ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 23, 2015

HATIMA YA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO KUAGWA JIJINI MWANZA KUAMULIWA KESHO NA MAHAKAMA\

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitoa taarifa kwa wananchi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Mmoja wa Mawakili wa Chadema John Mallya akitoa taarifa kesi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.

Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, ili kuiomba Mahakama hiyo kutengua zuio la kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, lililotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Katika kesi hiyo, Chadema inawakilishwa na Mawakili watatu ambao ni James Millya, John Mallya pamoja na Paul Kipeja ambapo mlalamikaji ni Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo.

Mahamaka hiyo chini ya Jaji Lameck Mlacha, imesikiliza malalamiko ya upande wa washtaki na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo imeamuru mlalamikiwa ambae ni Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali kupelekewa nyaraka za kesi hiyo kabla ya kusikiliza utetezi wao hapo kesho.

Mapema kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani hapo ili kujua hatima ya kesi hiyo, ambapo wamesema kitendo hicho kinaondoa dhana ya Rais John Pombe Magufuli, kuwa yeye ni rais wa wananchi wote wakati wao kama Chadema wananyimwa haki zao.

Licha ya Malalamiko hayo pamoja na ulinzi mkali wa polisi uliokuwa umetanda Mahakamani hapo, bado wafuasi wa Chadema hawakuondoka katika viunga vya Mahakama hiyo hadi pale Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe alipowasihi kurejea majumbani mwao hadi kesho kesi hiyo itakaposikilizwa tena.
  
Ni zaidi ya siku nane sasa tangu marehemu Alphonce Mawazo auawe kikatili Mkoani Geita na watu wasiojulikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni chuki za kisiasa ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.


Kesi ilisikilizwa katika Jengo la Mahakama ya Biashara lililopo katikati ya Jiji la Mwanza. Pichani ni mawakili wa Chadema wakielekea mahakamani huku kukiwa na umati wa wafuasi wa Chadema (Ukawa) pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema
Kesi ilisikilizwa katika Jengo la Mahakama ya Biashara lililopo katikati ya Jiji la Mwanza. Pichani ni mawakili wa Chadema wakielekea mahakamani huku kukiwa na umati wa wafuasi wa Chadema (Ukawa) pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo
Mmoja wa wafuasi wa Ukawa akilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani ili kujua hatima ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Chadema hii leo.

2 comments:

Anonymous said...

Hii ndio shida ya ku-politisize kila jambo.Siku hizi lika anaefariki basi mchawi wake lazima awe anatoka chama kinzani.Tufike mahali tuache ku polarize society between party' s lines.
Hata jambo ambalo kwa kawaida humalizwa kwa njia nyepesi linafanywa complicated kwasababu kuna politics ndani yake . please Stop thisssss.

Anonymous said...

Lakini nyie Chadema mnao ugonjwa gani jamani? Kampeni zilikwisha, msiwavuruge wananchi nyie viongozi wenye tamaa ya publicity. Watu wanataka kuendelea na maisha yao bila kusumbuliwa tena mpaka mwaka 2020.