachache msiojielewa mmeamua hivo. Walio wengi hawawezi kumpa Lowasa ridhaa ya kuongoza nchi hii.Kushindwa kujibu maswali mepesi wakati wa mahijiano ya BBC ni dhahiri huyu mzee hatufai.
ccm wamebanwa na mtu wanaemuita mgonjwa,hawezi kuongea.yaani kundi lote hilo la viongozi kwa mtu mgonjwa?ndio mjue hamkubaliki.
kelele miingi, chadema, ccm, si mnyamaze muone tarehe 25? mara nyingi unayedhani utamshinda, mara zote huwa anakushinda. tuliiiiiiia.
hao ndio mataahira wachache sugu wa ccm waliobaki,hawasikii,hawaambiliki,akina nape,makonda,mwigulu,yusuph mstaafu na mwanae january,bulembo,makongoro,lusinde,warioba,butiku,polepole,yaani waingereza wanasema "a very negligible political pocket resistance" na inabidi iwe hivyo,wee unasemaje unataka wafe kifo cha kunguni?hawa ni watu wazima wamefaidi sana vya ccm ni lazima,lazima wafe nayo.
Ushindi ni CCM na hapa ni kazi tu.
Post a Comment