Thursday, November 5, 2015

ACT yashindwa kumshawishi Nyari CCM yampitisha

JITIHADA za viongozi wa juu wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa na mkoani Arusha za kumshawishi mfanyabiashara wa madini Arusha, Justini Nyari kugombea kiti cha ubunge Jimbo la Arusha Mjini, zimeshindikana.

Nyari alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba kuwa mgombea ubunge kupitia ACT Wazalendo, lakini mfanyabiashara huyo alitoa sababu nne za kushindwa kuchukua fomu kuwania ubunge Jimbo la Arusha Mjini.

Uchaguzi wa ubunge Jimbo la Arusha Mjini uliahirishwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu baada ya aliyekuwa mgombea ubunge wa ACT Wazalendo, Estomih Mallah kufariki dunia kwa shinikizo la damu.

Uchaguzi mpya utafanyika Desemba 12, mwaka huu. Baada ya kufariki kwa Mallah, ACT Wazalendo kilikuwa kikihaha kila kona ya Jiji la Arusha na nje ya Arusha kusaka mgombea mwenye mvuto na mwenye kupendwa na wakazi wa Arusha ambao wengi wao ni vijana na kura yao ilimwangukia Nyari na kugundua kuwa ni mgombea pekee mwenye mvuto Arusha Mjini.

Habari zilisema kuwa mpaka juzi usiku saa 5:00 na jana mchana, vikao vilikuwa vikifanyika katika hoteli mbalimbali jijini Arusha kati ya Nyari na viongozi wa juu wa ACT Wazalendo na mawasiliano ya simu, lakini mwafaka haukupatikana baada ya Nyari kusema kuwa yeye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi na hatohama.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zilisema kuwa Nyari mbali ya kuahidiwa kutotoa fedha zozote katika kampeni yake pale atakapokubali kugombea, alipinga, akieleza kuwa muda mfupi sana amepewa kwa jambo hilo kwani alipaswa kupewa muda mrefu na kutafakari na rafiki zake na kutoa maamuzi kwani siasa sio suala la kukurupuka.

HABARI LEO

3 comments:

  1. SAWA ACT-WAZALENDO.FUATENI MAONO YA KIONGOZI WENU MKUUZITTO KABWE .DHAMIRA YAKE KAMA CCM-B NI KUICHIMBA UKAWA.MLISIMAMISHA WAGOMBEA UBUNGE 219 NA MMEFAULU KUMPATA MBUNGE MMOJA,218 KAPUNI TENA KAPU BOVU.SASA MNAITAFUTA UKAWA ARUSHA,HIVI ARE YOU SERIOUS?ARUSHA YA UKAWA ARUSHA YA LEMA?FUJO MBALI,NA,UKWELI MBALI.

    ReplyDelete
  2. Hivi vyama vya upinzani vitakuwa vinategemea mamluki mpaka lini? Kushawishi mtu wa chama kingine agombee nafasi ya uongozi, how loyal that individual will be to your party?

    ReplyDelete
  3. Hivi vyama vya upinzani vitakuwa vinategemea mamluki mpaka lini? Kushawishi mtu wa chama kingine agombee nafasi ya uongozi, how loyal that individual will be to your party?

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake