ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 15, 2015

ALPHONCE MAWAZO WA CHADEMA AUAWA KINYAMA HUKO GEITA

 Alphonce Mawazo enzi za uhai wake
Na K-Vis Media
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo mkoani Geita, Bw. Alphonce Mawazo, ameuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa shoka na watu wasiojulikana mapema leo Jumamosi Novemba 14, 2015.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na polisi zinasema, Mawazo, alivamiwa na kundi la watu wakati akiwa kwenye kampeni za udiwani kwenye eneo moja la vijijini huko mkoani Geita na kuanza kumshambulia kwa mapanga na hata alipokimbizwa hospitalini kwa matibabu, tayari mauti yalikwisha mkuta.
Mawazo atakumbukwa na wana Chadema kutokana na umahiri wake katika ushawishi wa kisiasa ambapo alijijengea heshima kubwa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani hapa nchini.
Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi kadri tutakavyozipokea.

1 comment:

Anonymous said...

Inasikitisha sana huko tunapokwendea sasa ni hatari. Tunaomba haki itendeke na wahusika wote wa kitendo hiki kiovu na cha kishenzi wafikishwe ndani ya mikono ya sheria. Tunategemea hakutatokea ubabaishaji kutoka kwa vyombo vya usalama katika kulitafutia ufumbuzi suala hili. Vile vile tunategemea watanzania kutolitilia siasa hili suala la mauaji kwani waliotenda hili jambo hakika lengo lao ni kuotesha mbegu za chuki miongoni mwa watanzania kwa hivyo tunatakiwa kuwa watulivu na makini. Vile vile mungu atawapa moyo wa subra ndugu jamaa na familiya ya marehemu, Poleni sana.