ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 31, 2015

TAARIFA YA ZADIA KUHUSU KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI ZANZIBAR.

Logo ya Zadia
Jumuiya ya Wazanzibari Waishio Nchini Marekani (ZADIA), imekuwa ikifuatilia kwa karibu na makini zaidi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mchakato wa uchaguzi ulifanyika kwa njia za amani na utulivu. Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.
Ama kwa hakika kitendo hicho hakikuwa cha busara na kinapelekea kurudisha nyuma maendeleao ya demokrasia Zanzibar, na vilevile hakiashirii mustakbali mwema kwa nchi yetu tuipendayo. Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.
Kwa hivyo, ZADIA inatoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, kumalizia mchakato mzima wa kuhesabu kura kwa majimbo yaliyobakia na kutoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi na kumtangaza mshindi ili kuiepusha Zanzibar yetu tuipendayo kuingia katika hali ya mtafaruku na mifarakano isiyokuwa na tija bali kuleta hasara.
ZADIA pia inaungana na jumuiya zote za kimataifa ambazo zimetoa msimamo wao juu ya uchaguzi wa Zanzibar, hasa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ambao ni kiungo madhubuti kati ya Wazanzibari walioko Zanzibar na wenzao wanaoishi nchini Marekani.
Aidha, tunapenda kumkumbusha Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dakta Ali Mohammed Shein kuwa Wazanzibari walimpa amana kubwa ya kuwaongoza, na kwa hivyo ni wajibu wake kuienzi amana hiyo kwa kuchukuwa hatua za kiungwana za kuitoa Zanzibar kwenye mgando huu wa kisiasa. Hali hii iliyopo sasa inaleta wasiwasi miongoni mwa raia na imekua ikiathiri maisha yao ya kila siku, na ikiachwa kuendelea huenda ikaathiri pia mustakbali maisha yao kwa jumla.
ZADIA pia inamtolea wito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake aliyonayo kuhakikisha Zanzibar inatoka kwenye mkwamo huu wa kisiasa na kwamba anaondoka madarakani akiiacha Zanzibar ikiwa katika hali ya amani na utulivu. Kwa kufanya hivyo atauthibitishia ulimwengu kuwa kweli Tanzania ni kisima cha amani.
Na mwisho tunawaomba Wazanzibari, wapenzi wa Zanzibar, na Watanzania wote kwa ujumla popote pale walipo, wajitahidi kufanya mawasiliano na Jumuiya nyengine za Kimataifa ili ziingilie kati suala hili kabla nchi yetu haijaingia kwenye mtafaruku mkubwa wa kisiasa na kijamii na hata kupelekea kuhatarisha amani ya nchi yetu.
Mungu Ibariki, Zanzibar.

3 comments:

Unknown said...

Sawa kabisa ZADIA lakini ingefurahisha zaidi kama mngeanisha kwamba mgombea wa uraisi wa chama cha wananchi CUF, SEIF SHARIFU Alivunja sheria kwa kitendo chake cha kujitangazia ushindi kabla ya mwenye zamana yake kufanya hivyo. Nna imani wengi tunaelewa jinsi gani siasa za Zanzibar zilivyokuwa very fragile kuanzia kabla ya mapinduzi na baada ya mapinduzi kwa watu wasioijua Zanzibar waache waseme watavyosema kwani hawaelewi yakwamba Zanzibar kiasilia katika masuala ya siasa sawa sawa na volcano iliokuwa imepoa lakini bado mbichi na wakati wowote inaweza kuripuka, maalimu seif anaelewa hivyo, mzanzibar yeyote halisi anaelewa hivyo tuombe mungu suala hili litatuliwe kwa njia za salama sio kusukumiza lawama upande mmoja bila ya kusikiliza madai ya upande mwengine na kuyafanyiatathmini.

Anonymous said...

Nawaungeni mkono ZADIA,asante.kilichotokea zanzibar sisi tuliona na kukijua tangu mwanzo.mwelekeo ulionyesha kuwa ushindi wa cuf ulikuwa ni wa dhahiri mno na ndicho kilichotokea.yalipoanza kutangazwa matokeo ya unguja,ccm na vyombo vyake vya habari,radio uhuru, gazeti la uhuru,na zanzibar leo vilianza kwa kumsifia sana mgombea wa ccm ally mohamed shein kwamba anaongoza na kwamba "anamtimulia vumbi maalim seif kwa mbali".tulichokua tunakishangaa matokeo yaliyokua yakitoka pemba ni ya urais wa jamhuri ya muungano na ubunge tuu.wapigaji kura ni wale wale.ccm walivyoona wameshindwa vibaya DR.SHEIN ALIWAITA KIKWETE NA MKAPA visiwani wakakaa na kikwete kutoa amri uchaguzi ule ulioendeshwa kwa amani na utulvu mkubwa UFUTWE.HII NI AMRI YA KIKWETE na ndipo tarehe 28 jecha akatumwa na kikwete kutoa tamko lile.barua ile iliandaliwa ofisini kwa dr.shein.hii ni aibu na fedheha kubwa kwa zanzibar na tanzania kwa ujumla.udikteta wa CCM ambao pia uliandaliwa kwa bara kama ule wizi mkubwa wa kura usingefaulu umewapiga wazanzibari ambaO safari hii wapo macho na makini sana.CCM HAIKO TAYARI KUSHINDWA KIHALALI,HAWAPO TAYARI KUKABIDHI NCHI KWA WASHINDI HALALI WA KITI CHA URAIS,WA VISIWANI NA ULE WA MUUNGANO.SASA TANZANIA TUADHIBIWE TUU NA JUMUIA YA KIMATAIFA.CCM NI MADIKTETA,WEZI NA WAUAJI WA DEMOKRASIA.

Anonymous said...

anonymous 3.61 ni kama taahira wa mawazo.na hii ni kutokana na kuipenda mno ccm.maalim seif amefanya jitihada zote kuomba azungumze na kikwete na shein.hawapokei kabisaaa simu zake.wewe unasema ooo,usikilizwe na upande mwingine,upi huo?msajili wa vyama tanzania jaji francis mutungi na ujumbe wake walikuwepo unguja,wakaonana na maalim seif wakaongea naye kirefu sana.kazi kumuona shein.haonekani,hapatikani.unabisha tumuulize jaji mutungi ili ushibe na ukae kimya.mmeanguka ccm visiwani,mmeanguka hakuna wa kulipindua hili,kabidhini nchi kwa cuf.