Ndugu Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, nachukua fursa hii kukupongeza kwa kuchaguliwa
kuliongoza taifa letu la Tanzania kama Rais wa awamu ya tano.
Nianze barua yangu kwa kugusia changamoto ya
ajali nchini. Ajali limekuwa ni tatizo sugu licha ya juhudi mbalimbali
zinazofanywa na wadau mbalimbali kutoka taasisi binafsi na serikali. Ni hivi
karibuni ripoti ya mwenendo wa ajali za barabarani imetolewa na Tanzania ikishika
nafasi ya tano kwa kuwa na matukio mengi ya ajali barani Afrika.
Ajali hizi zimekuwa zikipoteza raslimali
nyingi sana ikiwepo raslimali watu na raslimali mali. Hii ni vita inayohitaji
juhudi za wadau mbalimbali kupambana nayo kama ilivyo mapambano dhidi ya
Ukimwi, Malaria, Rushwa n.k
Barua yangu inalenga kutoa ushuri katika mambo 16 ya fuatayo;
1.
Katika
kuunda wizara zako, napendekeza kuwe na “Wizara ya Ujenzi ya Majiji” hii iwe
maalumu katika kuratibu shughuli zote zinazohusu Masterplan ya Majiji yetu
mbalimbali yaliyopo na yanayochipukia.Hii ijihusishe katika ujenzi wa barabara
za kisasa kwaajiri ya miaka 50 ijayo.
2.
Miji yote
mikubwa ijengwe “Ring roads” ili kupunguza misongamano ya magari isiyo ya
lazima
3.
Taa za
barabarani zibadilishwe kwa kuweka taa zinazohesabu kutoka 10 mpaka 0, ili
dereva aweze kukadiria kama anaweza kuwahi taa pasipo kuleta madhara kama
ilivyosasa.
4.
Maeneo ya
Makazi au maeneo ya watu wengi kama Buguruni, Manzese, Mbezi ya Kimara, Mwenge
na maeneo ya Mashuleni kama ilivyo Makongo na kwingineko kama maeneo haya
yajengwe madaraja “FOOT -BRIDGES” ili watu wavuke maeneo hayo, tofauti na
ilivyosasa watu wanavuka barabara huku mioyo wameshika mkononi.
5.
Kwa faida ya
wengi, nyumba zilizokaribu na miundo mbinu ya barabara watafutiwe mbadala na
kufidiwa kwa haki kulingana na thamani ya eneo lake kwaajiri ya kupisha
barabara zinazofaidisha wengi.
6.
Vivuko
maalumu viwepo kwenye barabara kwaajiri ya kuwapisha walemavu wanapotaka kuvuka
barabara hizo.
7.
Kuwekwe
Kamera barabara za mijini ili kuwawezesha askari wa barabarani wafanye kazi
wakiwa ofisini badala ya kusimama juani kama ilivyosasa.
8.
Kushughulikiwa
swala la rushwa sehemu za mizani, Checkpoints ambapo ulegevu wa usimamazi wa
sheria umesababisha barabara nyingi kuharibika kutokana na magari kuzidisha
mizigo na kuruhusiwa kupita kwa urahisi maeneo hayo.
9.
Serikali na
taasisi zake kufungua milango ili kuweza Kushirikiana kwa ukaribu na wadau wa
Usalama barabarani kama ilivyo “Dereva Makini Tanzania”, “Road Safety
Ambassadors Tanzania (RSA)”, “Amend Tanzania”, Safespeed Foundation n.k
10. Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa watumiaji
wa barabara mpya za mradi wa mwendo kasi kuwa ni nyembamba hususan maeneo ya Kimara,
tunashauri usanifu wa barabara zingine katika miradi kama hii izingatie upana
unaobaki kati ya gari moja na jingine ili kuondoa ajali zinazoweza kuzuilika.
11. Tunakuomba ushughulikie kwa ukaribu sana
tatizo ambalo linaonekana kuwa sugu linalo leta ajali za kuumiza sana, Malori
yenye makontena (Semi-Trailers) kudondokea na kuyafunika magari madogo.
12. Tunaomba pia liangaliwe upya swala la alama
na blocks zinazowekwa kwenye makutano ya barabara na reli ikibidi kuwe na
automatic blocks kuzuia magari treni inaposogea karibia na makutano haya.
13. Tunakuomba uumalize mgogoro sugu uliopo kati
ya madereva, serikali na waajiri kwakuwa tunaoumia ni sisi maskini tunaotegemea
usafiri wa mabasi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
14. Wachungulie kwa ukaribu wauza vipuli vya
mabasi na ubora wa vifaa hivyo kupitia TBS kwa kuwa kuna watu wanapiga deal
kwenye maisha ya watu.
15. Yamulike makampuni ya mabasi na ya bima
kuhakikisha wanakata bima kubwa kwaajiri ya mabasi yao, ili wahanga wa ajali
walipwe stahili zao kama inavyostahili kuliko kama ilivyosasa kampuni ya bima
inapiga deal na mmiliki wa mabasi.
16. Angalia uwezekano pia wakuingiza technolojia
ya Usafiri wa majini kupitia fukwe zetu mbalimbali za Bahari ya Hindi,Ziwa
Nyasa,Victoria,Tanganyika na Rukwa yaani “AMPHIBIOUS BUS TECHNOLOGY” ambayo
italiongezea taifa pesa kupitia Utalii wa majini "Ocean Tourism"
Peter George Nzunda,
Mdau wa Usalama barabarani
+255687 966 638
2 comments:
Safi sana mdau ila kwa kuchangia ni hizo bara bara hujengwa kwa harama kubwa na vile vile baada ya kwisha kujengwa matengenezo ya hapa na pale lazima yatahitajika baadae sasa sina uhakika kama kuna utaritibu wa toll stations kwa ajili ya uchangiaji wa bara bara kwa watumiaji mbali mbali wa magari . Ni njia moja nzuri tu ya kuzifanya bara bara zetu ziwe na uwezo wa kujiendeleza wenyewe, cha kutilia mkazo ni usimamizi imara wa ukasanyaji wa mapato na matumizi yake.
Asante sana mdau Peter Nzunda, barua yako kwa Rais imeelezea tatizo sugu watumiaji wa barabara Wana face kila siku, kweli points zako za kulitatua hili tatizo wengi tunaafikiana na wewe. Tunatumaini Rais wetu atazingatia maoni na ushauri uliotoa na kuwa implement to resolve the problem.
Post a Comment