Hata hivyo, tunapozungumzia masuala ya mahusiano, hakuna kitu cha hatari sana kama mimi au wewe kuwa na urafiki na mtu ambaye unajua yuko ndani ya ndoa au ana mpenzi wake. Ni hatari sana!
Lakini kabla ya kwenda mbali kulizungumzia hilo, nikuulize swali moja. Chukulia wewe umeoa, siku moja mkiwa mmetoka ‘out’, mnakutana na kijana ambaye anamchangamkia sana mkeo na kufikia hatua ya kumkumbatia wakati wakisalimiana.
Baada ya salamu, mkeo anakutambulisha kwa kijana huyo kwamba ni rafiki yake mkubwa na wamejuana miaka mingi iliyopita. Kama wewe ni mume, utachukulia sawa au utakuwa na hisia mbaya?
Najua kila msomaji atakuwa na jibu lake. Kwa wale wanaojifanya wanaishi Kizungu watachukulia poa lakini kwa waswahili walio wengi watamaindi na maswali yatakuwa ni mengi.
Mimi naomba niseme kwamba, tukiachilia mbali hayo masuala ya ‘uzungu’, hakuna kitu cha hatari kama kuwa na urafiki wa kupitiliza na mpenzi wa mtu.Ni sawa urafiki ni urafiki tu lakini Kibongobongo mwanaume kuwa na rafiki wa kike, tena yule wa kuchati na kupigiana simu kila mara, haiwezi kuwa na sura nzuri licha ya kwamba wapo ambao hawavuki mipaka.
Wapo wanaume wanatengeneza urafiki na wake za watu, urafiki ambao hata watu wanaowazunguka wanawafikiria tofauti. Yote hiyo inatokana na ukweli kwamba, wapo watu wanajifanya ni marafiki tu lakini wakiwa mbali na wapenzi wao dhambi ya usaliti inafanyika.
Sasa katika mazingira hayo unawezaje kuwa na amani mkeo kukutambulisha kwa mwanaume tena ‘handsome’ kuwa ni rafiki yake tu? Utajihakikishiaje kuwa ni urafiki tu na hakuna kinachoendelea wakikutana?
Lakini twende mbele na kurudi nyuma kwamba, hivi wewe mke wa mtu unaanzaanzaje kuwa na rafiki wa kiume tena ambaye huenda hana mpenzi? Urafiki huo ni kwa ajali ya nini? Huoni unajijengea mazingira ya mumeo kutokuamini?
Narudia tena kusema kwamba, kuwa na marafiki siyo kitu kibaya lakini uchague rafiki sahihi ambaye hawezi kukuletea matatizo. Ukijua mtu ana mpenzi wake au yuko ndani ya ndoa, hata kama anajiweka karibu yako vipi, wewe mkwepe.
Ukiona mwanaume f’lani mume wa mtu anakuvutia na ungetamani hata awe rafiki yako wa kawaida, pambana na hisia zako. Elewa kuanzisha urafiki na mume/mke wa mtu au hata mpenzi wa mtu ni hatari.Labda ukianzisha urafiki huo uhakikishe na mpenzi wake anakujua vizuri na hana shaka na wewe, kinyume chake mkifanya urafiki wenu kuwa siri ‘mwenye mali’ akijua, hawezi kuchukulia poa.
GPL
No comments:
Post a Comment