ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 30, 2015

Ujumbe wa maafisa kutoka Tanzania wamtembelea Mhe. Balozi Victoria Richard Mwakasege, Balozi wa Tanzania nchini Malawi

Ujumbe wa maafisa wanane kutoka Tanzania ulioko nchini Malawi kwa ziara ya kimafunzo umemtembelea Mhe. Victoria R. Mwakasege, Balozi wa Tanzania nchini Malawi, ofisini kwake mjini Lilongwe. Ujumbe huo wenye maafisa kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Ofisi ya Rais –Utumishi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Fedha, Clinton Health Access Initiative (CHAI), na Mpango wa Taifa wa Kuthibiti UKIMWI (National Aids Control Programme - NACP), uko nchini Malawi kujifunza namna ambavyo Serikali ya Malawi inachukua hatua mbalimbali kuboresha huduma za afya katika jamii kwa kutumia wahudumu wa kujitolea (Health Surveillance assistants). Mpango huo unatumika katika nchi mbalimbali zikiwemo Malawi, Tanzania, Ghana, Ethiopia na Rwanda kwa lengo la kuboresha huduma za afya na hatimaye kupunguza vifo vya akina mama na watoto katika jamii.
Mhe. Balozi Victoria R. Mwakasege wa sita kutoka kushoto akiwa na ujumbe wa maafisa kutoka Serikali ya Tanzania walipofika ofisini kwake tarehe 29 Oktoba, 2015 kumtembelea. Kushoto ni Afisa Ubalozi Bw. Wilbroad A. Kayombo
Mhe. Balozi Victoria R. Mwakasege wa sita kutoka kushoto akiwa na ujumbe wa maafisa kutoka Serikali ya Tanzania walipofika ofisini kwake tarehe 29 Oktoba, 2015 kumtembelea. Kushoto ni Afisa Ubalozi Bw. Wilbroad A. Kayombo

No comments: