ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 16, 2015

TANZIA


Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe pamoja Kapteni William Silaa ambaye ni baba yake Jerry Silaa, wamefariki dunia katika ajali ya helkopta iliyotokea jana jioni kwenye msitu wa Selous.
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.


Jerry Slaa kupitia akaunti yake ya Instagram amesema "Baba yangu Capt.William Silaa akiwa na Mhe.Deo Filikunjombe na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya helicopter 5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa. Taarifa za mwisho ilionekana imeanguka kwenye msitu wa Selous. Hakuna mawasiliano ya simu. Usiku kucha vyombo vyote vya serikali vimeendelea na jitihada za kufika eneo la tukio na jitihada kubwa zaidi zinaendelea asubuhi hii. Nawaomba wote kuwa watulivu kwani jambo hili linahitaji umakini wa hali ya juu na ushirikiano wa taasisi nyingi za wizara tofauti. Tuwaombee wote Mungu awanusuru.
Fuatilia taarifa zetu tutakujuza zaidi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

2 comments:

Anonymous said...

Mjifunze kuandika habari kwa makini huwezi kuandika kichwa cha habari "Tanzia" na kusema wamefariki dunia wakati haawaja thibitika kufa au kuona maiti zao. Ni mapema sana kusema wamekufa". Wanaweza wakapona au ni mahututi.

Anonymous said...

Poleni wafiwa kila mtu yupo safarini siku ikifika ikiwa ajalini au umelala usingizi, kifo hakichagui mahala gani ichukuwe uhai wa mtu, poleni sana.