ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 22, 2015

HABARI KAMILI YA VITANDA VYA MAGUFULI VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 251 ZILIZOKUWA ZITUMIKE KUJIPONGEZA WABUNGE

 Magari ya Bohari ya Dawa (MSD), yakishusha vifaa tiba Taasisi ya Moi kufuatia agizo la Rais Dk.John Magufuli kulitaka Bunge kutumia sh.milioni 15 kwa ajili ya kujipongeza na fedha zilizobaki kuzipeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kukabiliana na uhaba wa vifaa tiba na magodoro. 
Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais Dk. John Magufuli.

Vifaa hivyo vilianza kupelekwa juzi katika Taasisi hiyo ili kukabiliana na uhaba alioubaini Rais  Magufuli baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika mapema mwezi huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akizungumzia kuhusu vifaa hivyo jijini Dar es Salaam juzi wakati wa usambazaji alisema  hivyo vyenye gharama ya sh.milioni .251 ni pamoja na vitanda 300, magodoro 300, viti vya kusukuma (Wheel Chairs) 30, vitanda vya kubebea wagonjwa (Stretchers) 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400.

Alisema MSD ilianza kupeleka Vifaa hivyo MOI mwishoni mwa wiki na kuwa itaendelea kutoa vifaa hadi wiki hii inayoanza leo.

Fedha hizo zilizotumika kununulia vifaa hivyo zilitokana na agizo la Rais Dk.John Magufuli alilolitoa wakati akilihutubia bunge mjini Dodoma mwishoni mwa wiki ambapo alilitaka bunge kutumia sh.milioni 15 tu kwa ajili ya kujipongeza na kiasi hicho kilichobaki kitumike kununulia vifaa hivyo.

8 comments:

Anonymous said...

Asaante mdau pamoja na mheshimiwa Rais kwa kauli tekelezi. Ni jambo la kushangaza kuona hivi vifaa vinatoka katika bohari la madawa (MSD)! ina maana hivi vifaa vyote vilikuwepo lakini kutolewa ilikuwa mbinde? wahusika wakuu katika wizara ya afya walikuwa hawalioni hili? Ina maana tosha kuwa ni maeneo mengi sana ya serikali na utendaji wa kazi kuwa hautekelezeki hadi aje msemaji kama Rais PJM alivyofanya?? Pili inadhihilisha kuwa fedha zipo nyingii kabisa nchini lakini zinaenda kwenye mikono ya wachache! ELIMU BURE inawezekana kabisa kumbe ni mtandao wa mfumo dume unatawala!! Asante Rais John Pombe tunakuombea uweze kuangalia na maeneo mengine ni kazi kubwa sana ila watendaji utakaowaweka wawe waadilifu na wakiwa wanajua kabisa matatizo ya wananchi na uwezo wa utendaji mzuri upo na fedha zipo nyingi tukiwa na maana rasilimali na watu nguvu kazi.
Jingine kubwa ambalo ungeliweza kulifanya ni lile la kuagizwa kwa magari 770 ya Polisi ni sawa hatuna tatizo nalo. Tunakuomba kwa mamlaka uliyo nayo hayo magari kuna ngwe ambayo haijawasili labda na kama tayari, tunakuomba hili ulitizame. Kupunguza idadi hyo kwa kununulia Ambulance na kuzipa idara nyinginezo muhimu sehemu ya magari hayo. Na hata ikiwezekana basi kuwepo na ununuzi wa helikopta hata mbili kwa ajili ya dharura! ni chombo muhimu sana kwa polisi kufika eneo la hatari badala ya barabara ambazo zina msongamano mkubwa.Tunakuombea kila mafanikio tukijua kuwa utapambana na watu sugu na wasiopenda lile unalolenga! Amani.

Anonymous said...

Tueleweshane basi. Sasa kama hivi vitanda vilitoka katika bohari ya madawa manake vilinunuliwa zamani. Sasa hizi kamba zote za nini kutuzuga kwamba Rais katoa million 250,au bohari ya madawa ndiyo inayowauzia muhimbili...? Ufahamu wangu ni mdogo hasa kuhusu mambo ya serikali. Nisaidieni nielewe nisiendelee kuwa Maimuna.

Anonymous said...

NAREJEA KICHWA CHA HABARI PESA ZA SHEREHE..NA VITANDA VYA MAGUFULI. Tueleweshane basi. Sasa kama hivi vitanda vilitoka katika bohari ya madawa manake vilinunuliwa zamani. Sasa hizi kamba zote za nini kutuzuga kwamba Rais katoa million 250,au bohari ya madawa ndiyo inayowauzia muhimbili...? Ufahamu wangu ni mdogo hasa kuhusu mambo ya serikali. Nisaidieni nielewe nisiendelee kuwa Maimuna.

Anonymous said...

umefika wakati sasa mheshimiwa magufuli anapobaini na kugundua uzembe mkubwa wa kutikisa nchi wahusika wawekwe hadharani na kufukuzwa kazi,pili hawa wahujumu uchumi wafikishwe mahakamani.sasa unalalamika unachukua hatua wezi,wazembe,waahujumu unawaacha waendelee na kazi uliona wapi hiyo.hapa kuna mawili,aidha kuacha kulalamika na kuendelea kuchukua hatua kimya kimya,yaani kuacha kuji-promote kisiasa AU kuchukua hatua INAYOTARAJIWA NA WANANCHI KWA KUFUKUZA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAHUSIKA WOTE.mwisho mhe.magufuli usiendelee kusubiri muondoe OMBENI SEFUE HAKUFAI HAPO IKULU.matatizo mengi ya utumishi legelege chanzo ni yeye,MFUKUZE.

Anonymous said...

Uwepo wa vifaa hivi katika bohari ya madawa (msd) haina maana kuwa vinatolewa bure.

Anonymous said...

Hakika ufahamu wako ni mdogo.kwanza tambua kuwa MSD haifanyi charity kwa kugawa vitu bure.

Anonymous said...

Msd ni idara ya serikali inayojiendesha kibiasha yenye majukumu ya kununu,kutunza na kusambaza madawa na vifaa vya hospitalini.Pointi hapa ni kuwa msd inajiendesha kubiashara na kwa taarifa yako mdaiwa mkubwa wa msd ni serikali.kumbuka mwaka jana msd ili sutisha huduma zk ktk hospitali za serikali kutokana na madeni.
Hivyo, YES pesa za Magufuli zimewezesha kupatikana vitanda hivyo.
Hongera sana JPM

Anonymous said...

AFUKUZWE KAZI OMBENI SEFUE.KAHAIBU SANA UCHUMI