ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 12, 2015

HUYU NDO MSICHANA ANAYE KIMEGA CHAMA CHA CHADEMA BAADA YA KUPEWA UBUNGE ...WANACHAMA WENGI WAPINGA


Zubeda Sakuru Msichana mdogo anayedaiwa kuihadaa Chadema kwamba kwao ni Ruvuma na kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa na huku ni mwenyeji wa Tanga, well, binafsi ninamfahamu kwa karibu sana ni Msichana ambaye amekuwa akiifanyia kazi Chadema kwa muda mrefu kwenye ofisi zao za Bunge na ni mtoto wa Mchezaji wa zamani maarufu sana wa Simba Adam Sakuru. 
Kwamba Viongozi wa Chadema wameteua kwa sababu ni kutoka Ruvuma hapana siamini kabisa, na the idea kwamba wanajaribu kuficha ukweli kwamba wamekuwa naye Ofisi zao kwa muda mrefu lakini wamemteua kwa kisingizio cha kuwakilisha Ruvuma ndipo panaponitia wasi wasi wanajaribu kuficha nini hasa? Swali langu kwa Chadema ni moja haya mambo madogo ya kuteuana Ubunge wa Viti Maalum mnataka kuuana hivi je mngeshika Ikulu ingekuwaje

4 comments:

Anonymous said...

Wangeshika ikulu mpaka hivi tunavyozungunza wangekuwa wanagombana. Mbowe angesema yeye anastahili kuwa waziri mkuu. Sumaye nae angesema mbowe hana uzoefu. Lisu kwa kujifanya mwanasheria wa chama angemwamimbia sumaye yeye sie mwanachama halisi wa chadema. Lowasa nae angeshurutisha lazima aekewe kibaka mwenzake sumaye awe msaidizi wake. Mbatia nae angesema kama raisi katoka chadema lazima nafasi ya waziri mkuu iende NCCR Mageuzi la sivyo patachimbika ilimradi hali ingelikuwa tete sana lol

Anonymous said...

Hizi ni njama za Chadema kwani wanajua Ruvuma ni ngome kuu ya CCM. Chadema can't flourish there, hivyo wanadhani huyu binti atawavutia vijana wa kingoni, thubutu! Anyway, Tikuwonee kamwali?

Anonymous said...

Acheni majungu.Hicho chama kuchukua mamluki mbona ndio kawaida yao.Hakikumegeka wakati Lowasa amepewa nafasi ya kugombea uraisi siku mmoja baada ya kujiunga nacho.Hakikumegeka wakati akina Sumaye,Masha, Kingunge walipochukuahatamu ndani ya chama bila hata ya kuwa wanachama.

Anonymous said...

Mbowe nae tumemchoka