
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa taarifa zinazosambazwa si za kweli na kwamba waliosambaza habari hizo, watachukuliwa hatua za kisheria. Mwambene alisema watu waliosambaza taarifa hizo watakamatwa na kufikishwa mahakamani kama ilivyokuwa kwa Yericko Nyerere.
Alisisitiza kuwa Rais Mkapa yupo hai na kwamba haumwi ugonjwa wowote bali anaendelea na kazi zake. “Taarifa hizi sio za kweli na kama mtu haamini siwezi kumuita hapa aje akanushe, bali muende ofisini kwake mtamkuta,’’ alisema Mwambene.
Alifafanua kuwa siku ambayo mitandao ya kijamii ilidai kuwa Rais Mkapa amekufa, alikuwa Zanzibar kwa ajili ya shughuli za kitaifa. Aliwataka waandishi wa habari kuwa makini katika uandishi wao ili Sheria ya Mtandao ambayo imeanza kuwakumba watumiaji wa mitandao ya kijamii, isiwakute katika makosa hayo.
Aidha, aliwataka waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi katika shughuli ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Magufuli anayeapishwa leo.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake